Kumbukumbu 21 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 21:1-23

Upatanisho Kuhusu Mauaji

121:1 Hes 25:17; Za 9:12; Mit 28:17Kama mtu akikutwa ameuawa, naye amelala kwenye shamba katika nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa kuimiliki, wala haijulikani ni nani aliyemuua, 2wazee wenu na waamuzi watatoka na kupima umbali kutoka maiti alipolala mpaka kwenye miji ya jirani. 321:3 Hes 19:2Kisha wazee wa ule mji ulio karibu zaidi na yule maiti watamchukua mtamba ambaye hajapata kufanyishwa kazi na ambaye hajafungwa nira, 4na kumpeleka kwenye bonde ambalo halijapata kulimwa au kupandwa mazao na ambapo kuna chemchemi itiririkayo. Huko kwenye hilo bonde, wazee watamvunja yule mtamba shingo. 521:5 Mwa 48:20; Kut 39:43; Kum 17:8-11Makuhani, hao wana wa Lawi, watasogea mbele, kwa kuwa Bwana Mungu wenu, amewachagua kuhudumu na kutoa baraka katika jina la Bwana, na kuamua mashauri yote ya mabishano na mashambulio. 621:6 Mt 27:24; 1Nya 23:1321:6 Ay 9:30; Za 19:12; Yer 2:22; Mt 27:14; Ebr 9:10Ndipo wazee wote wa mji ulio karibu zaidi na huyo maiti watanawa mikono yao juu ya huyo mtamba ambaye shingo yake imevunjwa huko kwenye bonde, 721:7 2Sam 3:28nao watatangaza: “Mikono yetu haikumwaga damu hii, wala macho yetu hayakuona likifanyika. 821:8 Hes 35:33-34; Yer 26:15; Eze 22:3; Yn 1:14Ee Bwana, ukubali upatanisho kwa watu wako Israeli, ambao umewakomboa, wala usiwahesabie watu wako hatia ya damu ya mtu asiyekuwa na hatia.” Nayo damu iliyomwagika itakuwa imefanyiwa upatanisho. 921:9 Kum 19:13Hivyo mtakuwa mmejitakasa wenyewe kutoka hatia ya kumwaga damu isiyokuwa na hatia, kwa kuwa mmefanya lile lililo sawa mbele za macho ya Bwana.

Kuoa Mwanamke Mateka

1021:10 Yos 21:44; 1Fal 8:46; 1Nya 9:1; Ezr 5:12; Yer 40:1; Eze 1:1; 17:12; Dan 2:25; Mik 4:10; 2Nya 32:8Mkienda vitani kupigana na adui zenu naye Bwana Mungu wenu akawatia adui mikononi mwenu, nanyi mkachukua mateka, 1121:11 Mwa 6:2; 34:8kama ukiona miongoni mwa mateka mwanamke mzuri wa sura nawe wavutwa naye, waweza kumwoa akawa mke wako. 1221:12 Law 14:9; Hes 8:7; 1Kor 11:5; Hes 6:9Mlete nyumbani mwako, anyoe nywele na kukata kucha zake, 1321:13 Za 45:10avue nguo alizokuwa amevaa alipotekwa. Baada ya kuishi nyumbani mwako na kumwombolezea baba yake na mama yake kwa mwezi mzima, ndipo utakapoweza kumwendea na kuwa mume wake naye atakuwa mke wako. 1421:14 Mwa 34:2; Amu 19:24Lakini kama hutaendelea kupendezwa naye, mwache aende popote anapotaka. Kamwe huwezi kumuuza au kumtendea kama mtumwa, kwa sababu utakuwa umemvunjia heshima.

Haki Ya Mzaliwa Wa Kwanza

1521:15 Mwa 4:19; 29:33Kama mwanaume ana wake wawili, naye anampenda mmoja na mwingine hampendi na wote wawili wamemzalia wana wa kiume, lakini mwana mzaliwa wa kwanza ni wa yule mke asiyempenda, 1621:16 1Nya 26:10; Rum 8:29wakati anapotoa wosia wa mali yake kwa wanawe, kamwe asitoe haki za mzaliwa wa kwanza kwa mwana wa mke ampendaye kwa upendeleo, badala ya mzaliwa hasa wa kwanza, ambaye ni mwana wa mke ambaye hampendi. 1721:17 2Fal 2:9; Isa 40:2; 61:7; Zek 9:12; Mwa 49:3; 25:31; Lk 15:12; 1Nya 5:1Ni lazima amkubali mwana wa mke asiyempenda kama mzaliwa wa kwanza kwa kumpa sehemu ya vile vyote alivyo navyo maradufu. Mwana huyo ni ishara ya kwanza ya nguvu za baba yake. Haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye.

Mwana Mwasi

1821:18 Za 78:8; Yer 5:23; Sef 3:1; Mit 30:17; Mwa 31:35; Mit 1:8; Isa 30:1; Efe 6:1-3; Kut 20:12; 21:15, 17; Law 19:3; 21:9Kama mtu ana mwana mkaidi na mwasi ambaye hamtii baba yake na mama yake, na hasikii wazazi wanapomrudi, 19baba yake na mama yake watamleta kwa wazee kwenye lango la mji wake. 20Watawaambia wazee, “Huyu mwanetu ni mkaidi na mwasi. Hatutii sisi, yeye ni mpotovu na mlevi.” 2121:21 Law 20:9; Kum 19:19; 1Kor 5:13; Kum 13:11; 1Sam 26:16Kisha wanaume wote wa mjini mwake watampiga kwa mawe mpaka afe. Ndivyo imewapasa kuondoa maovu kati yenu. Israeli yote itasikia hili na kuogopa.

Sheria Mbalimbali

2221:22 Kum 22:26; Mt 26:66; Mk 14:64; Mdo 23:29Kama mtu ana hatia ya kosa linalompasa kuuawa naye akauawa, mwili wake utaangikwa mtini, 2321:23 Yos 8:29; 10:27; Yn 19:31; Eze 39:12; Ezr 6:11; Es 2:23; 7:9; 8:7; 9:13, 25; Isa 50:11; Gal 3:13; Law 18:25kamwe msiuache mwili wake mtini usiku kucha. Hakikisheni mnauzika mwili wake siku ile ile, kwa sababu kila mtu anayeangikwa mtini yupo chini ya laana ya Mungu. Msiinajisi nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa kama urithi wenu.