Kumbukumbu 25 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 25:1-19

125:1 Kut 21:6; Kum 17:8-13; 19:17; Mdo 23:3; 1Fal 8:32; Kut 23:7; Kum 1:16-17Watu wanapokuwa na ugomvi, wapeleke mahakamani na waamuzi wataamua shauri hilo; watawaachia wasio na kosa na kuwahukumu wenye hatia. 225:2 Mit 10:13; 19:29; Lk 12:48-49Kama mtu mwenye hatia anastahili kuchapwa, mwamuzi atamwamuru alale chini ili achapwe mbele yake idadi ya viboko kulingana na kosa lake, 325:3 Mt 27:26; Yn 19:1; 2Kor 11:24; Ay 18:3; Yer 20:2lakini kamwe asichapwe zaidi ya viboko arobaini. Ikiwa atachapwa zaidi ya viboko arobaini, nduguyo atadhalilika machoni pako.

425:4 Hes 22:29; 1Kor 9:9; 1Tim 5:18Usimfunge maksai kinywa anapopura nafaka.

525:5 Rut 4:10-13; Mt 22:24; Mk 12:19; Lk 20:28Ikiwa ndugu wanaishi pamoja na mmoja wao akafa bila kuacha mwana, kamwe mjane wake asiolewe nje ya jamaa hiyo. Ndugu wa mumewe atamchukua, amwoe na kutimiza wajibu wa shemeji kwake. 625:6 Mwa 38:9; Rut 4:5, 10Mwana wa kwanza atakayemzaa atapewa jina la ndugu aliyekufa ili jina lake lisifutike katika Israeli.

725:7 Rut 1:15; 4:2-6; Mwa 23:10Hata hivyo, ikiwa ndugu huyo wa mume hataki kuoa huyo mke wa nduguye, mjane atawaendea wazee kwenye lango la mji na kusema, “Ndugu wa mume wangu anakataa kuendeleza jina la nduguye katika Israeli. Hataki kutimiza wajibu wa shemeji kwangu.” 8Ndipo wazee wa mji wake watamwita na kuzungumza naye. Kama atashikilia kukataa akisema, “Sitaki kumwoa,” 925:9 Yos 24:22; Rut 4:7-11; Hes 12:14; Ay 17:6; 30:10; Isa 50:6mjane wa nduguye atamwendea mbele ya wazee, atamvua kiatu kimoja na kumtemea mate usoni, na kusema, “Hivi ndivyo ambavyo hufanywa kwa mtu ambaye atakataa kuendeleza jamaa ya ndugu yake.” 1025:10 Mit 6:33; 1Tim 3:7Jamaa ya mtu huyo itafahamika katika Israeli kama Jamaa ya Aliyevuliwa Kiatu.

11Ikiwa watu wawili wanapigana na mke wa mmoja wao akaja kumwokoa mumewe na yule anayemshambulia, naye mke huyo akifika na kumkamata sehemu za siri, 1225:12 Kum 7:2; 19:13huyo mwanamke utamkata mkono wake. Usimhurumie.

1325:13 Mit 11:1; 20:23; Eze 45:10; Mik 6:11; Amo 8:5Usiwe na mawe ya kupimia ya aina mbili katika mkoba wako, moja zito na jingine jepesi. 1425:14 Law 7:20; Hos 9:4Usiwe na vipimo viwili tofauti katika nyumba yako, kimoja kikubwa, kingine kidogo. 1525:15 Kut 20:12Ni lazima uwe na uzito na vipimo sahihi na vya haki, ili upate kuishi maisha marefu katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako. 1625:16 Mit 11:1; 20:23; Amo 8:9-11; Ufu 21:27; 1Tim 4:6; 1Kor 8:9-11Kwa maana Bwana Mungu wako humchukia yeyote ambaye hufanya mambo kama haya, yeyote anayetenda kwa udanganyifu.

1725:17 Mwa 36:12; Kut 17:8Kumbuka kile Waamaleki walichowatendea mlipokuwa njiani mkitoka Misri. 1825:18 Za 36:1; Rum 3:18; Mit 16:6Wakati mlipokuwa mmechoka na kuishiwa nguvu kwa safari yenu, wakawapiga wale wote waliokuja nyuma. Waamaleki hawakumwogopa Mungu. 1925:19 Kut 33:14; Ebr 3:18-19; Es 9:16; Mwa 36:12; 1Sam 15:2-3Bwana Mungu wako atakapokupa pumziko mbali na adui zako wote wanaokuzunguka katika nchi akupayo kuimiliki kuwa urithi, utafutilia mbali kumbukumbu lote la Waamaleki chini ya mbingu. Usisahau!