Isaya 64 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 64:1-12

164:1 Kut 19:18; Mik 1:3; Za 18:9Laiti ungelipasua mbingu na kushuka chini,

ili milima ingelitetemeka mbele zako!

264:2 Za 119:120; Yer 5:22; Isa 30:27; Yer 33:9Kama vile moto uteketezavyo vijiti

na kusababisha maji kuchemka,

shuka ukafanye jina lako lijulikane kwa adui zako,

na kusababisha mataifa yatetemeke mbele zako!

364:3 Za 65:5; 18:7Kwa maana ulipofanya mambo ya kutisha ambayo hatukuyatazamia,

ulishuka, nayo milima ikatetemeka mbele zako.

464:4 Za 31:19; Isa 30:18; 1Kor 2:9-10; Kol 1:26-27; Isa 43:10-11; 30:18Tangu nyakati za zamani hakuna yeyote aliyesikia,

hakuna sikio lililotambua,

hakuna jicho lililomwona Mungu mwingine ila wewe,

anayetenda mambo kwa ajili ya wale wamngojeao.

564:5 Isa 26:8; Mdo 10:35; Isa 10:4Uliwasaidia watu wale watendao yaliyo haki kwa furaha,

wale wazikumbukao njia zako.

Lakini wakati tulipoendelea kutenda dhambi kinyume na njia zako,

ulikasirika.

Tutawezaje basi kuokolewa?

664:6 Isa 46:12; Za 90:5-6; Yer 4:12; Law 12:2Sisi sote tumekuwa kama mtu aliye najisi,

nayo matendo yetu yote ya uadilifu ni kama matambaa machafu;

sisi sote tunasinyaa kama jani,

na kama upepo maovu yetu hutupeperusha.

764:7 Eze 22:30; Yer 8:6; Isa 9:18; Eze 22:18-22; Isa 41:28; Kum 31:18; Za 14:4Hakuna yeyote anayeliitia jina lako

wala anayejitahidi kukushika,

kwa kuwa umetuficha uso wako

na kutuacha tudhoofike kwa sababu ya dhambi zetu.

864:8 Yer 18:6; Kut 4:22; Isa 63:16; 29:16; Yer 3:4; Rum 9:20-21; Ay 10:3Lakini, Ee Bwana, wewe ndiwe Baba yetu.

Sisi ni udongo, wewe ndiye mfinyanzi;

sisi sote tu kazi ya mkono wako.

964:9 Isa 54:8; Mao 5:22; Isa 43:25; Za 100:3; Isa 51:4; 57:17Ee Bwana, usikasirike kupita kiasi,

usizikumbuke dhambi zetu milele.

Ee Bwana, utuangalie, twakuomba,

kwa kuwa sisi sote tu watu wako.

1064:10 Za 78:54; Isa 1:26; Kum 29:23Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa;

hata Sayuni ni jangwa, Yerusalemu ni ukiwa.

1164:11 2Fal 25:9; Eze 24:21; Mao 1:7-10Hekalu letu takatifu na tukufu, mahali ambapo baba zetu walikusifu wewe,

limechomwa kwa moto,

navyo vitu vyote tulivyovithamini vimeharibika.

1264:12 Mwa 43:31; Za 74:10-11; Es 4:14; Za 50:21Ee Bwana, baada ya haya yote, utajizuia?

Je, utanyamaza kimya na kutuadhibu kupita kiasi?