Kumbukumbu 23 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 23:1-25

Kutengwa Na Mkutano

123:1 Law 21:20Asiingie mtu yeyote aliyehasiwa kwa kupondwa makende au kwa kukatwa uume wake katika kusanyiko la Bwana.

2Mtu yeyote ambaye amezaliwa kwenye ndoa isiyo halali au wazao wake wasiingie kwenye kusanyiko la Bwana, hata mpaka kizazi cha kumi.

323:3 Mwa 19:38; Neh 13:2; Rut 4:5; Neh 4:3-7Hapatakuwa na Mwamoni au Mmoabu au yeyote wa wazao wao atakayeruhusiwa kuingia katika kusanyiko la Bwana, hata mpaka kizazi cha kumi. 423:4 Kum 2:28; Hes 23:7; 2Pet 2:15; Mwa 24:10; 14:18; Kum 2:29; 1Sam 25:11; 1Fal 18:4; Isa 63:9Kwa kuwa hawakuja kuwalaki wakiwa na mkate na maji mlipokuwa njiani mlipotoka Misri, tena walimwajiri Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyoko Aramu-Naharaimu23:4 Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi. ili kuwalaani ninyi. 523:5 Hes 24:10; Yos 24:10; Mit 26:2; Kum 4:37Hata hivyo, Bwana Mungu wenu hakumsikiliza Balaamu bali aligeuza laana kuwa baraka kwenu kwa sababu Bwana Mungu wenu anawapenda. 623:6 Hes 24:17; Isa 15:1; 25:10; Yer 25:21; 27:3; 48:1; Eze 25:8; Sef 2:9; Ezr 9:12; Mt 5:43Msitafute mapatano ya urafiki nao maisha yenu yote.

723:7 Mwa 25:30; 25:26; Law 19:34; Kut 23:9; Oba 1:11-12; Law 15:1-33; Kum 10:19; Law 19:34Usimchukie Mwedomu, kwa kuwa yeye ni ndugu yako. Usimchukie Mmisri, kwa sababu uliishi kama mgeni katika nchi yake. 8Kizazi cha tatu cha watoto watakaozaliwa nao wanaweza kuingia katika kusanyiko la Bwana.

Unajisi Katika Kambi

9Unapokuwa umepiga kambi dhidi ya adui zako, jitenge na kitu chochote kisicho safi. 1023:10 Law 15:16Ikiwa mtu amechafuka kwa sababu ya kutokwa na shahawa usiku, inampasa atoke nje ya kambi na kukaa huko. 1123:11 Law 15:16; 1Sam 21:5Lakini jioni ikikaribia ataoga, na baada ya jua kuzama ataingia tena kambini.

12Tengeni mahali nje ya kambi ambapo mnaweza kwenda kujisaidia. 13Kama sehemu ya vifaa vyenu kuweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kile kikutokacho. 1423:14 Mwa 3:8; Kut 3:4-5; Law 26:12; Yer 32:40; 2Kor 6:16Kwa kuwa Bwana Mungu wenu hutembea katika kambi yenu ili kuwalinda na kuwaweka adui zenu mikononi mwenu. Kambi yenu ni lazima iwe takatifu, ili asione kitu chochote miongoni mwenu kilicho kichafu akageuka na kuwaacha.

Sheria Mbalimbali

1523:15 2Sam 22:3; Za 2:12; 71:1; 1Sam 30:15Ikiwa mtumwa amekimbilia kwako, usimrudishe kwa bwana wake. 1623:16 Kut 22:21; 23:6; Mt 22:22; Yer 7:6; Zek 7:10; Yak 2:6Mwache aishi miongoni mwenu mahali popote anapopapenda na katika mji wowote anaochagua. Usimwonee.

1723:17 1Fal 14:24; 15:12; 22:46; 2Fal 23:7; Ay 36:14; Mwa 38:21; Law 19:29; Mit 2:16; Mwa 19:5Asiwepo Mwisraeli mwanamke kahaba au mwanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu. 1823:18 Mwa 19:5; Law 20:13; Ufu 22:15Kamwe usilete mapato ya ukahaba ikiwa ni ya mwanamke au ni ya mwanaume katika nyumba ya Bwana Mungu wako kwa ajili ya nadhiri yoyote, kwa sababu Bwana Mungu wako anachukizwa na yote mawili.

1923:19 Law 25:35-37; Neh 5:2-7; Kut 22:25; Za 15:5; Lk 6:34Usimtoze ndugu yako riba, iwe ni fedha ama chakula ama kitu kingine chochote ambacho waweza kupata riba juu yake. 2023:20 Hes 6:21; Amu 11:35; Za 15:4; Hes 30:1-2; Ay 22:27; Za 61:8; 65:1; 76:11; Mhu 5:4-5; Isa 19:21; Mt 5:33; Mdo 5:3; Kum 25:10; 28:12; Law 19:34Unaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili kwamba Bwana Mungu wako akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoingia kuimiliki.

2123:21 Ay 22:27; Za 61:8; Mhu 5:4-5Ukiweka nadhiri kwa Bwana Mungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi. 2223:22 Mdo 5:4Lakini ukijizuia kuweka nadhiri, hutakuwa na hatia. 2323:23 Za 66:13Chochote kitakachotamkwa kwa midomo yako ni lazima uhakikishe umekifanya, kwa sababu uliweka nadhiri yako kwa hiari mbele za Bwana Mungu wako kwa kinywa chako mwenyewe.

2423:24 Mt 12:1; Lk 12:15; 1Kor 6:10; Kol 3:5Kama ukiingia katika shamba la mizabibu la jirani yako, unaweza kula zabibu kadiri utakavyo, lakini usiweke chochote kwenye kikapu chako. 2523:25 Mt 12:1; Mk 2:23; Lk 6:1Kama ukiingia katika shamba la nafaka la jirani yako, unaweza kukwanyua kwa mikono yako, lakini usikate kwa mundu nafaka iliyosimama.