Kumbukumbu 15 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 15:1-23

Mwaka Wa Kufuta Madeni

(Walawi 25:1-7)

115:1 Kum 31:10; Neh 10:31; Kut 23:10; Yer 34:14Kila mwisho wa miaka saba ni lazima mfute madeni. 2Hivi ndivyo itakavyofanyika: Kila mkopeshaji atafuta mkopo aliomkopesha Mwisraeli mwenzake. Hatamtaka Mwisraeli mwenzake au ndugu yake amlipe hilo deni, kwa sababu wakati wa Bwana wa kufuta madeni umetangazwa. 315:3 Mwa 31:15; Kum 23:20; 28:12; Rut 2:10Unaweza kudai malipo kwa mgeni, lakini lazima ufute kila deni ambalo unamdai ndugu yako. 415:4 Kum 28:5, 8Hata hivyo, hapatakuwepo maskini miongoni mwenu, kwa kuwa katika nchi Bwana Mungu wenu anayowapa kuimiliki kama urithi wenu, atawabariki sana, 515:5 Kut 15:26; Kum 7:12; 28:1ikiwa tutamtii Bwana Mungu wenu kikamilifu na kuwa waangalifu kuyafuata maagizo haya yote ninayowapa leo. 615:6 Kum 28:12-13, 44; Mit 22:7Kwa kuwa Bwana Mungu wenu atawabariki kama alivyoahidi, nanyi mtawakopesha mataifa mengi lakini hamtakopa kwa yeyote. Mtatawala mataifa mengi lakini hakuna taifa litakalowatawala ninyi.

715:7 Mt 26:11; 18:30; 1Yn 3:17Ikiwa kuna mtu maskini miongoni mwa ndugu zenu, katika mji wowote wa hiyo nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, msiwe na moyo mgumu wala usimfumbie mkono ndugu yako aliye maskini. 815:8 Mt 5:42; Lk 6:34; Mdo 24:17; Law 25:35; Gal 2:10Afadhali fungua mikono yako na umkopeshe kwa hiari chochote anachohitaji. 915:9 Mt 20:15; Kut 22:23; Ay 5:15; Yak 5:4; Amo 5:11; Mit 28:22; Za 140:12Jihadhari usijiwekee wazo hili ovu: “Mwaka wa saba, mwaka wa kufuta madeni umekaribia,” usije ukaonyesha nia mbaya kwa ndugu yako mhitaji na ukaacha kumpa chochote. Anaweza kumlalamikia Bwana dhidi yako nawe utakuwa umepatikana na hatia ya dhambi. 1015:10 2Kor 9:5; Kum 14:29; 24:19; Mt 25:40; Mdo 20:35; Rum 12:8; 1Tim 6:18; 1Pet 4:11Mpe kwa ukarimu na ufanye hivyo bila kinyongo moyoni, ndipo kwa sababu ya hili Bwana Mungu wenu atakubariki katika kazi zako zote na kwa kila kitu utakachokiwekea mkono wako. 1115:11 Mt 26:11; Mk 14:7; Yn 12:8Siku zote watakuwepo watu maskini katika nchi. Kwa hiyo ninawaamuru mwe na mikono iliyokunjuliwa kuwaelekea ndugu zenu, kuwaelekea maskini na wahitaji katika nchi yenu.

Kuwaacha Huru Watumwa

(Kutoka 21:1-18)

1215:12 Yer 34:14; Kut 21:2; Law 25:39Kama Mwebrania mwenzako, mwanaume au mwanamke, akijiuza kwako na kukutumikia miaka sita, katika mwaka wa saba ni lazima umwache aende zake akiwa huru. 13Nawe wakati utakapomwachia usimwache aende mikono mitupu. 1415:14 Hes 18:27; Mit 10:22Mpe kwa uhuru kutoka zizi lako la kondoo na mbuzi, kutoka sakafu yako ya kupuria nafaka na kutoka mashinikizo yako ya kukamulia divai. Mpe kama vile ambavyo Bwana Mungu wako alivyokubariki. 1515:15 Kut 13:3; Yer 34:13; Kut 20:2; Kum 4:34; 9:26; 16:12; 24:18; Yer 16:14; 27:7Kumbukeni kuwa ninyi mlikuwa watumwa huko Misri naye Bwana Mungu wenu aliwakomboa. Ndiyo sababu nimewapa agizo hili leo.

1615:16 Kum 21:5-6Lakini mtumishi wako akikuambia, “Sitaki kukuacha,” kwa sababu anakupenda wewe na jamaa yako naye anaridhika nawe, 17ndipo utachukua chuma kidogo utoboe sikio lake mpaka hicho chuma kiingie kwenye ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako wa maisha. Ufanye vivyo hivyo kwa mtumishi wa kike.

1815:18 Isa 16:14; 21:16Usifikiri kuwa kuna ugumu kumwacha mtumishi wako huru, kwa sababu utumishi wake kwako kwa miaka hii sita umekuwa wa thamani mara mbili ya ujira wa mtumishi wa kuajiriwa. Naye Bwana Mungu wenu atakubarikia kwa kila kitu utakachofanya.

Wazaliwa Wa Kwanza Wa Wanyama

1915:19 Law 27:9; Kut 13:2; Mwa 4:4; Kut 22:30Wekeni wakfu kwa Bwana Mungu wenu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa makundi yenu ya ngʼombe na ya mbuzi na kondoo. Maksai walio wazaliwa wa kwanza msiwafanyize kazi, wala msinyoe manyoya ya wazaliwa wa kwanza wa kondoo. 2015:20 Law 7:15-18; Kum 12:5-7; 14:23Kila mwaka ninyi na jamaa zenu mtapaswa kuwala mbele za Bwana Mungu wenu pale mahali atakapopachagua. 2115:21 Kut 12:5; Law 22:19-25; Kum 17:1; Mal 1:8, 13Kama mnyama ana dosari, akiwa ni kilema au kipofu au kama ana kilema kibaya, kamwe usimtoe dhabihu kwa Bwana Mungu wenu. 2215:22 Kum 12:15, 22Itawapasa kumla ninyi wenyewe katika miji yenu. Wote wasio safi na walio safi kwa desturi za kiibada mwaweza kula kama vile mnavyokula paa au kulungu. 2315:23 Mwa 9:4; Kum 12:16; Eze 33:25; Law 7:26; 17:10Lakini kamwe msinywe damu; imwageni ardhini kama maji.