Isaya 59 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 59:1-21

Dhambi, Toba Na Ukombozi

159:1 Hes 11:23; Isa 50:2; 30:19; 41:20; 58:9; 65:24Hakika mkono wa Bwana si mfupi hata usiweze kuokoa,

wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia.

259:2 Za 18:41; Yn 9:31; Yer 11:11; Isa 58:4; Eze 39:23; Yer 5:25Lakini maovu yenu yamewatenga

ninyi na Mungu wenu,

dhambi zenu zimewaficha ninyi uso wake,

ili asisikie.

359:3 2Fal 21:16; Eze 22:9; Rum 3:15; Isa 1:15; Za 7:3; Isa 3:8Kwa maana mikono yenu imetiwa mawaa kwa damu

na vidole vyenu kwa hatia.

Midomo yenu imenena uongo,

nazo ndimi zenu zimenongʼona mambo maovu.

459:4 Za 7:14; Yak 1:15; Isa 5:23; Ay 15:31; Isa 44:20; 29:20; Ay 4:8Hakuna hata mmoja anayedai kwa haki;

hakuna hata mmoja anayetetea shauri lake kwa haki.

Wanategemea mabishano matupu na kusema uongo,

huchukua mimba ya magomvi na kuzaa uovu.

559:5 Ay 8:14; Mt 3:7; Isa 11:8Huangua mayai ya nyoka wenye sumu kali

na kutanda wavu wa buibui.

Yeyote alaye mayai yao atakufa,

na wakati moja lianguliwapo, nyoka hutoka humo.

659:6 Isa 28:20; Mit 4:17; Za 55:9; Isa 58:4Utando wao wa buibui haufai kwa nguo;

hawawezi kujifunika kwa kile walichokitengeneza.

Matendo yao ni matendo maovu,

vitendo vya jeuri vipo mikononi mwao.

759:7 2Fal 21:16; Mik 3:10; Mit 6:17; Rum 3:15-17; Mk 7:21-22Miguu yao hukimbilia kwenye dhambi,

ni myepesi kumwaga damu isiyo na hatia.

Mawazo yao ni mawazo maovu;

uharibifu na maangamizi huonekana katika njia zao.

859:8 Mit 2:15; Isa 57:21; Lk 1:79; Amu 5:6; Rum 3:15-17Hawajui njia ya amani,

hakuna haki katika mapito yao.

Wameyageuza kuwa njia za upotovu,

hakuna apitaye njia hizo atakayeifahamu amani.

959:9 Yer 8:15; Ay 19:8; Za 107:14; Isa 5:30; 8:20; Lk 1:79Hivyo uadilifu uko mbali nasi,

nayo haki haitufikii.

Tunatazamia nuru, kumbe! Yote ni giza,

tunatazamia mwanga, lakini tunatembea katika giza kuu.

1059:10 Mao 4:14; Sef 1:17; Ay 3:23; Yn 11:10; Kum 28:29; Isa 6:9-10; Mao 3:6Tunapapasa ukuta kama kipofu,

tunapapasa katika njia zetu kama watu wasio na macho.

Adhuhuri tunajikwaa kama wakati wa gizagiza;

katikati ya wenye nguvu, tuko kama wafu.

1159:11 Eze 7:16Wote tunanguruma kama dubu;

tunalia kwa maombolezo kama hua.

Tunatafuta haki, kumbe hakuna kabisa;

tunatafuta wokovu, lakini uko mbali.

1259:12 Ezr 9:6; Yer 2:19; Mwa 4:7; Isa 57; 12; 3:9; Yer 51:3Kwa sababu makosa yetu ni mengi machoni pako,

na dhambi zetu zinashuhudia dhidi yetu.

Makosa yetu yako pamoja nasi daima,

nasi tunayatambua maovu yetu:

1359:13 Hes 11:20; Za 12:5; Mt 12:34; Mk 7:21-22; Mit 30; 9; Tit 1:16; Isa 48:8Uasi na udanganyifu dhidi ya Bwana,

kumgeuzia Mungu wetu kisogo,

tukichochea udhalimu na maasi,

tukinena uongo ambao mioyo yetu imeuhifadhi.

1459:14 Neh 8:1; Isa 48:1; Yer 33:16; Isa 29:21; 1:21Hivyo uadilifu umerudishwa nyuma,

nayo haki inasimama mbali,

kweli imejikwaa njiani,

uaminifu hauwezi kuingia.

1559:15 Yer 7:28; Dan 8:12; Isa 5:7Kweli haipatikani popote,

na yeyote aepukaye uovu huwa mawindo.

Bwana alitazama naye akachukizwa

kwamba hapakuwepo haki.

1659:16 Isa 41:28; 65:3; Za 98:1; Isa 53:12; 46:13Aliona kuwa hakuwepo hata mtu mmoja,

akashangaa kwamba hakuwepo hata mmoja wa kuingilia kati;

hivyo mkono wake mwenyewe

ndio uliomfanyia wokovu,

nayo haki yake mwenyewe

ndiyo iliyomtegemeza.

1759:17 Efe 6:14; 1The 5:8; Ay 27:6; Eze 5:13; Efe 6:17; Isa 63:3Alivaa haki kama dirii kifuani mwake,

na chapeo ya wokovu kichwani mwake,

alivaa mavazi ya kisasi

naye akajifunga wivu kama joho.

1859:18 Hes 10:35; Isa 34:8; Mt 16:27Kulingana na kile walichokuwa wametenda,

ndivyo atakavyolipa

ghadhabu kwa watesi wake

na kisasi kwa adui zake,

atavilipa visiwa sawa na wanavyostahili.

1959:19 Isa 49:12; Za 113:3; Ufu 12:15; Mt 8:11; Za 97:6Kuanzia magharibi, watu wataliogopa jina la Bwana

na kuanzia mawio ya jua, watauheshimu utukufu wake.

Wakati adui atakapokuja kama mafuriko,

Roho wa Bwana atainua kiwango dhidi yake na kumshinda.

2059:20 Yer 35:15; Mdo 2:38-39; Rum 11:26; Ay 19:25; Isa 52:8; Yoe 3:21; Yer 35:15“Mkombozi atakuja Sayuni,

kwa wale wa Yakobo

wanaozitubu dhambi zao,”

asema Bwana.

2159:21 Isa 44:3; Ebr 8:10; Eze 36:37; Mwa 9:16; Kum 29:14; Isa 42:6; Kut 4:15“Kwa habari yangu mimi, hili ndilo agano langu nao,” asema Bwana. “Roho wangu, aliye juu yenu, na maneno yangu ambayo nimeyaweka katika vinywa vyenu, havitaondoka vinywani mwenu, wala kutoka vinywani mwa watoto wenu, wala kutoka vinywani mwa wazao wao, kuanzia sasa na hata milele,” asema Bwana.