Isaya 63 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 63:1-19

Siku Ya Mungu Ya Kisasi Na Ukombozi

163:1 Mwa 36:33; Amo 1:12; Yer 42:11; Sef 3:17; 2Nya 28:17; Isa 11:14; Ufu 19:13; Ay 9:4Ni nani huyu anayekuja kutoka Edomu,

kutoka Bosra, mwenye mavazi yaliyotiwa madoa mekundu?

Ni nani huyu, aliyevikwa joho la kifahari,

anayetembea kwa ukuu wa nguvu zake?

“Mimi ndimi, nisemaye katika haki,

mwenye nguvu wa kuokoa.”

263:2 Ufu 19:13; Mwa 49:11Kwa nini mavazi yako ni mekundu,

kama ya yule akanyagaye shinikizo la zabibu?

363:3 Amu 6:11; Ufu 19:15; Mao 1:15; Ufu 19:13; 14:19-20; Za 108:13“Nimekanyaga shinikizo la zabibu peke yangu;

kutoka mataifa hakuna mtu aliyekuwa pamoja nami.

Nimewaponda kwa miguu katika hasira yangu

na kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu;

damu yao ilitia matone kwenye mavazi yangu,

na kutia madoa nguo zangu zote.

463:4 Isa 1:24; Yer 50:15Kwa kuwa siku ya kisasi ilikuwa moyoni mwangu,

mwaka wa ukombozi wangu umefika.

563:5 2Fal 14:26; Isa 41:28; 59:16; Za 44:3; Yn 16:32; Isa 33:2Nilitazama, lakini hakuwepo yeyote wa kunisaidia,

nilishangaa kwa kuwa hakuwepo yeyote aliyetoa msaada;

hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu,

na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza.

663:6 Isa 29:9; Mao 4:21; Isa 34:3; Ay 40:12Nilikanyaga mataifa kwa miguu katika hasira yangu,

katika ghadhabu yangu niliwalewesha,

na kumwaga damu yao juu ya ardhi.”

Kusifu Na Kuomba

763:7 Isa 54:8; Efe 2:4; Kut 18:9Nitasimulia juu ya wema wa Bwana,

kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa,

sawasawa na yote ambayo Bwana

ametenda kwa ajili yetu:

naam, mambo mengi mema aliyoyatenda

kwa ajili ya nyumba ya Israeli,

sawasawa na huruma zake

na wema wake mwingi.

863:8 Mdo 9:4; Kut 14:19; 33:14; Kum 7:7-8; Ezr 9:9; Za 28:9; Ay 37:23Alisema, “Hakika wao ni watu wangu,

wana ambao hawatanidanganya”;

hivyo akawa Mwokozi wao.

963:9 Kut 14:19; 33:14; Kum 7:7-8; Ezr 9:9; Isa 48:20; Kum 1:31; 32:7; Za 28:9; Ay 37:23Katika taabu zao zote naye alitaabika,

na malaika wa uso wake akawaokoa.

Katika upendo wake na rehema zake aliwakomboa,

akawainua na kuwachukua siku zote zilizopita.

1063:10 Eze 20:8; Mdo 7:39-42; Efe 4:30; Za 106:40; 78:17; Isa 10:4; Yos 10:14Lakini waliasi,

na kumhuzunisha Roho Mtakatifu wake.

Hivyo aligeuka na kuwa adui yao,

na yeye mwenyewe akapigana dhidi yao.

1163:11 Kut 14:22, 30; Hes 11:17; Za 77:20Ndipo watu wake wakazikumbuka siku zilizopita,

siku za Mose na watu wake:

yuko wapi yeye aliyewaleta kupitia katikati ya bahari,

pamoja na wachungaji wa kundi lake?

Yuko wapi yule aliyeweka

Roho wake Mtakatifu katikati yao,

1263:12 Kut 14:21-22; Isa 11:15; Mwa 49:24aliyetuma mkono wake uliotukuka wenye nguvu

kuwa katika mkono wa kuume wa Mose,

aliyegawa maji ya bahari mbele yao,

ili kujipatia jina milele,

1363:13 Kum 32:12; Yer 31:9; Kut 14:24; Za 119:11aliyewaongoza kupitia kwenye vilindi?

Kama farasi katika nchi iliyo wazi,

wao hawakujikwaa,

1463:14 Kut 33:14; Kum 12:9kama ngʼombe washukao bondeni kwenye malisho,

walipewa pumziko na Roho wa Bwana.

Hivi ndivyo ulivyowaongoza watu wako

ili kujipatia mwenyewe jina tukufu.

1563:15 Za 80:14; Mao 3:50; 1Fal 22:19; 2:26; Hos 11:8; Kum 26:15; Isa 64:12Tazama chini kutoka mbinguni ukaone

kutoka kiti chako cha enzi

kilichoinuliwa juu, kitakatifu na kitukufu.

Uko wapi wivu wako na uweza wako?

Umetuzuilia wema wako na huruma zako.

1663:16 Ay 14:21; Gal 3:28; Isa 44:6; Kut 4:22; Yer 3:4; Yn 8:41; Isa 59:20Lakini wewe ni Baba yetu,

ingawa Abrahamu hatufahamu sisi

wala Israeli hatutambui;

wewe, Ee Bwana, ndiwe Baba yetu,

Mkombozi wetu tangu zamani za kale ndilo jina lako.

1763:17 Isa 6:10; 29:13; Hes 10:36; Mt 13:15; Mwa 20:13; Mao 3:9; Kut 4:21; 34:9Ee Bwana, kwa nini unatuacha twende mbali na njia zako,

na kuifanya mioyo yetu migumu hata hatukukuheshimu?

Rudi kwa ajili ya watumishi wako,

yale makabila ambayo ni urithi wako.

1863:18 Law 26:31; Dan 8:24; Za 74:3-8; Kum 4:26; Isa 28:18; Lk 21:24; Dan 8:13Kwa maana kwa muda mfupi watu wako walimiliki mahali pako patakatifu,

lakini sasa adui zetu wamepakanyaga mahali patakatifu pako.

1963:19 Isa 43:7; Yer 14:9Sisi tumekuwa kama wale ambao hujawatawala kamwe,

kama wale ambao hawajaitwa kwa jina lako.