Kumbukumbu 14 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 14:1-29

Vyakula Vilivyo Najisi Na Vilivyo Safi

(Walawi 11:1-47)

114:1 Yn 1:12; Rum 8:14; 9:8; Yer 16:6; Mwa 6:2-4; Kut 4:22-23; Gal 3:26; 1The 4:13Ninyi ni watoto wa Bwana Mungu wenu. Msijichanje ama kujinyoa upara kwenye paji la uso kwa ajili ya aliyekufa, 214:2 Mwa 28:14; Kut 8:22; 22:31; Isa 6:13; Mt 2:15; Law 20:26; Rum 12:1; Kum 7:6; 26:18-1914:2 Kut 19:5; 2Sam 7:23, 24kwa maana ninyi ni taifa takatifu kwa Bwana Mungu wenu. Bwana amewachagua ninyi kuwa taifa la kipekee kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia, mwe tunu yake.

314:3 Eze 4:14; Isa 65:4; Mdo 10:13; Rum 14:14Msile kitu chochote ambacho ni machukizo. 414:4 Mdo 10:14; Law 7:23; 11:2-45Hawa ndio wanyama mtakaokula: ngʼombe, kondoo, mbuzi, 514:5 Kum 12:15; Ay 39:1; Za 104:18kulungu, paa, kongoni, paa mweupe, mbuzi-mwitu, pofu na kondoo wa mlimani. 6Mnaweza kumla mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika mara mbili, pia yule anayecheua. 7Hata hivyo, miongoni mwa wale wanaocheua au wale walio na kwato zilizogawanyika kamwe msile ngamia, sungura na pelele. Iwapo wanacheua, lakini hawana kwato zilizogawanyika; ni najisi kwenu kwa taratibu za kiibada. 814:8 Law 5:12; 11:26-27Nguruwe pia ni najisi; ingawa ana kwato zilizogawanyika, hacheui. Msile nyama yake wala kugusa mzoga wake.

9Katika viumbe hai vyote viishivyo kwenye maji, mnaweza kula yeyote aliye na mapezi na magamba. 10Lakini chochote kisicho na mapezi na magamba msile; kwenu ni najisi.

11Mnaweza kula ndege yeyote aliye safi. 1214:12 Law 11:13Lakini wafuatao msiwale: tai, furukombe, kipungu, 1314:13 Mwa 2:11; Isa 34:15kengewa mwekundu, kengewa mweusi, mwewe wa aina yoyote, 1414:14 Mwa 8:17kunguru wa aina yoyote, 15mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga wa aina yoyote, 16bundi, mumbi, bundi mkubwa, 1714:17 Za 102:6; Isa 13:21; 14:23; 34:11; Sef 2:14mwari, nderi, mnandi, 18korongo, koikoi wa aina yoyote, hudihudi na popo.

19Wadudu wote warukao kwa makundi ni najisi kwenu, msiwale. 2014:20 Law 20:25Lakini viumbe vyote vyenye mabawa vilivyo safi mwaweza kula.

2114:21 Law 11:39; 14:2; 17:15; Kut 23:19; 22:31; Law 22:8; Eze 44:31Msile kitu chochote mtakachokuta kimekufa. Mnaweza kumpa mgeni yeyote anayeishi katika mojawapo ya miji yenu, naye anaweza kula au mnaweza kumuuzia mtu wa nchi nyingine. Lakini ninyi ni watu watakatifu kwa Bwana Mungu wenu.

Msitokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

Zaka

2214:22 Mwa 14:20; Law 27:30; Hes 18:21; Neh 10:37; Kum 12:6, 17Hakikisheni mmetenga sehemu ya kumi ya mazao yote ya mashamba yenu kila mwaka. 2314:23 Kum 12:5, 17, 18; Za 4:7; 1Fal 3:2; Kum 4:10; Za 22:23; 33:8; Mal 2:5; Mit 3:13; Isa 8:13; Yer 32:38-41; Ebr 12:28Mtakula zaka za nafaka yenu, divai mpya, mafuta na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ngʼombe na ya kondoo na mbuzi mbele za Bwana Mungu wenu pale mahali atakapopachagua kama maskani kwa ajili ya Jina lake, ili kwamba mpate kujifunza kumheshimu Bwana Mungu wenu daima. 2414:24 Kum 12:21Lakini ikiwa mahali pale ni mbali sana nanyi mmebarikiwa na Bwana Mungu wenu na hamwezi kubeba zaka yenu (kwa sababu mahali pale Bwana atakapopachagua kuliweka Jina lake ni mbali sana), 2514:25 Mt 21:12; Yn 2:14basi badilisheni zaka yenu kuwa fedha, mkaichukue hiyo fedha mwende nayo mahali Bwana Mungu wenu atakapopachagua. 2614:26 Law 10:9; 23:40; Mhu 10:16-17; Kum 12:7-8Tumieni hiyo fedha kununua chochote ukitakacho: ngʼombe, kondoo, divai au kinywaji chochote chenye chachu au chochote mnachotaka. Kisha ninyi na wa nyumbani mwenu mtaila mbele za Bwana Mungu wenu na kufurahi. 2714:27 Kum 12:19; Hes 18:20; 26:62; Kum 18:1-2; Rum 13:4; 15:27; 1Kor 9:1-14Msiache kuwajali Walawi waishio katika miji yenu, kwa kuwa hao hawana shamba wala urithi wao wenyewe.

2814:28 Law 27:30; Kum 26:12Mwishoni mwa kila mwaka wa tatu, leteni zaka zote za mazao ya miaka ile na uyahifadhi kwenye miji yenu, 2914:29 Mwa 47:22; Hes 26:62; Kum 16:11; 24:19-21; Za 94:6; Isa 1:17; 58:6; Kum 6:11; 15:10; Za 41:1; Mit 22:9; Mt 3:10; Kum 10:18; Eze 22:7, 29; Lk 14:12; Ebr 13:2; Mal 3:10; Lk 11:41; 2Kor 9:6-11ili Walawi (ambao hawana mashamba wala urithi wao wenyewe) na wageni, yatima na wajane wanaoishi kwenye miji yenu wapate kuja kula na kushiba, ili Bwana Mungu wenu apate kuwabariki ninyi katika kazi zote za mikono yenu.