Kumbukumbu 29 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 29:1-29

Kufanya Upya Agano

129:1 Law 7:38; Kut 3:1; Kum 5:2-3Haya ndiyo maneno ya Agano Bwana aliyomwagiza Mose kufanya na Waisraeli huko Moabu, kuwa nyongeza ya Agano alilofanya nao huko Horebu.

229:2 Kut 19:4Mose akawaita Waisraeli wote akawaambia:

Macho yenu yameona yale yote Bwana aliyofanya kwa Mfalme Farao huko Misri, kwa maafisa wake wote na kwa nchi yake yote. 329:3 Kum 4:34; 7:19Kwa macho yenu wenyewe mliona yale majaribu makubwa, ishara zile za miujiza na maajabu makubwa. 429:4 Isa 6:10; 32:3; 48:8; Yer 5:21; Eze 12:2; Mt 13:15; Rum 11:8; Efe 4:18; Mdo 28:26-27; Za 13:3; 19:8; Yn 8:43; Efe 1:18; 2The 2:11Lakini mpaka leo Bwana hajawapa akili ya kuelewa au macho yanayoona au masikio yanayosikia. 529:5 Kum 8:2-4Kwa muda wa miaka arobaini niliyowaongoza jangwani, nguo zenu hazikuchakaa, wala viatu miguuni mwenu. 629:6 Law 10:9; Kum 8:4; Kut 16:12; Neh 9:15; Za 78:24Hamkula mkate na hamkunywa divai wala kileo chochote. Nilifanya hivi ili mpate kujua kuwa mimi ndimi Bwana Mungu wenu.

729:7 Hes 21:25-26; 21:21-24, 33-35; Kum 2:26–3:11Wakati mlipofika mahali hapa, Sihoni mfalme wa Heshboni na Ogu mfalme wa Bashani walikuja kupigana dhidi yetu, lakini tuliwashinda. 829:8 Za 78:55; 135:12; 136:22; Hes 32:33; Kum 3:12-13Tuliichukua nchi yao na kuwapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kama urithi wao.

929:9 Kum 4:6; Yos 1:7; Kut 19:5; Za 25:10; 103:18; 2Nya 31:21; 1Fal 2:3; Yos 1:8Fuateni kwa bidii masharti ya Agano hili, ili kwamba mweze kustawi katika kila kitu mnachofanya. 10Ninyi nyote leo mnasimama mbele za Bwana Mungu wenu; mkiwa viongozi na wakuu wenu, wazee na maafisa wenu, na wanaume wengine wote wa Israeli, 1129:11 Yos 9:21, 23, 27; 1Nya 20:3pamoja na watoto wenu, wake zenu na pia wageni waishio katika kambi zenu wanaowapasulia kuni na kuwachotea maji. 12Mnasimama hapa ili kufanya Agano na Bwana Mungu wenu, Agano ambalo Mungu analifanya nanyi siku hii ya leo na kulitia muhuri kwa kiapo, 1329:13 Mwa 6:18; Kut 6:7; 19:6; Mwa 17:7kuwathibitisha ninyi siku hii ya leo kama taifa lake, ili aweze kuwa Mungu wenu kama alivyowaahidi na kama alivyowaapia baba zenu Abrahamu, Isaki na Yakobo. 1429:14 Kut 19:5; Isa 59:21; Yer 31:31; 32:40; 50:5; Eze 16:62; 37:26; Ebr 8:7-8Ninafanya Agano hili pamoja na kiapo chake, sio na ninyi tu 1529:15 Mwa 6:18; Mdo 2:39mnaosimama hapa na sisi leo mbele za Bwana Mungu wetu, bali pia pamoja na wale ambao hawapo hapa leo.

16Ninyi wenyewe mnajua jinsi tulivyoishi nchini Misri na jinsi tulivyopita katikati ya nchi mpaka tukafika hapa. 1729:17 Kut 20:23; Kum 4:28; 28:36Mliona miongoni mwao vinyago vyao vya kuchukiza na sanamu za miti na mawe, za fedha na dhahabu. 1829:18 Kum 13:6; 11:16; Ebr 12:15Hakikisheni kwamba hakuna mwanaume au mwanamke, ukoo au kabila miongoni mwenu leo ambalo moyo wake utamwacha Bwana Mungu wetu, kwenda kuabudu miungu ya mataifa hayo. Hakikisheni hakuna mzizi miongoni mwenu unaotoa sumu chungu ya namna hii.

1929:19 Za 72:17; Isa 65:16; Za 36:2; 14:1; Hes 15:39; Yer 7:24; Ay 15:16; 34:7; Efe 4:19Wakati mtu wa namna hii asikiapo maneno ya kiapo hiki, hujibariki mwenyewe na kisha hufikiri, “Nitakuwa salama, hata kama nikiendelea kuifuata njia yangu mwenyewe.” Hili litaleta maafa juu ya nchi iliyonyeshewa sawasawa na nchi kame. 2029:20 Kut 23:21; 34:4; Eze 23:25; Sef 1:18; Za 74:1; 79:5; 80:4; Eze 36:5; 2Fal 13:23; 14:27; Ufu 3:5; Kut 32:33Bwana kamwe hatakuwa radhi kumsamehe, ghadhabu na wivu wa Mungu vitawaka dhidi ya mtu huyo. Laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki zitamwangukia na Bwana atafuta jina lake chini ya mbingu. 2129:21 Kum 28:61; 32:23; Eze 7:26; Mt 24:51Bwana atamtwaa peke yake kutoka makabila ya Israeli kwa maangamizo, kulingana na laana zote za Agano zilizoandikwa kwenye Kitabu hiki cha Sheria.

2229:22 Yer 19:8; 49:17; 50:13Watoto wako watakaofuata baada yako katika vizazi vya baadaye na wageni ambao watakuja kutoka nchi za mbali, wataona maafa, yaliyoipata nchi na magonjwa ambayo Bwana aliyaleta juu yake. 2329:23 Isa 1:7; 6:11; 9:18; 64:10; Yer 12:11; 44:2; 6; Mik 5:11; Mwa 13:10; Eze 47:11; Mwa 19:24-25; Sef 2:9; Mt 10:15; Rum 9:29; Mwa 14:8; Yer 17:6Nchi yote itakuwa jaa linaloungua la chumvi na kiberiti: hakutakuwa kilichopandwa, hakutakuwa kinachochipua, wala hakutakuwa mimea inayoota juu yake. Itakuwa kama maangamizo ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, ambazo Bwana aliangamiza kwa hasira kali. 2429:24 1Fal 9:6; 2Nya 36:19; Yer 16:10; 22:8-9; 52:13Mataifa yote yatauliza: “Kwa nini Bwana amefanya hivi juu ya nchi hii? Kwa nini hasira hii kali ikawaka?”

2529:25 2Fal 17:23; 2Nya 36:21Na jibu litakuwa: “Ni kwa sababu watu hawa waliacha Agano la Bwana, Mungu wa baba zao, Agano alilofanya nao wakati alipowatoa katika nchi ya Misri. 26Walienda zao na kuabudu miungu mingine na kuisujudia, miungu wasioijua, miungu ambayo Mungu hakuwapa. 2729:27 Kum 28:15; Dan 9:11-14Kwa hiyo hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya nchi hii, hivyo Mungu akaleta juu yake laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki. 2829:28 Za 7:11; 1Fal 14:15; 2Nya 7:20; Za 9:6; 52:5; Mit 2:22; Yer 12:14; 31:28; 42:10; Eze 19:12Katika hasira kali na katika ghadhabu kuu Bwana aliwangʼoa kutoka nchi yao na kuwasukumia katika nchi nyingine, kama ilivyo sasa.”

2929:29 Mdo 1:7; Yn 5:39; Mdo 17:11; 2Tim 3:16; Ay 11:6; 7; Mit 3:32; Yer 23:18; Amo 3:7; Za 19:7; Lk 16:29; 2Tim 3:16; Mdo 17; 11Mambo ya siri ni ya Bwana Mungu wetu, bali yaliyofunuliwa ni yetu na watoto wetu milele, ili tuweze kuyafanya maneno yote ya sheria hii.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

申命记 29:1-29

在摩押立约

1耶和华除了与以色列人在何烈山立约外,还在摩押吩咐摩西以色列人立以下的约。

2摩西召来所有以色列人,对他们说:“你们曾亲眼见过耶和华在埃及怎样对付法老及其臣仆和国民, 3亲眼看见祂怎样降下巨大的灾难,行伟大的神迹奇事。 4但耶和华至今还没有赐给你们能明白的心、能看见的眼、能听清的耳。 5四十年来,耶和华领你们走过旷野,你们身上的衣服没有穿破,脚上的鞋没有穿坏; 6你们没有吃饼,也没有喝淡酒和烈酒。这是为了让你们知道耶和华是你们的上帝。 7我们来到这里的时候,希实本西宏巴珊都出来攻击我们,我们击败了他们, 8并将占领的土地分给吕便支派、迦得支派和玛拿西半个支派作产业。 9所以,你们要谨遵这约上的话,以便凡事顺利。

10“今天,你们全都站在你们的上帝耶和华面前,包括你们的族长、长老、官员、所有以色列男子、 11你们的孩子、妻子和寄居在你们营中为你们砍柴挑水的外族人, 12为要接受你们的上帝耶和华今天与你们立的誓约。 13这样,祂今天将确立你们作祂的子民、祂作你们的上帝,正如祂对你们的应许和对你们祖先亚伯拉罕以撒雅各的誓言。 14耶和华的这誓约不仅是与你们立的, 15也是与今天一同站在我们的上帝耶和华面前的人,以及今天不在这里的人29:15 “今天不在这里的人”或译“我们将来的子孙”。立的。

16“你们知道我们如何在埃及生活,也知道我们如何穿越列国来到这里。 17你们也见过他们可憎的木、石、金、银偶像。 18你们中间,不论男人或女人,家族或支派,切不可有人背弃我们的上帝耶和华,去祭拜列国的神明,你们中间切不可有残根长出苦毒的果实, 19免得有人听了这誓言后,心存侥幸地说,‘即使我一意孤行,连累他人,也必平安无事。’ 20耶和华绝不会赦免这样的人,祂必向这样的人发烈怒和义愤,使记在这书上的一切咒诅临到他身上,从世上抹去他的名字。 21耶和华必把他从以色列各支派中隔离出来,使他按律法书上约中的一切咒诅受惩罚。

22“你们的子孙后代和从远方来的外族人,必看见耶和华降在这地方的灾祸和疾病。 23遍地将是硫磺和盐,无法耕种,寸草不生,如同耶和华盛怒之下毁灭的所多玛蛾摩拉押玛洗扁24万国必问,‘耶和华为什么要这样对待这地方?祂为什么大发烈怒?’ 25必有人回答说,‘因为这地方的人背弃了他们祖先的上帝耶和华领他们出埃及时与他们所立的约, 26去供奉其他神明,祭拜他们不认识、也非耶和华分派给他们的神明。 27因此,耶和华向这片土地发怒,把这书上写的一切咒诅都降在这里。 28耶和华在怒气、义愤和烈怒中把他们从这地方连根拔起,扔到别的地方,正如今日的情形。’

29“奥秘的事属于我们的上帝耶和华,只有显明的事永远属于我们和我们的子孙,以便我们可以遵守这律法上的一切话。”