Isaya 8 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 8:1-22

Ashuru, Chombo Cha Bwana

18:1 Kum 27:8; Ay 19:23; Yer 20:3; 51:60; Isa 30:8; 8:3; Hos 1:4Bwana akaniambia, “Chukua gombo kubwa, uandike juu yake kwa kalamu ya kawaida jina: Maher-Shalal-Hash-Bazi.8:1 Maher-Shalal-Hash-Bazi maana yake ni Haraka kuteka nyara, Upesi kwenye hizo nyara. 28:2 2Fal 16:10; Yos 24:22; Rut 4:9; Yer 10:10-12; 32:10Nami nitawaita kuhani Uria, na Zekaria mwana wa Yeberekia kama mashahidi wangu waaminifu.”

38:3 Kut 15:20; Mwa 3:15Kisha nikaenda kwa nabii mke, naye akapata mimba, akazaa mwana. Kisha Bwana akaniambia, “Mwite huyo mtoto Maher-Shalal-Hash-Bazi. 48:4 Isa 7:8, 16; Mwa 14:15; Isa 7:8Kabla mtoto hajaweza kusema ‘Baba yangu’ au ‘Mama yangu,’ utajiri wa Dameski na nyara za Samaria zitachukuliwa na mfalme wa Ashuru.”

5Bwana akasema nami tena:

68:6 Neh 3:15; Isa 5:24; 7:1; Yn 9:7“Kwa sababu watu hawa wamekataa maji ya Shilo yatiririkayo taratibu

wakamfurahia Resini na mwana wa Remalia,

78:7 Isa 7:20; Dan 11:40; Nah 1:8; 2Nya 28:20; Isa 17:12-13; 30:28; Yos 3:15; Isa 10:16kwa hiyo Bwana yu karibu kuleta dhidi yao

mafuriko makubwa ya Mto:8:7 Yaani Frati.

yaani mfalme wa Ashuru na fahari yake yote.

Yatafurika juu ya mifereji yake yote,

yatamwagikia juu ya kingo zake zote,

88:8 Isa 7:14; 28:15; 18:6; 46:11; Yer 4:13; 48:40na kufika hadi Yuda, yakizunguka kwa kasi juu yake,

yakipita katikati na yakifika hadi shingoni.

Mabawa yake yaliyokunjuliwa

yatafunika upana wa nchi yako,

Ee Imanueli!”8:8 Imanueli maana yake Mungu yu pamoja nasi.

98:9 Isa 17:12-13; Eze 38:7; 38:3; Zek 14:2-3; Ay 34:24; Yer 46:3; 6:4; Zek 14:2; Yos 6:5Inueni kilio cha vita, enyi mataifa,

na mkavunjwevunjwe!

Sikilizeni, enyi nyote nchi za mbali.

Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!

Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!

108:10 Ay 5:12; Isa 7:7, 14; Rum 8:31; Mit 19:21; Mt 1:23Wekeni mikakati yenu, lakini itashindwa;

fanyeni mipango yenu, lakini haitafanikiwa,

kwa maana Mungu yu pamoja nasi.8:10 Kiebrania ni Imanueli.

Mwogope Mungu

118:11 Eze 3:14; 2:8; 1:3Bwana alisema nami mkono wake wenye nguvu ukiwa juu yangu, akinionya nisifuate njia za taifa hili. Akasema:

128:12 Isa 36:6; 7:2; 20:5; 1Pet 3:14; Mt 10:28“Usiite fitina kila kitu ambacho watu hawa hukiita fitina,

usiogope kile wanachokiogopa,

wala usikihofu.

138:13 Hes 20:12; Isa 29:23; Kut 20:20Bwana Mwenye Nguvu Zote ndiye peke yake

ikupasaye kumheshimu kuwa mtakatifu,

ndiye peke yake utakayemwogopa,

ndiye peke yake utakayemhofu,

148:14 Rum 9:33; Eze 11:16; Isa 24:17-18; Za 118:22; Yer 6:21; Lk 2:34; Isa 4:6; Lk 20:18; Eze 3:20naye atakuwa mahali patakatifu;

lakini kwa nyumba zote mbili za Israeli atakuwa

jiwe lile linalosababisha watu kujikwaa

na mwamba wa kuwaangusha.

Kwa watu wa Yerusalemu,

atakuwa mtego na tanzi.

158:15 Lk 20:18; Isa 28:13; 59:10; Rum 9:32; Mt 4:19; Lk 20:18; Isa 59:10Wengi wao watajikwaa;

wataanguka na kuvunjika,

watategwa na kunaswa.”

168:16 Dan 8:26; 12:4; Yer 32:14; Rut 4:7; Isa 29:11-12Funga ushuhuda na kutia muhuri sheria

miongoni mwa wanafunzi wangu.

178:17 Kum 31:17; Za 27:14; 22:5; Ebr 2:13Nitamngojea Bwana,

ambaye ameificha nyumba ya Yakobo uso wake.

Nitaliweka tumaini langu kwake.

188:18 Mwa 33:5; Ebr 2:13; Kut 3:12; Lk 2:34; Eze 12:6; 24:24; 4:3; Kum 28:46; Eze 12:11; Za 9:11Niko hapa, pamoja na watoto ambao Bwana amenipa. Sisi ni ishara na mfano wake katika Israeli, kutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayeishi juu ya Mlima Sayuni.

198:19 1Sam 28:8; Isa 29:4; Hes 27:21; Law 19:31Wakati watu wanapowaambia ninyi kutafuta ushauri kwa waaguzi na wenye kuongea na mizimu, ambao hunongʼona na kunungʼunika, je, watu wasingeuliza kwa Mungu wao? Kwa nini watake shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai? 208:20 Mik 3:6; Isa 60:2; 1:10; Rut 4:7; Lk 16:29; Isa 9:2; 59:9; 9:2Kwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatasema sawasawa na neno hili, hawana mwanga wa mapambazuko. 218:21 Ay 18:12; Kut 22:28; Ay 30:3; Ufu 16:11Watazunguka katika nchi yote, wakiwa na dhiki na njaa. Watakapotaabika kwa njaa, watapatwa na hasira kali, nao, wakiwa wanatazama juu, watamlaani mfalme wao na Mungu wao. 228:22 Ay 15:24; 3:13; Isa 5:30; Ufu 16:10; Mt 25:30Kisha wataangalia duniani na kuona tu dhiki na giza, hofu na huzuni tupu, nao watasukumiwa kwenye giza nene kabisa.