Isaya 57 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 57:1-21

Ibada Ya Sanamu Ya Israeli Iliyo Batili

157:1 Eze 21:3; 2Fal 22:20; Za 12:1; Isa 42:25Mwenye haki hupotea,

wala hakuna hata mmoja awazaye hilo moyoni mwake;

watu wanaomcha Mungu huondolewa,

wala hakuna hata mmoja anayeelewa

kuwa wenye haki wameondolewa

ili wasipatikane na maovu.

257:2 Isa 26:7; Kum 12:13Wale waendao kwa unyofu

huwa na amani;

hupata pumziko walalapo mautini.

357:3 Mal 3:5; Yak 4:4; Yer 2:20; Kut 22:18; Mt 16:4; Isa 1:20“Lakini ninyi:

Njooni hapa, ninyi wana wa wachawi,

ninyi wazao wa wazinzi na makahaba!

457:4 Isa 1:2Mnamdhihaki nani?

Ni nani mnayemcheka kwa dharau,

na kumtolea ndimi zenu?

Je, ninyi si watoto wa waasi,

uzao wa waongo?

557:5 Kum 12:2; 2Fal 16:4; Eze 16:20; Kum 18:10; Isa 1:29; Law 18:21; 18:2; Za 106:37-38Mnawaka tamaa katikati ya mialoni

na chini ya kila mti uliotanda matawi;

mnawatoa kafara watoto wenu kwenye mabonde

na chini ya majabali yenye mianya.

657:6 2Fal 17:10; Hab 2:19; Yer 44:18; 19:13; 7:18; 3:9; 7:18; 5:9-29; 9:9; 2:19“Sanamu zilizo katikati ya mawe laini ya mabondeni ndizo fungu lenu;

hizo ndizo sehemu yenu.

Naam, kwa hizo mmemimina sadaka za vinywaji,

na kutoa sadaka za nafaka.

Katika haya yote,

niendelee kuona huruma?

757:7 Yer 3:6; Eze 6:3; 23:41; 20:29; 20:27-28Umeweka kitanda chako juu kwenye kilima kirefu kilichoinuka,

huko ulikwenda kutoa dhabihu zako.

857:8 Eze 16:26; 23:7, 18; 23:18Nyuma ya milango yako na miimo yako

umeweka alama zako za kipagani.

Kwa kuniacha mimi, ulifunua kitanda chako,

umepanda juu yake na kukipanua sana;

ulifanya patano na wale ambao unapenda vitanda vyao,

nawe uliangalia uchi wao.

957:9 Law 18:21; 1Fal 11:5; Wim 4:10; Eze 23:16, 40Ulikwenda kwa Moleki57:9 Moleki alikuwa mungu aliyekuwa anaabudiwa na Waamoni; pia alijulikana kama Malkomu, Maloki au Kemoshi wa Moabu. ukiwa na mafuta ya zeituni,

na ukaongeza manukato yako.

Ukawatuma wajumbe wako mbali sana,

ukashuka kwenye kaburi57:9 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. lenyewe!

1057:10 Yer 18:12; Mal 3:14; Isa 47:13; Yer 2:25; 1Sam 2:4Ulikuwa umechoshwa na njia zako zote,

lakini hukusema, ‘Hakuna tumaini.’

Ulipata uhuisho wa nguvu zako,

kwa sababu hiyo hukuzimia.

1157:11 Mit 29:25; Eze 22:12; Yer 18:15; Es 4:14; Za 50:21; Yer 3:21; 1Fal 1:15; Isa 17:10“Ni nani uliyemhofu hivyo na kumwogopa

hata ukawa mwongo kwangu,

wala hukunikumbuka

au kutafakari hili moyoni mwako?

Si ni kwa sababu nimekuwa kimya muda mrefu

hata huniogopi?

1257:12 Eze 16:2; Mik 2:2-8; Isa 29:15; 66:18Nitaifunua haki yako na matendo yako,

nayo hayatakufaidi.

1357:13 Za 37:3-9; Yer 30:15; Isa 2:2-3; Yer 22:20; Amu 10:14; Za 118:8; Isa 65:9-11Utakapolia kwa kuhitaji msaada,

sanamu zako ulizojikusanyia na zikuokoe!

Upepo utazipeperusha zote,

pumzi peke yake itazipeperusha,

Lakini mtu atakayenifanya kimbilio lake,

atairithi nchi

na kuumiliki mlima wangu mtakatifu.”

Faraja Kwa Wenye Majuto

1457:14 Isa 62:10; Yer 18:15; Isa 11:16Tena itasemwa:

“Jengeni, jengeni, itengenezeni njia!

Ondoeni vikwazo katika njia ya watu wangu.”

1557:15 Kum 33:27; Ay 6:10; Mik 6:8; Za 90:2; 2Fal 22:19; Zek 2:13; Isa 52:13; Ay 16:19Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu, yeye aliyeinuliwa sana,

yeye aishiye milele, ambaye jina lake ni Mtakatifu:

“Ninaishi mimi mahali palipoinuka na patakatifu,

lakini pia pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu

na mwenye roho ya unyenyekevu,

ili kuzihuisha roho za wanyenyekevu

na kuihuisha mioyo yao waliotubu.

1657:16 Za 85:5; Mik 7:18; Ebr 12:9; Isa 3:13-14; 54:9; Zek 12:1Sitaendelea kulaumu milele,

wala sitakasirika siku zote,

kwa kuwa roho ya mwanadamu

ingezimia mbele zangu:

yaani pumzi ya mwanadamu niliyemuumba.

1757:17 Isa 56:11; Yer 8:10; Isa 30:15; 53:6; 66:3Nilighadhibika na tamaa yake ya dhambi;

nilimwadhibu, nikauficha uso wangu kwa hasira,

na bado aliendelea katika njia zake za tamaa.

1857:18 Kum 32:39; 2Nya 7:14; Isa 49:13; Za 48:14; Isa 42:16; 48:17Nimeziona njia zake, lakini nitamponya,

nitamwongoza na kumrudishia upya faraja,

1957:19 Isa 51:16; Ebr 13:15; Efe 2:17; Mdo 2:39; Lk 2:14; Isa 32:17; 26:3nikiumba sifa midomoni ya waombolezaji

katika Israeli.

Amani, amani, kwa wale walio mbali

na kwa wale walio karibu,”

asema Bwana. “Nami nitawaponya.”

2057:20 Ay 18:5-21; Mwa 49:4; Efe 4:14; Yud 13; Za 69:14Bali waovu ni kama bahari ichafukayo,

ambayo haiwezi kutulia,

mawimbi yake hutupa takataka na matope.

2157:21 Isa 26:3; Eze 13:16; Isa 59:8; 48:22Mungu wangu asema,

“Hakuna amani kwa waovu.”

New International Version

Isaiah 57:1-21

1The righteous perish,

and no one takes it to heart;

the devout are taken away,

and no one understands

that the righteous are taken away

to be spared from evil.

2Those who walk uprightly

enter into peace;

they find rest as they lie in death.

3“But you—come here, you children of a sorceress,

you offspring of adulterers and prostitutes!

4Who are you mocking?

At whom do you sneer

and stick out your tongue?

Are you not a brood of rebels,

the offspring of liars?

5You burn with lust among the oaks

and under every spreading tree;

you sacrifice your children in the ravines

and under the overhanging crags.

6The idols among the smooth stones of the ravines are your portion;

indeed, they are your lot.

Yes, to them you have poured out drink offerings

and offered grain offerings.

In view of all this, should I relent?

7You have made your bed on a high and lofty hill;

there you went up to offer your sacrifices.

8Behind your doors and your doorposts

you have put your pagan symbols.

Forsaking me, you uncovered your bed,

you climbed into it and opened it wide;

you made a pact with those whose beds you love,

and you looked with lust on their naked bodies.

9You went to Molek57:9 Or to the king with olive oil

and increased your perfumes.

You sent your ambassadors57:9 Or idols far away;

you descended to the very realm of the dead!

10You wearied yourself by such going about,

but you would not say, ‘It is hopeless.’

You found renewal of your strength,

and so you did not faint.

11“Whom have you so dreaded and feared

that you have not been true to me,

and have neither remembered me

nor taken this to heart?

Is it not because I have long been silent

that you do not fear me?

12I will expose your righteousness and your works,

and they will not benefit you.

13When you cry out for help,

let your collection of idols save you!

The wind will carry all of them off,

a mere breath will blow them away.

But whoever takes refuge in me

will inherit the land

and possess my holy mountain.”

Comfort for the Contrite

14And it will be said:

“Build up, build up, prepare the road!

Remove the obstacles out of the way of my people.”

15For this is what the high and exalted One says—

he who lives forever, whose name is holy:

“I live in a high and holy place,

but also with the one who is contrite and lowly in spirit,

to revive the spirit of the lowly

and to revive the heart of the contrite.

16I will not accuse them forever,

nor will I always be angry,

for then they would faint away because of me—

the very people I have created.

17I was enraged by their sinful greed;

I punished them, and hid my face in anger,

yet they kept on in their willful ways.

18I have seen their ways, but I will heal them;

I will guide them and restore comfort to Israel’s mourners,

19creating praise on their lips.

Peace, peace, to those far and near,”

says the Lord. “And I will heal them.”

20But the wicked are like the tossing sea,

which cannot rest,

whose waves cast up mire and mud.

21“There is no peace,” says my God, “for the wicked.”