Kumbukumbu 30 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 30:1-20

Mafanikio Baada Ya Kumgeukia Bwana

130:1 Kum 11:26; Law 26:40-45; Kum 4:32; 29:28; 1Fal 8:47Wakati baraka hizi zote pamoja na laana nilizoziweka mbele yako zitakapokujia, nawe ukazitafakari moyoni popote Bwana Mungu wako atakapokutawanya miongoni mwa mataifa, 230:2 Kum 4:29-30hapo wewe na watoto wako mtakapomrudia Bwana Mungu wako, na kumtii kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote kulingana na kila kitu ninachokuamuru leo, 330:3 Za 14:7; 53:6; 85:1; 126:4; Yer 30:18; 33:11; Eze 16:53; Yoe 3:1; Sef 2:7; Kum 13:17; Mwa 48:21; 11:4; Kum 4:27; Isa 11:11; Yer 12:15; 16:15; 26:4; 29:14; 48:47; 49:6ndipo Bwana Mungu wako atakapokurudisha kutoka utumwani na kukuhurumia, naye atakukusanya tena kutoka mataifa yote kule alikutawanya. 430:4 Isa 17:6; 24:13; 27:12; 40:11; 41:5; 49:5; 56:8; Eze 20:34, 41; 34:13; Za 19:6; Neh 1:8-9; Isa 11:12; 42:10; 43:6; 48:20; 62:11; Yer 31:8, 10; 50:2Hata kama umefukuziwa katika nchi ya mbali kiasi gani chini ya mbingu, kutoka huko Bwana Mungu wako atakukusanya na kukurudisha. 530:5 Yer 29:14; Kum 7:13Yeye Bwana atakurudisha katika nchi iliyokuwa mali ya baba zako, nawe utaimiliki. Naye atakufanya ufanikiwe sana na kukuzidisha kwa idadi kuliko baba zako. 630:6 Kum 6:24; 10:16; 6:5; Yer 32:29Bwana Mungu wako ataitahiri mioyo yenu na mioyo ya wazao wenu ili mweze kumpenda kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote ukaishi. 730:7 Mwa 12:3; Kum 7:15Bwana Mungu wako ataweka laana hizi zote juu ya adui zako ambao wanakuchukia na kukutesa. 8Utamtii tena Bwana na kuzishika amri zake zote ninazokupa leo. 930:9 Yer 1:10; 24:6; 31:28; 32:41; 42:10; 45:4; Kum 28:63; Eze 34:27; Yer 32:41; 33:9; Sef 3:17; Lk 15:6, 10, 32; Yn 15; 11Ndipo Bwana Mungu wako atakapokufanikisha sana katika kazi zote za mikono yako na katika uzao wa tumbo lako, wadogo wa mifugo yako na mazao ya nchi yako. Bwana atakufurahia tena na kukufanikisha, kama alivyowafurahia baba zako, 1030:10 Kum 28:61; 4:29kama ukimtii Bwana Mungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake ambayo yameandikwa katika Kitabu hiki cha Sheria, na kumgeukia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote.

Uzima Na Mauti

1130:11 Za 19:8; Isa 45:19-23; 63:1Ninachokuagiza leo sio kigumu sana kwako au usichokiweza. 1230:12 Mit 30:4; Rum 10:6; Yn 3:13Hakiko juu mbinguni, ili uulize, “Ni nani atakayepanda mbinguni kukileta na kututangazia ili tuweze kutii?” 1330:13 Ay 28:14; Rum 10:7Wala hakiko ngʼambo ya bahari, ili uulize, “Ni nani atakayevuka bahari kwenda kukichukua na kututangazia ili tupate kutii?” 1430:14 Kum 6:6; Rum 10:8La hasha! Lile neno liko karibu sana nawe; liko kinywani mwako na ndani ya moyo wako ili uweze kulitii.

1530:15 Mit 10:16; 11:9; 12:28; 3:1-2; Kum 28:11; Za 25:13; 106:5; Mwa 2:17; Kum 11:26Tazama, naweka mbele yako leo uzima na mafanikio, mauti na maangamizo. 1630:16 Kum 6:5; 4:1; 32:17; Neh 9:29Ninakuamuru leo kwamba umpende Bwana Mungu wako, utembee katika njia zake, na kutunza maagizo yake, amri na sheria zake; ndipo utakapoishi na kuongezeka, naye Bwana Mungu wako atakubariki katika nchi unayoingia kuimiliki.

17Lakini kama moyo wako ukigeukia mbali ukawa huna utii, kama umevutwa kuisujudia miungu mingine na kuiabudu, 1830:18 Kum 8:19nakutangazia leo hii kwamba hakika utaangamizwa. Hutaishi maisha marefu katika nchi unayovuka Yordani kuiingia na kuimiliki.

1930:19 Kum 4:26; 11:26Leo ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yako kwamba nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana. Basi sasa chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kuishi, 2030:20 Kum 6:5; 4:1; 8:3; 32:47; 10:20; Za 27:1; Yn 5:26; Mdo 17:28; Mit 3:22; Mwa 12:7; Za 37:3na ili upate kumpenda Bwana Mungu wako, uisikilize sauti yake na kuambatana naye. Kwa kuwa Bwana ndiye uzima wako, na atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi aliyoapa kuwapa baba zako Abrahamu, Isaki na Yakobo.