Kumbukumbu 24 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 24:1-22

Sheria Kuhusu Ndoa Na Talaka

124:1 Kum 22:13; 2Fal 17:6; Isa 50:1; Yer 3:8; Mt 1:19; 5:31; 19:7-9; Mk 10:4-5; Mal 2:16Ikiwa mtu atamwoa mke na akamchukia kwa sababu ya kukosa adabu, naye akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza kutoka nyumbani kwake, 2ikiwa baada ya kuondoka nyumbani kwake atakuwa mke wa mtu mwingine, 3ikiwa mume wake wa pili atachukizwa naye akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza kutoka nyumbani kwake, au kama akifa, 424:4 Yer 3:1basi yule mume wake wa kwanza, ambaye alimpa talaka, haruhusiwi kumwoa tena baada ya mwanamke huyo kuwa najisi. Hayo yatakuwa machukizo machoni pa Bwana. Usilete dhambi juu ya nchi ambayo Bwana Mungu wako anakupa kama urithi.

524:5 Kum 20:7; Mit 5:18Kama mtu ameoa karibuni, kamwe asipelekwe vitani au kupewa wajibu mwingine wowote. Kwa mwaka mmoja atakuwa huru kubaki nyumbani ili amfurahishe mke aliyemwoa.

624:6 Kut 22:22; Isa 47:2Usitoe jozi ya mawe ya kusagia, hata ikiwa lile la juu, kuweka rehani kwa ajili ya deni, kwa sababu itakuwa ni kuweka uhai wa mtu kama dhamana.

724:7 Yer 11:2; Ebr 9:15; 10:15-17; Mwa 17:9; Kut 3:1; Kum 4:2324:7 Kut 21:16; 1Kor 5:13Kama mtu akikamatwa akiiba yeyote miongoni mwa ndugu zake wa Waisraeli na kumtenda kama mtumwa au akimuuza, mwizi huyo ni lazima auawe. Nawe utaondoa uovu kutoka miongoni mwenu.

824:8 Law 13:1-46; Kum 17:9; Law 14:2; Mt 8:4; Lk 5:14; 7:14Pakitokea magonjwa ya ngozi ya kuambukiza, mwe waangalifu sana kufanya sawasawa na maagizo ya makuhani, ambao ni Walawi. Ni lazima mfuate kwa uangalifu yale niliyowaamuru. 924:9 Hes 12:10; Lk 17:32; 1Kor 10:6Kumbukeni kile Bwana Mungu wenu alichomfanyia Miriamu njiani baada ya ninyi kutoka Misri.

1024:10 Kut 22:25-27Unapomkopesha jirani yako chochote, usiingie nyumbani kwake kutwaa kile anachokitoa kama rehani. 11Ukae nje na umwache huyo mtu uliyemkopesha akuletee hiyo rehani. 1224:12 Kut 22:26Ikiwa mtu huyo ni maskini, usiende kulala ukiwa na hiyo rehani yake katika milki yako. 1324:13 Kut 22:26-27; Kum 6:25; Za 106:31; Dan 4:27; Ay 24:7, 8; 31:16-20; Eze 18:7, 12, 16; 33:15; Amo 2:8; Ay 29:11; 2Kor 9:13; 2Tim 1:18Rudisha vazi lake kabla ya machweo ya jua ili apate kulilalia. Kisha atakushukuru na kitaonekana kama kitendo cha haki mbele za Bwana Mungu wako.

1424:14 Law 19:13; 25:35-43; Kum 15:12-18; Ay 24:4; Mit 14:31; 19:17; 1Tim 5:18; Amo 4:1; Mal 3:5Usimwonee mtu maskini na mhitaji ambaye umemwajiri, akiwa ni nduguyo Mwisraeli au mgeni anayeishi katika mojawapo ya miji yenu. 1524:15 Law 25:35; 19:13; Mt 20:8; Kut 22:23; Ay 12:19; Yak 5:4; Yer 22:13Mlipe ujira wake kila siku kabla ya jua kutua, kwa sababu yeye ni maskini na anautegemea ujira huo. La sivyo, anaweza kumlilia Bwana dhidi yako, nawe ukapata hatia ya dhambi.

1624:16 Hes 26:11; Yer 31:29-30; Eze 18:20; 2Fal 14:6Baba wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.

1724:17 Kut 22:22; Ay 6:27; 24:9; 29:12; Za 10:17-18; 82:3; Mit 23:10; Eze 22:7; Kut 22:21; 23:2; Kum 10:18Usipotoshe hukumu ya mgeni au yatima, au kuchukua vazi la mjane kama rehani. 18Kumbukeni kwamba mlikuwa watumwa huko Misri, naye Bwana Mungu wenu akawakomboa kutoka huko. Hii ndiyo sababu ninawaamuru kutenda hili.

1924:19 Law 19:9; Kum 10:19; 27:19; Eze 47:22; Zek 7:10; Mal 3:5; Kum 14:29; Law 23:22; Mit 19:17; 28:27; Mhu 11:1Unapovuna shamba lako na ukasahau mganda, usirudi kuuchukua. Acha kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane, ili Bwana Mungu wako aweze kukubariki wewe katika kazi zote za mikono yako. 2024:20 Law 19:10Unapovuna zeituni kutoka miti yako, usirudie matawi mara ya pili. Acha kilichobaki kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane. 21Unapochuma zabibu katika shamba lako la mizabibu usirudie tena. Acha zinazobaki kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane. 22Kumbuka kwamba mlikuwa watumwa katika nchi ya Misri. Ndiyo sababu ninawaamuru kufanya hili.