Isaya 7 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 7:1-25

Ishara Ya Imanueli

17:1 2Fal 16:5; 2Nya 28:5; 2Fal 15:25, 37; 1Nya 3:13; Isa 8:6; 7:5, 9Wakati Ahazi mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, alipokuwa mfalme wa Yuda, Mfalme Resini wa Aramu,7:1 Yaani Shamu. na Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli walipanda kupigana dhidi ya Yerusalemu, lakini hawakuweza kuushinda.

27:2 2Sam 7:11; Amo 9:11; Hos 5:8; Isa 16:5; Yer 21:12; Isa 6:4; 22:22; 9:9; Dan 5:6; Hos 5:3Wakati huu nyumba ya Daudi iliambiwa, “Aramu wameungana na Efraimu.” Kwa hiyo mioyo ya Ahazi na watu wake ilitikiswa, kama miti ya msituni inavyotikiswa na upepo.

37:3 2Fal 18:17; Isa 36:2; 10:21-22Ndipo Bwana akamwambia Isaya, “Toka uende, wewe na mwanao Shear-Yashubu,7:3 Shear-Yashubu maana yake Mabaki Watarudi. mkutane na Ahazi huko mwisho wa mfereji wa Bwawa la Juu, kwenye barabara iendayo Shamba la Dobi. 47:4 Kum 3:2; 20:3; Mao 3:26; Zek 3:2; Mt 24:6; Isa 54:14; 30:15; 21:4; 8:12; 10:24; 51:13; Mwa 15:1Mwambie, ‘Uwe mwangalifu, utulie na usiogope. Usife moyo kwa ajili ya watu hawa wawili walio kama visiki vya kuni vifukavyo moshi, kwa ajili ya hasira kali ya Resini na Aramu na ya mwana wa Remalia. 57:5 Isa 6:1Aramu, Efraimu na mwana wa Remalia wamepanga shauri baya ili wakuangamize, wakisema, 67:6 Isa 24:3; 25:8; 28:10“Tuishambulie Yuda, naam, tuirarue vipande vipande na kuigawa miongoni mwetu, na kumtawaza mwana wa Tabeeli awe mfalme juu yake.” 77:7 Mdo 4:25; Isa 24:3; 25:8; 28:16; 8:10; 40:8; 46:10; 14:24; Za 2:1Lakini Bwana Mwenyezi asema hivi:

“ ‘Jambo hili halitatendeka,

halitatokea,

87:8 Mwa 3:15; 14:15; 2Sam 8:6; 2Fal 17:24; Isa 9:11; 17:1-3; 8:4; 17:1-3kwa kuwa kichwa cha Aramu ni Dameski,

na kichwa cha Dameski ni Resini peke yake.

Katika muda wa miaka sitini na mitano,

Efraimu atakuwa ameharibiwa

kiasi kwamba hataweza tena kuwa taifa.

97:9 2Nya 20:20; Isa 8:6-8; 30:12-14; 9:9; 9:1, 3; Za 20:8; 2Fal 15:29Kichwa cha Efraimu ni Samaria,

na kichwa cha Samaria

ni mwana wa Remalia peke yake.

Kama hamtasimama thabiti katika imani yenu,

hamtaimarika kamwe.’ ”

10Bwana akasema na Ahazi tena, 117:11 Kum 13:2; Za 139:8; Kut 7:9“Mwombe Bwana Mungu wako ishara, iwe kwenye vina virefu sana, au kwenye vimo virefu sana.”

127:12 Kum 4:34Lakini Ahazi akasema, “Sitaomba; sitamjaribu Bwana.”

137:13 Za 63:1; 118:28; Mwa 30:15; Isa 1:14; 49:4; 61:10Ndipo Isaya akasema, “Sikia sasa, ewe nyumba ya Daudi! Je, haitoshi kujaribu uvumilivu wa wanadamu? Je, mtaujaribu uvumilivu wa Mungu wangu pia? 147:14 Mwa 5:13; 21:22; 24:43; Kut 3:12; Lk 2:12; Mt 1:23; Mwa 3:15; 21:22; Lk 1:31Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara: Bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, na ataitwa Imanueli.7:14 Imanueli maana yake Mungu yu pamoja nasi. 157:15 Mwa 18:8; Isa 8:4; Kum 1:39; 13:16Atakula jibini na asali atakapokuwa ameweza kukataa mabaya na kuchagua mema. 167:16 Isa 8:4; 17:3; Yer 13:5; 7:15; Kum 13:16; 1:39; Hos 5:9-13Lakini kabla mtoto hajajua kukataa mabaya na kuchagua mema, nchi ya wafalme hao wawili unaowaogopa itafanywa ukiwa. 177:17 2Nya 28:20; 1Fal 12:16; Neh 9:32; 2Nya 7:18; Isa 17:9; 34:13Bwana ataleta juu yako, juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako wakati ambao haujawahi kuwako tangu Efraimu alipojitenga na Yuda: yeye atawaleteeni mfalme wa Ashuru.”

187:18 Isa 5:26; 13:5; 7:25Katika siku ile Bwana atawapigia filimbi mainzi kutoka vijito vya mbali vya Misri, na nyuki kutoka nchi ya Ashuru. 197:19 Isa 2:19; 7:25; 17:9; 34:13; 55:13Wote watakuja na kukaa kwenye mabonde yenye miteremko, na kwenye nyufa za miamba, kwenye vichaka vyote vyenye miiba, na kwenye mashimo yote ya maji. 207:20 Isa 10:15; 29:16; 8:7; 11:15; 2Fal 18:16; Yer 27:6-7; 2:18; 2Sam 10:4; Kum 28:40Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ngʼambo ya Mto,7:20 Yaani Frati. yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia. 217:21 Isa 2:17; Yer 39:10Katika siku ile, mtu atahifadhi hai ndama mmoja na kondoo wawili. 227:22 Mwa 18:8; Isa 14:30Kwa ajili ya wingi wa maziwa watakayotoa, atapata jibini ya kula. Wote watakaobakia katika nchi watakula jibini na asali. 237:23 Isa 5:6; 8:11; 7:2; Hos 2:12Katika siku ile, kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu moja yenye thamani ya shekeli 1,0007:23 Shekeli 1,000 ni kama kilo 11.5. za fedha, patakuwa na michongoma na miiba tu. 247:24 Isa 5:6Watu watakwenda huko wakiwa na upinde na mshale, kwa maana nchi itafunikwa na michongoma na miiba. 257:25 Isa 5:17; Hag 1:11Kuhusu vilima vyote vilivyokuwa vikilimwa kwa jembe, hamtakwenda huko tena kwa ajili ya hofu ya michongoma na miiba. Patakuwa mahali ambapo ngʼombe wataachiwa huru, na kondoo kukimbia kimbia.