Kumbukumbu 27 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 27:1-26

Madhabahu Katika Mlima Ebali

127:1 Za 78:7Mose na wazee wa Israeli wakawaagiza watu: “Yashikeni maagizo haya yote ninayowaagiza leo. 227:2 Yos 4:1; Kut 24:4; Yos 24:26; 1Sam 7:12; Yos 8:31Mtakapokuwa mmevuka Mto Yordani na kuingia katika nchi awapayo Bwana Mungu wenu, msimamishe mawe makubwa na mkayatie lipu. 327:3 Kut 3:8; Kum 26:9Andikeni juu yake maneno yote ya sheria hii wakati mtakapokuwa mmevuka na kuingia katika nchi awapayo Bwana Mungu wenu, nchi itiririkayo maziwa na asali, kama vile Bwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi. 427:4 Kum 11:29; Yos 8:30Mtakapokuwa mmevuka Yordani, simamisheni mawe haya juu ya Mlima Ebali, kama ninavyowaagiza leo, mkayatie lipu. 527:5 Kut 20:24-25; Yos 8:31Huko mjengeeni Bwana Mungu wenu madhabahu, madhabahu ya mawe. Msitumie kifaa chochote cha chuma juu yake. 6Jengeni madhabahu ya Bwana Mungu wenu kwa mawe ya shambani, na mtoe sadaka za kuteketezwa juu yake kwa Bwana Mungu wenu. 727:7 Kut 32:6; Kum 16:11; Yos 8:31Toeni sadaka za amani juu yake, mkizila na kufurahia mbele za Bwana Mungu wenu. 827:8 Isa 8:1; 30:8; Hab 2:2; Yos 8:32Nanyi mtaandika maneno yote ya sheria hii kwa wazi sana juu ya mawe haya ambayo mmesimamisha.”

Laana Kutoka Mlima Ebali

927:9 Kum 17:9; 26:18Kisha Mose na makuhani, ambao ni Walawi, wakawaambia Israeli wote, “Nyamaza ee Israeli, sikiliza! Sasa umekuwa taifa la Bwana Mungu wako. 10Mtii Bwana Mungu wako, na kufuata amri zake na maagizo ninayokupa leo.”

11Siku ile ile Mose akawaagiza watu:

1227:12 Kum 11:29; Mwa 30:18; Yos 8:35; Amu 9:7Mtakapovuka Mto Yordani, makabila haya yatasimama juu ya Mlima Gerizimu kubariki watu: Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Yosefu na Benyamini. 1327:13 Kum 11:29Makabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali.

1427:14 Kum 33:10; Yos 8:33; Neh 8:7-8; Dan 9:11; Mal 2:7-9Nao Walawi watawasomea watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa:

1527:15 Kut 20:4; 34:17; 1Fal 11:5-7; 2Fal 23:13; Isa 44:9, 19; 66:3; Hes 5:22; 1Kor 14:6; Law 19:4; 26:1; Kum 4:16, 23; Isa 44:9; Hos 13:2; Hes 5:22; Yer 11:5“Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

1627:16 Mwa 31:35; Kut 21:12; Kum 5:16; Law 19:3“Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

1727:17 Kum 19:14; Mit 22:28“Alaaniwe mtu asogezaye jiwe la mpaka wa jirani yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

1827:18 Law 19:14; Ay 29:15; Mit 28:10; Mt 15:14; Ufu 2:14“Alaaniwe mtu ampotoshaye kipofu njiani.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

1927:19 Kut 22:21; Kum 24:19; Kut 23:2; Kum 10:18; Mal 3:5“Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

2027:20 Mwa 34:5; Law 18:7; 1Kor 5:1“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mke wa baba yake, kwa maana anadharau malazi ya baba yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

2127:21 Kut 22:19; Law 8:23“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama yeyote.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

2227:22 Law 18:9; 20:17; 2Sam 13:1“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na dada yake, binti wa baba yake au binti wa mama yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

2327:23 Law 20:14“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mama mkwe wake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

2427:24 Mwa 4:23; Law 24:17; Kut 21:12; Hes 35:31“Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

2527:25 Kut 23:7-8; Law 19:16; Eze 22:12; Kum 10:17; 16:19; Za 15:5; Eze 22:12“Alaaniwe mtu apokeaye rushwa ili kumuua mtu asiye na hatia.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

2627:26 Law 26:14; Kum 28:15; Za 119:21; Yer 11:3; Gal 3:10; Yer 11:5“Alaaniwe mtu yule ambaye hatashikilia maneno ya sheria hii kwa kuyatekeleza.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”