Kumbukumbu 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 3:1-29

Kushindwa Kwa Ogu Mfalme Wa Bashani

(Hesabu 21:31-35)

13:1 Hes 21:33; 32:19Kisha tukageuka tukakwea kufuata njia iliyoelekea Bashani, Ogu mfalme wa Bashani akaondoka na jeshi lake lote kupigana na sisi huko Edrei. 23:2 Yos 10:8; 2Fal 19:6; Isa 7:4Bwana akaniambia, “Usimwogope kwa kuwa nimekwisha mkabidhi mikononi mwako pamoja na jeshi lake lote na nchi yake. Umfanyie sawasawa na ulivyomfanyia Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.”

33:3 Hes 21:24; 21:35Hivyo Bwana Mungu wetu pia akamweka Ogu mfalme wa Bashani pamoja na jeshi lake lote mikononi mwetu. Tuliwaangamiza wote, hakubakia hata mmoja. 43:4 Hes 21:24, 33; 1Fal 4:13Wakati huo tuliteka miji yake yote. Hakuna mji hata mmoja kati ya ile sitini ambao hatukuuteka, yaani eneo lote la Argobu, utawala wa Mfalme Ogu katika Bashani. 5Miji yote hii ilijengewa ngome zenye kuta ndefu zenye malango na makomeo, pia kulikuwako na vijiji vingi ambavyo havikujengewa kuta. 63:6 Kum 2:24; Za 135:10-12; 136:19-21Tuliwaangamiza kabisa, kama tulivyomfanyia Sihoni mfalme wa Heshboni, tukiangamiza kila mji, yaani wanaume, wanawake na watoto. 73:7 Kum 2:35Lakini wanyama wote wa kufuga pamoja na nyara kutoka kwenye miji yao tulichukua vikawa vyetu.

83:8 Hes 32:33; Yos 13:8-12; Kum 4:48; Yos 11:3; 12:1; 13:5; Amu 3:3; 1Nya 5:23; Za 42:6; 89:12; 133:3; Wim 4:8Hivyo kwa wakati huo tukachukua kutoka kwa wafalme hawa wawili wa Waamori nchi ya mashariki ya Yordani, kutoka Bonde la Arnoni mpaka kufika kwenye Mlima Hermoni. 93:9 Za 29:6; 89:12; 1Nya 5:23; Wim 4:8; Eze 27:5; Kum 4:48(Wasidoni huuita mlima huo Sirioni, nao Waamori huuita Seniri.) 103:10 Yos 12:5; 13:11; 1Nya 5:11; Kum 4:49Tuliteka miji yote kwenye uwanda wa juu, Gileadi yote, Bashani yote mpaka kufika Saleka na Edrei, miji ya utawala wa Ogu huko Bashani. 113:11 Mwa 14:5; Yos 13:25; 15:60; 2Sam 11:1; 12:26; 17:27; 1Nya 20:7; Yer 49:2; Eze 21:20; 25:5; Amo 1:14; 2:9(Mfalme Ogu wa Bashani ndiye peke yake aliyesalia miongoni mwa mabaki ya Warefai. Kitanda chake kilikuwa cha chuma chenye urefu wa dhiraa tisa3:11 Dhiraa tisa ni sawa na mita 4. na upana wa dhiraa nne.3:11 Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8. Mpaka sasa kinaweza kuonekana katika mji wa Waamoni wa Raba.)

Mgawanyo Wa Nchi Mashariki Ya Yordani

(Hesabu 32:1-42)

123:12 Kum 2:36; Hes 32:32-38; Yos 13:8-13Katika nchi tuliyoiteka wakati ule, niliwapa kabila la Reubeni na Gadi eneo lililoko kaskazini la Aroeri kando ya Bonde la Arnoni, na nusu ya eneo la milima ya Gileadi, pamoja na miji yake. 133:13 Kum 29:8; Mwa 14:5Kisha nusu ya kabila la Manase niliwapa sehemu ya Gileadi iliyobaki pamoja na Bashani yote, ambayo ilikuwa utawala wa Ogu. (Eneo lote la Argobu katika Bashani lilikuwa linajulikana kama nchi ya Warefai. 143:14 Hes 32:41; Yos 12:5; 13:11-13; 2Sam 10:6; 23:34; 2Fal 25:23; 1Nya 4:19; Yer 40:8; Yos 19:46-47; Za 49:11; 1Nya 2:22Yairi, mzao wa kabila la Manase, alichukua eneo lote la nchi ya Argobu hadi kufikia mpaka wa Wageshuri na Wamaaka, ukaitwa kwa jina lake; kwa hiyo mpaka leo hii Bashani inaitwa Hawoth-Yairi.) 153:15 Mwa 50:23; Hes 32:39-40Nikampa Makiri nchi ya Gileadi. 163:16 Hes 21:24; 2Sam 24:5; Hes 21:24Lakini niliwapa Wareubeni na Wagadi eneo kuanzia Gileadi hadi Bonde la Arnoni (katikati ya bonde ulikuwa ndio mpaka), kuelekea mpaka Mto Yaboki, ambao ndio mpaka wa Waamoni. 173:17 2Sam 2:29; 4:7; Eze 47:8; Hes 34:11; 14:3; Yos 12:3; 13:27Kwa upande wa magharibi mpaka wao ulikuwa Yordani katika Araba, toka ziwa Galilaya hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), kwenye miteremko ya Pisga upande wa mashariki.

183:18 Yos 1:13; Hes 32:17Wakati huo nilikuamuru: “Bwana Mungu wako amekupa nchi hii uimiliki. Lakini ni lazima wanaume wenu wote wenye uwezo, wakiwa wamejiandaa tayari kwa vita, wavuke ngʼambo wakiwatangulia ndugu zako Waisraeli. 193:19 Yos 1:14; Hes 32:16Lakini wake zenu, watoto wenu na mifugo yenu (kwani najua mnayo mifugo mingi) wanaweza kukaa katika miji niliyowapa, 203:20 Yos 22:4mpaka hapo Bwana atakapowapa ndugu zenu kupumzika kama alivyowapa ninyi, wao pia wamiliki ile nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, ngʼambo ya Yordani. Baada ya hapo, kila mmoja wenu anaweza kurudi kwenye milki niliyowapa.”

Mose Akatazwa Kuvuka Yordani

21Wakati huo nilimwamuru Yoshua, “Umejionea kwa macho yako mwenyewe yale yote ambayo Bwana Mungu wenu amewafanyia wafalme hawa wawili. Bwana atazifanyia falme zote huko mnakokwenda vivyo hivyo. 223:22 Kum 1:29; 7:18; 20:4; 31:6; 2Nya 32:8; Za 23:4; Isa 41:10; Kut 14:143:22 Yos 23:10Msiwaogope, Bwana Mungu wenu atapigana kwa ajili yenu.”

233:23 Kum 1:37; 31:2; 32:52; 34:4Wakati huo nilimsihi Bwana: 243:24 Kum 5:24; 11:2; 32:3; Kut 8:10; Za 71:16; 86:8; 106:2; 145:12; 150:2; 2Sam 7:22; Neh 9:32; Yer 32:18-21; Kut 15:11“Ee Bwana Mwenyezi, umemwonyesha mtumishi wako ukuu wako na mkono wako wenye uweza. Kwa kuwa ni mungu yupi aliye mbinguni au duniani anayeweza kufanya kazi na matendo makuu kama ufanyayo wewe? 253:25 Kum 4:25; 1:7; Yos 1:4; 9:1; 11:17; 12:7; 13:5; Amu 3:3; 9:13; 1Fal 4:33Acha niende nikaione hiyo nchi nzuri ngʼambo ya Yordani, ile nchi nzuri ya vilima na Lebanoni.”

263:26 Kum 1:37; 31:2Lakini kwa sababu yenu Bwana alinikasirikia na hakutaka kunisikiliza. Bwana aliniambia, “Hilo latosha; usiseme nami jambo hili tena. 273:27 Hes 21:20; 27:12; Mwa 13:14; Hes 20:12; Kum 32:52Kwea juu ya kilele cha Pisga uangalie magharibi, kaskazini, kusini na mashariki. Iangalie hiyo nchi kwa macho yako, kwa vile wewe hutavuka Yordani. 283:28 Hes 27:18-23; Kum 31:7; 1:38; 31:3-23Lakini mwagize Yoshua, mtie moyo na umtie nguvu, kwa kuwa yeye atawaongoza watu hawa hadi ngʼambo na kuwarithisha nchi utakayoiona.” 293:29 Hes 23:28; Kum 4:46; 34:6; Yos 13:20Kwa hiyo tulikaa kwenye bonde karibu na Beth-Peori.