Kumbukumbu 28 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 28:1-68

Baraka Za Utiifu

(Walawi 26:3-13; Kumbukumbu 7:12-24)

128:1 Kum 15:5; Law 26:3; Hes 24:7; Kum 26:19; Kut 15:26; Za 106:3; 111:10; Isa 1:19; 3:10; Yer 11:4; 12:16; 1Nya 14:2; Rum 2:10Kama ukimtii Bwana Mungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa bidii, Bwana Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia. 228:2 Yer 32:24; Zek 1:6Baraka hizi zote zitakuja juu yako na kukupata, kama ukimtii Bwana Mungu wako:

328:3 Za 144:15; Mwa 39:5; Za 128:1-4Utabarikiwa mjini na utabarikiwa mashambani.

428:4 Mwa 49:25; Kum 8:18; Mit 10:22; 1Tim 4:8Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na wanyama wako wachanga wa kufugwa, yaani ndama wa makundi yako ya ngʼombe, na wana-kondoo wa makundi yako.

5Kapu lako na vyombo vyako vya kukandia vitabarikiwa.

628:6 Za 121:8Utabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo.

728:7 2Nya 6:34; Law 26:8, 17Bwana atasababisha adui wainukao dhidi yako kushindwa mbele yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.

828:8 Kum 15:4Bwana ataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu utakachogusa kwa mkono wako. Bwana Mungu wako atakubariki katika nchi anayokupa.

928:9 Kut 19:6; Law 26:3; Kum 7:6Bwana atakufanya kuwa taifa lake takatifu, kama alivyokuahidi kwa kiapo, kama ukishika maagizo ya Bwana Mungu wako na kwenda katika njia zake. 1028:10 Hes 6:27; 1Fal 8:43; Yer 25:29; Dan 9:18; 2Nya 7:14Kisha mataifa yote ya dunia wataona kuwa unaitwa kwa jina la Bwana, nao watakuogopa. 1128:11 Kum 30:9; Mwa 30:27; Mit 10:22Bwana atakupa kustawi kwa wingi, katika tunda la uzao wa tumbo lako, katika wanyama wachanga wa mifugo yako na katika mazao ya ardhi yako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwapa.

1228:12 Ay 38:22; Za 135:7; Yer 10:13; 51:16; Za 65:11; 58:10; Yer 31:12; Law 26:4; 1Fal 8:35-36; 18:1; Za 104:13; Isa 5:6; 30:23; 32:20; 61:9; 65:23; Yer 32:38-41; Mal 3:12; Law 25:19; Kum 15:3-6; Eze 34:26Bwana atafungua mbingu, ghala zake za baraka, kukupa mvua kwa majira yake na kubariki kazi zako zote za mikono yako. Utakopesha mataifa mengi lakini hutakopa kwa yeyote. 1328:13 Yer 11:6; Kum 26:19Bwana atakufanya kichwa, wala si mkia. Kama utazingatia maagizo ya Bwana Mungu wako ninayokupa siku hii ya leo na kuyafuata kwa bidii, daima utakuwa juu, kamwe hutakuwa chini. 1428:14 Kum 5:32; Yos 1:7Usihalifu amri zangu zozote ninazokupa leo, kwa kwenda kuume au kushoto, kwa kufuata miungu mingine na kuitumikia.

Laana Kwa Kutokutii

(Walawi 26:14-46)

1528:15 1Fal 9:6; 2Nya 7:19; Kum 27:26; 27:26; Yos 23:15; 2Nya 12:5; Dan 9:11; Mal 2:2Hata hivyo, kama hutamtii Bwana Mungu wako na kuzishika kwa bidii amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata:

16Utalaaniwa mjini na utalaaniwa mashambani.

17Kapu lako na chombo chako cha kukandia kitalaaniwa.

1828:18 Isa 3:1; Hab 3:17Uzao wa tumbo lako utalaaniwa, mazao ya ardhi yako, ndama wa makundi yako ya ngʼombe na wana-kondoo wa makundi yako.

19Utalaaniwa uingiapo na utokapo.

2028:20 Law 26:16; Yer 42:18; Mal 2:2; 3:9; 4:6; Za 39:11; 76:6; 80:16; Isa 17:13; 51:20; 54:9; 66:15; Eze 5:15; Kum 4:26; Kut 32:22Bwana ataleta laana juu yako, fadhaa na kukaripiwa katika kila kitu unachokigusa kwa mkono wako, mpaka uwe umeharibiwa na kuangamizwa ghafula kwa ajili ya maovu uliyoyafanya kwa kumwacha yeye. 2128:21 Law 26:25; Hes 14:12; Yer 24:10; Amo 4:10Bwana atakupiga kwa magonjwa mpaka akuangamize kutoka nchi unayoingia kuimiliki. 2228:22 Kum 32:24; Law 26:16; 2Fal 8:1; Ay 12:15; Za 105:16; Yer 14:1; Hag 1:11; Mal 3:9; Hag 2:17; Law 26:25; Kum 4:26; Amo 4:9Bwana atakupiga kwa magonjwa ya kudhoofisha, kwa homa na kuwashwa, hari na kwa ukame, kutu na kuwa na uchungu ambavyo vitakupiga mpaka uangamie.

2328:23 Law 26:19Anga juu yako itakuwa shaba, na ardhi chini yako itakuwa chuma. 2428:24 Law 26:19; Kum 11:17; 1Fal 8:35; 17:1; Isa 5:6; Yer 14:1; Hag 1:10Bwana atafanya mvua ya nchi yako kuwa mavumbi na mchanga; vitakujia kutoka angani mpaka uangamie.

2528:25 1Sam 4:10; Za 78:62; Law 26:17; 2Nya 29:8; 30:7; Yer 15:4; 24:9; 26:6; 29:18; 44:12; Eze 23:46Bwana atakufanya ushindwe mbele ya adui zako. Utawajia kwa njia moja lakini utawakimbia mbele yao kwa njia saba, nawe utakuwa kitu cha kuchukiza kwa falme zote za dunia. 2628:26 Mwa 40:19; Za 79:2; Isa 18:6; Yer 7:33; 12:9; 15:2; 16:4; 19:7; 34:20Mizoga yenu itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi, wala hapatakuwepo mtu yeyote wa kuwafukuza. 2728:27 Kum 7:15; 1Sam 5:6Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri na kwa vidonda vitokavyo usaha na kuwashwa, ambako huwezi kuponywa. 28Bwana atakupiga kwa wazimu, upofu na kuchanganyikiwa kwa akili. 2928:29 Mwa 19:11; Kut 10:21; Ay 5:14; 12:25; 24:13; 38:15; Isa 59:10; Amu 3:9; 2Fal 13:5; Es 4:14; Isa 19:20; 43:11; Hos 13:4; Oba 1:21Wakati wa adhuhuri utapapasapapasa huku na huko kama mtu kipofu katika giza. Hutafanikiwa katika lolote ufanyalo; siku baada ya siku utaonewa na kunyangʼanywa, wala hakuna yeyote atakayekuokoa.

3028:30 Ay 31:10; Isa 65:22; Amo 5:11; Yer 12:13; 8:10Utaposa mke, lakini mtu mwingine atakutana naye kimwili. Utajenga nyumba, lakini hutaishi ndani yake. Utapanda shamba la mizabibu, lakini hutakula matunda yake. 31Ngʼombe wako atachinjwa mbele ya macho yako lakini hutakula nyama yake. Punda wako atachukuliwa kwa nguvu kutoka kwako wala hatarudishwa. Kondoo wako watapewa adui zako, wala hakuna mtu yeyote wa kuwaokoa. 32Wanao na binti zako watatolewa kwa mataifa mengine, nawe utayachosha macho yako ukiwatazamia siku baada ya siku, hutakuwa na nguvu kuinua mkono. 3328:33 Yer 5:15-17; Eze 25:4Taifa usilolijua watakula mazao ya nchi yako na taabu ya kazi yako, hutakuwa na chochote, bali kuonewa kikatili siku zako zote. 34Vitu utakavyoviona kwa macho yako vitakufanya wazimu. 3528:35 Kum 7:15; Ufu 16:2; Ay 2:7; 7:5; 13:28; 30:17; Isa 1:6Bwana atayapiga magoti yako na miguu yako kwa majipu yenye maumivu makali yasiyoponyeka, yakienea kutoka nyayo za miguu yako hadi utosini.

3628:36 1Sam 12:25; Kum 4:27; 2Fal 24:14; 25:7-11; 2Nya 33:11; 36:21; Ezr 5:12; Yer 15:14; 16:13; 27:20; 29:1-9; 52:28; Mao 1:3; Kum 4:28Bwana atakupeleka wewe na mfalme uliyemweka juu yako uende kwenye taifa ambalo hukulijua wewe wala baba zako. Huko utaabudu miungu mingine, miungu ya miti na mawe. 3728:37 Yer 42:18; Eze 5:15; Za 22:7; 39:8; 44:13; 64:8; Yer 18:16; 48:27; Mik 6:16; 2Nya 7:20; Ezr 9:7; Yer 44:8; 1Fal 9:7; Za 44:14; Yer 19:8; 24:9; 25:9, 18; 29:18; Mao 2:15Utakuwa kitu cha kuchukiza, tena kitu cha kudharauliwa na kudhihakiwa kwa mataifa yote huko Bwana atakakokupeleka.

3828:38 Law 26:20; Za 129:7; Isa 5:10; Yer 12:13; Hos 8:7; Mik 6:15; Hag 1:6-9; 2:16; Kut 10:4; 10:15; Yoe 1:4Utapanda mbegu nyingi katika shamba lakini utavuna haba, kwa sababu nzige watazila. 3928:39 Law 10:9; Yoe 1:4; 2:25; Mal 3:11; Isa 5:10; 17:10-11; Sef 1:13Utapanda mashamba ya mizabibu na kuyapalilia, lakini hutakunywa divai yake wala hutakusanya zabibu, kwa sababu wadudu watazila. 4028:40 Yer 11:16; Mik 6:15Utakuwa na mizeituni katika nchi yako yote, lakini hutatumia hayo mafuta yake, kwa sababu zeituni zitapukutika. 41Utakuwa na wana na binti lakini hawatakuwa nawe, kwa sababu watachukuliwa mateka. 4228:42 Amu 6:5; 7:12; Yer 46:23Makundi ya nzige yatavamia miti yako yote na mazao ya nchi yako.

43Mgeni anayeishi miongoni mwako atainuka juu zaidi na zaidi kuliko wewe, lakini wewe utashuka chini zaidi na zaidi. 4428:44 Kum 26:19Yeye atakukopesha, lakini wewe hutamkopesha. Yeye atakuwa kichwa, lakini wewe utakuwa mkia.

4528:45 Kut 15:9; Kum 4:25-26Laana hizi zote zitakuja juu yako. Zitakufuatia na kukupata mpaka uangamizwe, kwa sababu hukumtii Bwana Mungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake aliyokupa. 4628:46 Hes 16:38; Za 71:7; Isa 8:18; 20:3; Eze 5:15; Zek 3Zitakuwa ishara na ajabu kwako na kwa wazao wako milele. 4728:47 Kum 10:12; Law 23:20; Neh 9:35; 9:35-37Kwa sababu hukumtumikia Bwana Mungu wako kwa furaha na kwa moyo wakati wa kufanikiwa kwako, 4828:48 Yer 14:3; Mao 4:4; Yer 28:13-14; Mwa 49:8; Isa 47:6; Yer 27:12; 28:14; Mt 11:29kwa hiyo katika njaa na kiu, katika uchi na umaskini wa kutisha, utawatumikia adui ambao Bwana atawatuma dhidi yako. Yeye ataweka nira ya chuma shingoni mwako hadi amekwisha kukuangamiza.

4928:49 Law 26:44; Isa 5:26-30; 7:18-20; 39:3; Yer 4:16; 5:15; 6:22; 25:32; 31:8; Hab 1:6; 2Sam 1:23; Yer 4:13; 48:40; 49:22; Mao 4:19; Eze 17:3; Hos 8:1; Mwa 11:7; 1Kor 14:21Bwana ataleta taifa dhidi yako kutoka mbali, kutoka miisho ya dunia, kama tai ashukiavyo mawindo chini, taifa ambalo hutaijua lugha yake, 5028:50 Isa 47:6taifa lenye uso mkali lisilojali wazee wala kuwahurumia vijana. 5128:51 Za 4:7; Isa 36:17; Hag 1:11; Hes 18:12; Amu 6:428:51 Isa 1:7; 62:8; Yer 5:15-17Watakula wadogo wa mifugo yako na mazao ya nchi yako mpaka umeangamia. Hawatakuachia nafaka, divai mpya au mafuta, wala ndama wowote wa kundi lako au wana-kondoo wa kundi lako mpaka umekuwa magofu. 5228:52 2Fal 6:24; Yer 10:18; Eze 1:10; Sef 1:14-17Nao wataizingira miji yote katika nchi yako mpaka kuta ndefu za ngome ambazo unazitegemea zimeanguka. Watazingira miji yote katika nchi ambayo Bwana Mungu wako anakupa.

5328:53 Law 26:29; 2Fal 6:28-29; Mao 2:20; 4:10; Yer 19:9Utakula uzao wa tumbo lako, nyama ya wana wako na binti zako ambao Bwana Mungu wako amekupa, kwa sababu ya mateso yale adui zako watakayokuletea wakati wa kukuzingira. 54Hata yule mtu muungwana sana na makini miongoni mwako hatakuwa na huruma kwa ndugu yake mwenyewe au kwa mke ampendaye au watoto wake waliosalia, 5528:55 2Fal 6:29naye hatampa hata mmoja wao nyama ya watoto wake ambao anawala. Kwa kuwa hakuna kitu kingine kilichosalia kwake katika mazingirwa makali ambayo adui yako watakuletea kwa miji yako yote. 5628:56 Isa 47:1; Mao 4:10Mwanamke ambaye ni muungwana sana na makini miongoni mwako, yaani ambaye ni makini sana na muungwana kiasi kwamba asingethubutu kugusa ardhi kwa wayo wa mguu wake, yeye atakuwa mchoyo kwa mume ampendaye na mwanawe mwenyewe au binti yake, 5728:57 Kum 28:53kondoo wa nyuma kutoka kwenye tumbo lake na watoto anaowazaa. Kwa kuwa anakusudia kuwala kwa siri wakati wa kuzingirwa na katika taabu zile ambazo adui yako atazileta juu yako na miji yako.

5828:58 Kum 31:24; Za 96:4; Yer 5:22; Mal 1:14; 2:5; 3:5, 16; 4:2; Kut 3:15; 6:3; Yos 7:9Kama hutafuata kwa bidii maneno yote ya sheria hii, ambayo yameandikwa katika kitabu hiki na kama hutalicha hili jina la fahari na la kutisha, yaani la Bwana Mungu wako, 5928:59 1Fal 9:7, 9; Mao 1:9, 12; 4:12; Dan 9:12; 2Nya 21:12-15Bwana ataleta mapigo ya kutisha juu yako na kwa wazao wako, maafa makali na ya kudumu, magonjwa mazito na ya kudumu. 6028:60 Kut 15:26Atakuletea juu yako magonjwa yote ya Misri yale uliyoyaogopa, nayo yataambatana nawe. 6128:61 Kum 29:21; 30:10; 31:26; Yos 1:8; 8:34; 23:6; 24:26; 2Fal 14:6; 22:8; 2Nya 17:9; 25:4; Neh 8:1, 18; Mal 4:4; Kum 4:25-26Pia Bwana atakuletea kila aina ya ugonjwa na maafa ambayo hayakuandikwa humu katika kitabu hiki cha sheria, mpaka utakapokuwa umeangamizwa. 6228:62 Mwa 22:17; Kum 4:27; 10:22; Law 26:22; Neh 9:23Ninyi ambao mlikuwa wengi kama nyota za angani mtaachwa wachache tu, kwa sababu hamkumtii Bwana Mungu wenu. 6328:63 Kum 30:9; Isa 62:5; 65:19; Yer 32:41; Sef 3:17; Mit 1:26; Mwa 6:7; Za 52:5; Yer 12:14; 31:28; 45:4Kama ilivyompendeza Bwana kuwafanya ninyi mstawi na kuongezeka kwa idadi, ndivyo itakavyompendeza kuwaharibu na kuwaangamiza ninyi. Mtangʼolewa kutoka nchi mnayoiingia kuimiliki.

6428:64 Kum 4:27; Ezr 9:7; Isa 6:12; Yer 32:23; 43:11; 52:27; Za 44:11; Neh 1:8; Yer 13:24; 18:17; 22:22; Kum 4:32; Yer 8:19; Kum 11:28; 32:17; Law 26:33Kisha Bwana atawatawanya miongoni mwa mataifa yote, kutoka mwisho mmoja wa dunia hadi mwingine. Huko mtaabudu miungu mingine, miungu ya miti na ya mawe, ambayo ninyi wala baba zenu hamkuijua. 6528:65 Mao 1:3; Ay 11:20; Law 26:16, 30; Hos 9:17Miongoni mwa mataifa hayo hamtapata raha wala mahali pa kupumzisha wayo wa mguu wenu. Huko Bwana atawapa mahangaiko ya mawazo, macho yaliyochoka kwa kungojea na moyo uliokata tamaa. 66Utaishi katika mahangaiko siku zote, ukiwa umejaa hofu usiku na mchana, wala hutakuwa kamwe na uhakika wa maisha yako. 6728:67 Ay 7:4Wakati wa asubuhi utasema hivi, “Laiti ingekuwa jioni!” Jioni utasema, “Laiti ingekuwa asubuhi,” kwa sababu ya hofu ile itakayojaza moyo wako na vitu vile macho yako yatakavyoviona. 6828:68 Kut 13:14; Yer 44:7; Hos 8:13; 9:3Bwana atawarudisha tena Misri kwa meli, safari niliyosema kamwe hamngeenda tena. Huko mtajiuza ninyi wenyewe kwa adui zenu kama watumwa wa kiume na wa kike, lakini hakuna yeyote atakayewanunua.