Kumbukumbu 13 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 13:1-18

Kuabudu Miungu Mingine

113:1 Mt 24:24; Mk 13:22; 2The 2:9; Mwa 20:3; Yer 23:25; 27:9; 29:8Kama nabii, au yule anayetabiri kwa njia ya ndoto, akijitokeza miongoni mwenu na akawatangazia ishara ya miujiza na ajabu, 213:2 Kum 11:28; 18:22; 1Sam 2:34; 10:9; 2Fal 19:29; 20:9; Isa 7:11; Kum 11:28ikiwa ishara au ajabu ya aliyozungumza ikatokea, naye akasema, “Na tufuate miungu mingine” (miungu ambayo hamjaifahamu) “na tuiabudu,” 313:3 2Pet 2:1; 1Sam 28:6; Mwa 22:1; 1Fal 13:18; 22:23; Yer 29:31; 43:2; Eze 13:9; 1Kor 11:19; Kum 6:5kamwe msiyasikilize maneno ya nabii wala mwota ndoto huyo. Bwana Mungu wenu anawajaribu kuangalia kama mnampenda kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote. 413:4 2Fal 23:8; 2Nya 34:31; 2Yn 6; Kum 6:13; 10:20; Za 5:7Ni Bwana Mungu wenu ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye. 513:5 Kut 21:12; 22:20; Kum 4:19; 17:7-12; 19:19; 24:7; Amu 20:13; 1Kor 5:13Huyo nabii au mwota ndoto lazima auawe, kwa sababu amehubiri uasi dhidi ya Bwana Mungu wenu, ambaye aliwatoa kutoka nchi ya Misri na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa; amejaribu kuwageuza kutoka njia ambayo Bwana Mungu wenu aliwaagiza mfuate. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.

613:6 Kum 17:2-7; 29:18; 11:28Kama ndugu yako hasa, au mwanao au binti yako, au mke umpendaye, au rafiki yako wa karibu sana akikushawishi kwa siri, akisema, “Na twende tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo ninyi wala baba zenu hamkuifahamu, 7miungu ya watu wanaowazunguka, ikiwa karibu au mbali, kutoka mwisho mmoja wa nchi mpaka mwingine), 813:8 Mit 1:10; Kum 7:2; Kut 20:3; Gal 1:8-9; 1Yn 5:21usikubali wala usimsikilize. Usimhurumie! Usimwache wala usimkinge. 913:9 Law 24:14; Kum 17:5-7; Mdo 7:58Hakika ni lazima auawe. Ni lazima mkono wako uwe wa kwanza katika kumuua kisha mikono ya watu wengine wote. 1013:10 Kut 20:3Mpigeni kwa mawe mpaka afe, kwa sababu alijaribu kuwageuza mtoke kwa Bwana Mungu wenu ambaye aliwatoa Misri, kutoka nchi ya utumwa. 1113:11 Kum 17:13; 19:20; 21:21; 1Tim 5:20Kisha Israeli wote watasikia na kuogopa, wala hakuna mmoja miongoni mwenu atakayefanya uovu tena.

1213:12 Yos 22:11; Amu 20:1Kama mkisikia ikisemwa kwamba moja ya miji ambayo Bwana Mungu wenu anawapa mkae ndani yake 1313:13 Amu 19:22; 20:13; 1Sam 2:12; 10:27; 25:17; 1Fal 21:10; 1Yn 2:19kuna wanaume waovu wameinuka miongoni mwenu na wamewapotosha watu wa mji, wakisema, “Twendeni tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo hamkuifahamu), 1413:14 Amu 20:12; Kum 17:4ndipo itakubidi kuuliza, kupima na kuchunguza kwa makini. Kama ni kweli, tena ikihakikishwa kwamba jambo hili lichukizalo limefanyika miongoni mwenu, 1513:15 Isa 24:6; 34:5; 43:28; 47:6; Mao 2:6; Dan 9:11; Zek 8:13; Mal 4:6; Kut 22:20kwa hakika ni lazima mwaue kwa upanga wale wote wanaoishi katika mji ule. Uharibuni kabisa, pamoja na watu wake na mifugo yake. 1613:16 2Fal 25:9; Yer 39:9; 52:13; Eze 16:41; Kum 7:25-26; Yos 6:24; 8:28; Isa 7:16; 17:1; 24:10; 25:2; 27:10; 32:14-19; 37:26; Yer 49:2; Mik 1:6Kusanyeni nyara zote za mji katika uwanja wa wazi na kuuchoma mji kabisa pamoja na nyara zake zote kama sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana Mungu wenu. Utabaki kuwa magofu milele na hautajengwa tena. 1713:17 Kut 30:12; Mwa 12:2; 13:14; 26:24; 28:14; 43:14; Hes 25:4; Kum 30:3; 7:13Hakuna kimoja kati ya vitu vilivyolaaniwa kitakachokutwa mikononi mwenu, ili Bwana ageuze hasira yake kali. Atawahurumia na kuwa na rehema kwenu pia kuongeza idadi yenu, kama alivyowaahidi baba zenu, 1813:18 Kum 12:25-28; 12:25-28; Mt 6:33; 7:21-24kwa sababu mnamtii Bwana Mungu wenu, mkizishika amri zake zote zile ninazowapa leo na kufanya lile lililo jema machoni pake.