Kumbukumbu 20 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 20:1-20

Kwenda Vitani

120:1 Za 20:7; Isa 31:1; Hes 14:9; Kum 3:22; 1Sam 17:45; Isa 41:10; 2Nya 32:7-8; Hes 23:21; Kum 31:6, 8; 2Nya 13:12; 32:7, 8Mtakapokwenda vitani kupigana na adui zenu na mkaona farasi na magari ya vita na jeshi kubwa kuliko lenu, msiwaogope, kwa sababu Bwana Mungu wenu aliyewatoa kutoka Misri, atakuwa pamoja nanyi. 2Wakati mtakapokaribia kwenda vitani, kuhani atakuja mbele na kuhutubia jeshi. 320:3 1Sam 17:32; Ay 23:16; Za 22:14; Isa 7:4; 35:4; Yer 51:46Atasema: “Sikia, ee Israeli, leo unakwenda vitani kupigana na adui zako. Usife moyo wala usiogope, usitishwe wala usitiwe hofu mbele yao. 420:4 2Nya 20:14-22; Kut 14:14; 1Nya 5:22; Neh 4:20; Amu 12:3; 15:18; Za 44:7; 144:10; Kum 1:30Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ndiye huenda pamoja nanyi kuwapigania dhidi ya adui zenu na kuwapatia ushindi.”

520:5 Neh 12:27Maafisa wataliambia jeshi: “Je, kuna yeyote aliyejenga nyumba mpya ambayo haijawekwa wakfu? Yeye na arudi nyumbani, ama sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akaiweka wakfu. 620:6 Yer 31:5; Eze 28:26; Mik 1:6; 1Kor 9:7Je, kuna yeyote aliyepanda shamba la mizabibu na hajaanza kulifurahia? Yeye na arudi nyumbani, au sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akalifurahia. 720:7 Kum 24:5; Mit 5:18Je, kuna yeyote aliyeposa mwanamke na hajamwoa? Yeye na arudi nyumbani, ama sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akamwoa.” 820:8 Amu 7:3Kisha maafisa wataongeza haya, “Je, kuna mtu anayeogopa ama kufa moyo? Yeye na arudi nyumbani ili ndugu zake nao wasije wakafa moyo pia.” 9Wakati maafisa watakapomaliza kuzungumza na jeshi, watawateua wakuu wa vikosi.

1020:10 Kum 2:26; Lk 14:31-32; 2Sam 20:18-20Wakati mtakapokwenda kushambulia mji, wapeni watu wake masharti ya amani. 1120:11 2Fal 6:22; 1Fal 9:21; 1Nya 22:2; Isa 31:7Wakikubali na kuwafungulia malango yao, watu wake wote watawatumikia kwa kufanya kazi ngumu na watawatumikia. 12Ikiwa watakataa kufanya mapatano ya amani na wakiwaingiza katika vita, basi mtauzunguka mji huo kwa vita. 1320:13 Hes 31:7Wakati Bwana Mungu wenu atakapouweka mji huo mkononi mwenu, waueni kwa upanga wanaume wote waliomo ndani yake. 1420:14 Yos 8:2; 22:8; Hes 31:11; 31:53Kwa upande wa wanawake, watoto, mifugo na kila kitu kingine chochote ndani ya huo mji, mnaweza kuvichukua kama nyara kwa ajili yenu. Nanyi mnaweza kuzitumia hizo nyara ambazo Bwana Mungu wenu amewapa kutoka kwa adui zenu. 1520:15 Yos 9:9Hivi ndivyo mtakavyofanya kwa miji yote ambayo iko mbali nanyi, ambayo haimilikiwi na mataifa ya karibu.

1620:16 Kut 23:31-33; Hes 21:2-3; Kum 7:2; Yos 6:21; 10:1; 11:14Hata hivyo, katika miji ya mataifa ambayo Bwana Mungu wenu anawapa kama urithi, msiache kitu chochote hai kinachopumua. 17Waangamizeni kabisa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, kama Bwana Mungu wenu alivyowaamuru. 1820:18 Kut 34:16; 10:7; 23:33; Kum 12:30-31; Yos 23:12-13; 1Kor 15:33; 2Fal 21:3, 15; Za 106:34-41; Hos 8:11La sivyo, watawafundisha kufuata mambo yote ya machukizo wanayofanya wakiabudu miungu yao, nanyi mtatenda dhambi dhidi ya Bwana Mungu wenu.

19Wakati mtakapouzunguka mji kwa vita kwa muda mrefu, mkipigana dhidi yake ili kuuteka, msiharibu miti yake kwa kuikata kwa shoka, kwa sababu mtaweza kula matunda yake. Hivyo msiikate. Je, miti hiyo ya mashambani ni watu, hata muizingire? 20Hata hivyo, mnaweza kuikata miti ambayo sio miti ya matunda na kuitumia kujenga ngome, mpaka mji ulio katika vita na ninyi utakapoanguka.