Kumbukumbu 22 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 22:1-30

122:1 Kut 23:4-5; Mit 27:10; Zek 7:9Kama ukimwona ngʼombe au kondoo wa ndugu yako anapotea, usipuuze, bali uhakikishe unamrudisha kwa mwenyewe. 2Ikiwa huyo ndugu haishi karibu nawe au kama hufahamu yeye ni nani, mchukue nyumbani kwako huyo mnyama umweke mpaka mwenyewe aje kumtafuta. Ndipo umrudishie. 3Fanya vivyo hivyo ukimkuta punda wa nduguyo au joho lake au chochote alichopoteza. Usipuuze jambo hilo.

422:4 Kut 23:5; 1Kor 9:9; Rum 12:10; 2Pet 1:7; 1Yn 3:15; 4:21; Zek 7:9Kama ukimwona punda wa nduguyo au ngʼombe wake ameanguka barabarani, usipuuze jambo hilo. Msaidie asimame kwa miguu yake.

522:5 1Kor 14:40Haimpasi mwanamke kuvaa nguo za kiume wala mwanaume kuvaa nguo za kike, kwa maana Bwana Mungu wenu anachukia yeyote ambaye hufanya hivi.

622:6 Law 22:28; Neh 9:6; Za 36:6; 145:9; Mt 10:29; Lk 12:6Kama ukikuta kiota cha ndege kando ya barabara, iwe juu ya mti au chini, naye ndege amelala juu ya makinda au mayai, usimchukue huyo ndege pamoja na makinda yake. 722:7 Law 22:28; Kum 5:29; 4:20Waweza kuchukua makinda, lakini uwe na hakika ya kumwacha huyo ndege, ili upate kufanikiwa na uweze kuishi maisha marefu.

822:8 Yos 2:8; 1Sam 11:2Wakati unapojenga nyumba mpya, fanya ukuta wa kuzuia kandokando ya dari ili usijiletee hatia ya kumwaga damu juu ya nyumba yako ikiwa yeyote ataanguka kutoka humo.

922:9 Law 19:9; Mt 6:24; 9:16; 2Kor 6:14-16Usipande aina mbili za mbegu katika shamba lako la mizabibu; ikiwa utafanya hivyo, si mazao utakayopanda tu yatakuwa najisi, bali nayo matunda ya shamba la mizabibu pia.

1022:10 2Kor 6:14-16Usilime kwa maksai aliyefungwa nira pamoja na punda.

1122:11 Law 19:9; 19:19Usivae nguo za sufu na kitani zilizofumwa pamoja.

1222:12 Hes 15:37-41; Mt 23:5Fanya vishada kwenye pembe nne za joho unalovaa.

Kukiuka Taratibu Za Ndoa

1322:13 Kum 24:1; Mwa 29:21; Amu 15:1; Efe 5:28-29Ikiwa mtu atamwoa mke na, baada ya kufanya naye tendo la ndoa, akamchukia, 14akimsingizia na kumwita jina baya, akisema, “Nilimwoa mwanamke huyu, lakini nilipomkaribia sikupata uthibitisho wa ubikira wake” 1522:15 Mwa 23:10ndipo baba na mama wa msichana wataleta uthibitisho kwamba alikuwa bikira kwa wazee wa mji kwenye lango. 16Baba wa msichana atawaambia wazee, “Nilimwoza binti yangu kwa huyu mwanaume, lakini hampendi. 17Sasa amemsingizia na kusema, ‘Sikumkuta huyu binti akiwa bikira.’ Lakini hapa kuna uthibitisho wa ubikira wa binti yangu.” Kisha wazazi wake wataonyesha nguo zake kwa wazee wa mji, 1822:18 Kut 18:21; Kum 1:9-18; Rum 13:3nao wazee watamchukua huyo mwanaume na kumwadhibu. 19Watamtoza shekeli mia moja22:19 Shekeli 100 za fedha ni sawa na kilo moja. za fedha na kupewa wazazi wa msichana, kwa sababu mwanaume huyu amempa bikira wa Kiisraeli jina baya. Ataendelea kuwa mke wake; kamwe hawezi kumpa talaka siku zote za maisha yake.

2022:20 Kum 17:4Hata hivyo, kama shtaka ni la kweli na hakuna uthibitisho juu ya ubikira wa huyo msichana ulioweza kupatikana, 2122:21 Mwa 34:7; 38:24; Law 19:29; Kum 23:17-18; 1Kor 5:13; 2Sam 13:12, 13huyo msichana ataletwa kwenye mlango wa nyumba ya baba yake, na hapo watu wa mji wake watampiga kwa mawe hadi afe. Amefanya kitu cha aibu katika Israeli kwa kufanya ukahaba akiwa nyumbani kwa babaye. Lazima mwondoe uovu katikati yenu.

2222:22 2Sam 11:4; Mwa 38:24; Kut 21:12; Mt 5:27-28; Yn 8:5; 1Kor 6:9; Ebr 13:4; Law 20:10; Mit 6:22; Mal 3:5; Yn 8:5Ikiwa mwanaume atakutwa akizini na mke wa mtu mwingine, wote wawili, mwanaume na mwanamke aliyezini naye, lazima wauawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli.

2322:23 Mt 1:18, 19Ikiwa mwanaume atakutana na bikira mjini ambaye ameposwa na mtu akazini naye, 2422:24 1Kor 5:13; Kum 21:14; Mt 1:20, 24utawachukua wote wawili kwenye lango la mji na kuwapiga kwa mawe mpaka wafe; yule msichana kwa kuwa alikuwa mjini na hakupiga kelele kuomba msaada, na yule mwanaume kwa sababu amemtenda jeuri mke wa mtu mwingine. Lazima mwondoe uovu katikati yenu.

25Lakini ikiwa itatokea mwanaume akakutana na msichana aliyeposwa huko mashambani, akambaka, mwanaume aliyefanya hivi peke yake ndiye atakayeuawa. 26Usimtendee msichana yule jambo lolote; hajafanya dhambi inayostahili kifo. Shauri hili ni kama lile la yeyote ambaye anamshambulia na kumuua kwa makusudi jirani yake, 2722:27 Mwa 39:14kwa maana mwanaume huyo alimkuta msichana huko mashambani, na ingawa msichana aliyeposwa alipiga kelele, hapakuwa na mtu wa kumwokoa.

2822:28 Kut 22:16, 17Ikiwa itatokea mwanaume akutane na bikira ambaye hajaposwa na kumbaka nao wakakutwa, 29mwanaume atamlipa baba wa msichana shekeli hamsini22:29 Shekeli 50 za fedha ni sawa na gramu 600. za fedha. Ni lazima amwoe huyo msichana, kwa maana amemfanyia jeuri. Kamwe hawezi kumpa talaka siku zote za maisha yake.

3022:30 Mwa 29:29; Law 18:8; 20:9; Kum 27:20Mwanaume asimwoe mke wa baba yake; kamwe asidhalilishe kitanda cha baba yake.