Kumbukumbu 10 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 10:1-22

Vibao Vingine Vya Amri Kumi

(Kutoka 34:1-10)

110:1 Kut 34:2; 25:10Wakati ule Bwana aliniambia, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza uje kwangu juu mlimani. Pia utengeneze Sanduku la mbao. 210:2 Kut 25:16, 21; 2Nya 5:10; 6:11Nitaandika juu ya vibao maneno yaliyokuwa katika vile vibao vya kwanza, ambavyo ulivivunja. Kisha utaviweka ndani ya Sanduku.”

310:3 Kut 37:1-9; 34:4; 26:5Hivyo nikatengeneza Sanduku kwa mti wa mshita, nikachonga pia vibao vya mawe kama vile vya kwanza, kisha nikakwea mlimani nikiwa na vibao viwili mikononi mwangu. 410:4 Kut 24:12; 34:28; 20; 1; Kum 9:10; Yer 31:33Bwana akaandika juu ya hivi vibao kile alichokuwa amekiandika kabla, Amri Kumi alizokuwa amewatangazia juu mlimani, kutoka kwenye moto siku ile ya kusanyiko. Bwana akanikabidhi. 510:5 Kut 19:11; 25:10; 25:21; 34:29; 40:21; 1Sam 8:3; 1Fal 8:9Kisha nikashuka kutoka mlimani na kuweka vibao ndani ya Sanduku nililokuwa nimelitengeneza, kama Bwana alivyoniagiza, navyo viko huko sasa.

610:6 Hes 33:30; 27:13; 20:25-28; Kut 6:23(Waisraeli walisafiri kutoka visima vya Yaakani hadi Mosera. Huko Aroni alifariki na kuzikwa, naye Eleazari mwanawe akachukua nafasi yake kama kuhani. 710:7 Hes 33:32-34; Za 42:1; Wim 5:12; Isa 32:2Kutoka pale, walisafiri hadi Gudgoda wakaendelea mpaka Yotbatha, nchi yenye vijito vya maji. 810:8 Hes 3:6; 10:33; 16:9; Mwa 48:20; 1Nya 23:26; Kum 18:5; 21:5; Law 9:22Wakati huo Bwana aliteua kabila la Lawi kulibeba Sanduku la Agano la Bwana, kusimama mbele za Bwana ili kutoa huduma, na kutangaza baraka kwa Jina lake, kama wanavyofanya mpaka leo. 910:9 Hes 18:20; Eze 44:28Hiyo ndiyo sababu ya Walawi kutokuwa na sehemu wala urithi miongoni mwa ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama Bwana Mungu wao alivyowaambia.)

1010:10 Kut 33:17; 34:28; Kum 9:18-19; 25Basi nilikaa mlimani kwa siku arobaini usiku na mchana, kama nilivyofanya mara ya kwanza, pia Bwana alinisikiliza hata wakati huu. Haikuwa nia yake kuwaangamiza. 11Bwana akaniambia, “Nenda, ukawaongoze watu katika njia yao ili kwamba waweze kuingia na kuimiliki nchi ile niliyowaapia baba zao kuwapa.”

Mche Bwana

1210:12 Mik 6:8; Kut 20:20; 1Fal 2:3; 3:3; 4:4; Kum 5:32; 5:33; 6:13; 6:5; 11:13; 28:47; Mt 22:37; 1Tim 1:5; Za 100:2; Kum 6:5; Za 119:2; Kum 5:32Na sasa, ee Israeli, Bwana Mungu wako anataka nini kwako ila kumcha Bwana Mungu wako, kwenda katika njia zake, kumpenda na kumtumikia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, 1310:13 Kum 4:2; 5:33; 6:25na kuyashika maagizo ya Bwana na amri zake ninazokupa leo kwa mafanikio yako mwenyewe?

1410:14 Za 148:4; Isa 19:1; Hab 3:8; Neh 9:6; Ay 35:5; Za 8:3; 89:11; 104:3; Kum 33:26; Za 115:16; 1Fal 8:27; Kut 19:5; Za 24:1; Mdo 17:24Mbingu, hata mbingu za juu sana, dunia na kila kitu kilichomo ndani yake, ni mali ya Bwana Mungu wako. 1510:15 Kum 4:37; Za 105:6; 135:4; Hes 14:8; Rum 11:28; 1Pet 2:9Hata hivyo Bwana alikuwa na shauku na baba zako, akawapenda na akawachagua ninyi, wazao wao, kuliko mataifa yote, kama ilivyo leo. 1610:16 Mwa 17:11; Law 26:41; Kum 30:6; Yer 32:39; Kut 32:9; 9:13; Yer 4:4; Kum 9:6Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena. 1710:17 Yos 22:22; Za 135:9; 136:2; Dan 2:47; 11:36; Za 136:3; 1Tim 6:15; Kum 7:21; 1:17; Mal 2:9; Kut 23:8; Law 19:16; Efe 6:9Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa. 1810:18 Kut 22:21, 22-24; 23:9; Law 19:33; Kum 27:19; Ay 29:13; Za 94:6; Isa 10:2; Yer 49:11; Hes 10:32Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi. 1910:19 Kum 7:12; Kut 22:21; Kum 24:19; Law 19:34; Eze 47:22-23Nanyi wapendeni wageni, kwa kuwa ninyi wenyewe mlikuwa wageni huko Misri. 2010:20 Mt 4:10; Kum 11:22; 13:4; 30:20; Yos 23:8; Rut 1:14; 2Fal 18:6; Za 119:31; Isa 38:3; Kut 20:7; Za 63:11Mche Bwana Mungu wako na umtumikie yeye. Shikamana naye kwa uthabiti na kuapa kwa jina lake. 2110:21 Kut 15:2; 1Sam 12:24; Za 126:2; 2Sam 7:23; Yer 17:14; Za 106:21-22Yeye ni sifa yako; yeye ni Mungu wako, ambaye alikutendea yale maajabu makubwa na ya kutisha uliyoyaona kwa macho yako mwenyewe. 2210:22 Mwa 34:30; 46:26; Mdo 7:14; Mwa 12:2; Hes 10:36Baba zako walioshuka kwenda Misri jumla yao walikuwa sabini, na sasa Bwana Mungu wako amekufanya wengi kama nyota za angani.

New International Version

Deuteronomy 10:1-22

Tablets Like the First Ones

1At that time the Lord said to me, “Chisel out two stone tablets like the first ones and come up to me on the mountain. Also make a wooden ark.10:1 That is, a chest 2I will write on the tablets the words that were on the first tablets, which you broke. Then you are to put them in the ark.”

3So I made the ark out of acacia wood and chiseled out two stone tablets like the first ones, and I went up on the mountain with the two tablets in my hands. 4The Lord wrote on these tablets what he had written before, the Ten Commandments he had proclaimed to you on the mountain, out of the fire, on the day of the assembly. And the Lord gave them to me. 5Then I came back down the mountain and put the tablets in the ark I had made, as the Lord commanded me, and they are there now.

6(The Israelites traveled from the wells of Bene Jaakan to Moserah. There Aaron died and was buried, and Eleazar his son succeeded him as priest. 7From there they traveled to Gudgodah and on to Jotbathah, a land with streams of water. 8At that time the Lord set apart the tribe of Levi to carry the ark of the covenant of the Lord, to stand before the Lord to minister and to pronounce blessings in his name, as they still do today. 9That is why the Levites have no share or inheritance among their fellow Israelites; the Lord is their inheritance, as the Lord your God told them.)

10Now I had stayed on the mountain forty days and forty nights, as I did the first time, and the Lord listened to me at this time also. It was not his will to destroy you. 11“Go,” the Lord said to me, “and lead the people on their way, so that they may enter and possess the land I swore to their ancestors to give them.”

Fear the Lord

12And now, Israel, what does the Lord your God ask of you but to fear the Lord your God, to walk in obedience to him, to love him, to serve the Lord your God with all your heart and with all your soul, 13and to observe the Lord’s commands and decrees that I am giving you today for your own good?

14To the Lord your God belong the heavens, even the highest heavens, the earth and everything in it. 15Yet the Lord set his affection on your ancestors and loved them, and he chose you, their descendants, above all the nations—as it is today. 16Circumcise your hearts, therefore, and do not be stiff-necked any longer. 17For the Lord your God is God of gods and Lord of lords, the great God, mighty and awesome, who shows no partiality and accepts no bribes. 18He defends the cause of the fatherless and the widow, and loves the foreigner residing among you, giving them food and clothing. 19And you are to love those who are foreigners, for you yourselves were foreigners in Egypt. 20Fear the Lord your God and serve him. Hold fast to him and take your oaths in his name. 21He is the one you praise; he is your God, who performed for you those great and awesome wonders you saw with your own eyes. 22Your ancestors who went down into Egypt were seventy in all, and now the Lord your God has made you as numerous as the stars in the sky.