Isaya 58 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 58:1-14

Mfungo Wa Kweli

158:1 Isa 24:20; 40:6; 48:8; Eze 3:17; Isa 57:12“Piga kelele, usizuie.

Paza sauti yako kama tarumbeta.

Watangazieni watu wangu uasi wao,

na kwa nyumba ya Yakobo dhambi zao.

258:2 Isa 29:13; Yak 4:8Kwa maana kila siku hunitafuta,

wanaonekana kutaka kujua njia zangu,

kana kwamba walikuwa taifa linalotenda lililo sawa,

na ambalo halijaziacha amri za Mungu wake.

Hutaka kwangu maamuzi ya haki,

nao hutamani Mungu awakaribie.

358:3 Law 16:29; Mal 3:14; Zek 7:5-6; Kut 10:3; 2Nya 6:37; Yer 44:10; Isa 22:13Wao husema, ‘Mbona tumefunga, nawe hujaona?

Mbona tumejinyenyekeza, nawe huangalii?’

“Lakini katika siku ya kufunga kwenu, mnafanya mnavyotaka

na kuwadhulumu wafanyakazi wenu wote.

458:4 Mal 2:16; Mao 3:44; Mik 3:4; 1Fal 21:9-13; Isa 59:6; Eze 7:11; 8:18; 1Sam 8:18Kufunga kwenu huishia kwenye magomvi na mapigano,

na kupigana ninyi kwa ninyi kwa ngumi za uovu.

Hamwezi kufunga kama mnavyofanya leo

na kutazamia sauti zenu kusikiwa huko juu.

558:5 Zek 7:5; 1Fal 21:27; Mt 6:16; Ay 2:8; Isa 36:6Je, hii ndiyo aina ya mfungo niliouchagua,

siku moja tu ya mtu kujinyenyekeza?

Je, ni kwa kuinamisha kichwa chini kama tete,

na kwa kujilaza juu ya nguo ya gunia na majivu?

Je, huo ndio mnaouita mfungo,

siku iliyokubalika kwa Bwana?

658:6 Neh 5:10-11; Kum 14:29; Lk 4:19; Yoe 2:12-13; Yer 34:9; Amo 4:1; Isa 9:4“Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua:

kufungua minyororo ya udhalimu,

na kufungua kamba za nira,

kuwaweka huru walioonewa,

na kuvunja kila nira?

758:7 Ay 22:7; Dan 4:27; Ebr 13:12; Ay 31:19-20; Mwa 29:14; Mt 25:36; Eze 18:16Je, sio kushirikiana chakula chako na wenye njaa

na kuwapatia maskini wasiokuwa na makao hifadhi,

unapomwona aliye uchi, umvike,

wala si kumkimbia mtu wa nyama na damu yako mwenyewe?

858:8 Isa 9:2; 30:26; Kut 14:19; Ay 11:17; Isa 26:2Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko

na uponyaji wako utatokea upesi;

ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako,

na utukufu wa Bwana utakuwa mlinzi nyuma yako.

958:9 Mit 6:13; Za 50:12; 12:2; Isa 59:13; Ay 8:6; Dan 9:20; Zek 10:6Ndipo utaita, naye Bwana atajibu,

utalia kuomba msaada,

naye atasema: Mimi hapa.

“Kama ukiiondoa nira ya udhalimu,

na kunyoosha kidole na kuzungumza maovu,

1058:10 Kum 15:7-8; Ay 11:17; Isa 42:16nanyi kama mkimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi zenu

na kutosheleza mahitaji ya walioonewa,

ndipo nuru yenu itakapongʼaa gizani,

nao usiku wenu utakuwa kama adhuhuri.

1158:11 Za 104:28; Wim 4:15; Yn 4:14; Za 48:14; Isa 42:16; 48:7; Za 68:1; 72:6Bwana atakuongoza siku zote,

atayatosheleza mahitaji yako katika nchi kame,

naye ataitia nguvu mifupa yako.

Utakuwa kama bustani iliyonyweshwa vizuri,

kama chemchemi ambayo maji yake hayakauki kamwe.

12Watu wako watajenga tena magofu ya zamani

na kuinua misingi ya kale;

utaitwa Mwenye Kukarabati Kuta Zilizobomoka,

Mwenye Kurejeza Barabara za Makao.

1358:13 Law 19:20; Kut 20:8; Za 37:4; Isa 56:2“Kama ukitunza miguu yako isivunje Sabato,

na kutokufanya kama vile upendavyo katika siku yangu takatifu,

kama ukiita Sabato siku ya furaha

na siku takatifu ya Bwana ya kuheshimiwa,

kama utaiheshimu kwa kutoenenda

katika njia zako mwenyewe,

na kutokufanya yakupendezayo

au kusema maneno ya upuzi,

1458:14 Ay 22:26; Kum 32:13; Isa 1:20; Za 105:10-11ndipo utakapojipatia furaha yako katika Bwana,

nami nitakufanya upande juu ya miinuko ya nchi

na kusherehekea urithi wa Yakobo baba yako.”

Kinywa cha Bwana kimenena haya.