Isaya 55 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 55:1-13

Mwaliko Kwa Wenye Kiu

155:1 Mao 5:4; Mit 9:5; Ufu 3:18; Yer 2:31; Isa 35:7; Mt 5:6; Lk 5:21; Yn 4:14; Zek 14:8; Hos 14:4; Eze 47:1, 12“Njooni, ninyi nyote wenye kiu,

njooni kwenye maji;

nanyi ambao hamna fedha,

njooni, nunueni na mle!

Njooni, nunueni divai na maziwa

bila fedha na bila gharama.

255:2 Yer 12:13; Hag 1:6; Za 22:26; Mhu 6:2; Isa 49:4; Hos 4:10; 8:7Kwa nini kutumia fedha kwa kitu ambacho si chakula,

na kutaabikia kitu kisichoshibisha?

Sikilizeni, nisikilizeni mimi na mle kilicho kizuri,

nazo nafsi zenu zitafurahia utajiri wa unono.

355:3 Law 18:5; Yn 6:27; Mwa 9:16; Ebr 13:20; Mdo 13:34; Rum 10:5; Isa 54:10Tegeni sikio mje kwangu,

nisikieni mimi, ili nafsi zenu zipate kuishi.

Nitafanya agano la milele nanyi,

pendo la uaminifu nililomwahidi Daudi.

455:4 1Tim 6:13; 1Sam 13:14; Eze 34:23-24; Ebr 2:10; 2Nya 7:18Tazama, nimemfanya kuwa shahidi wa mataifa,

kiongozi na jemadari wa mataifa.

5Hakika utaita mataifa usiyoyajua,

nayo mataifa yale yasiyokujua yataharakisha kukujia,

kwa sababu ya Bwana Mungu wako,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,

kwa maana amekutukuza.”

655:6 Mdo 17:27; Za 32:6; Amo 5:14; Yer 33:3; Isa 9:13; Kum 4:29; 2Nya 15:2Mtafuteni Bwana maadamu anapatikana;

mwiteni maadamu yu karibu.

755:7 Yer 3:12; 26:3; Isa 32:7; Eze 18:32; 2Nya 6:21; 30:6; Eze 18:27-28Mtu mwovu na aiache njia yake,

na mtu mbaya na ayaache mawazo yake.

Yeye na amrudie Bwana, naye atamrehemu,

arudi kwa Mungu wetu, kwa kuwa atamsamehe bure kabisa.

855:8 Isa 53:6; Mik 4:12; Flp 2:5; 4:8“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu,

wala njia zenu si njia zangu,”

asema Bwana.

955:9 Ay 11:8; Za 103:11; Hes 23:19; Isa 40:13-14“Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia,

ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu

na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.

1055:10 2Kor 9:10; Isa 30:23; Mwa 47:23; Za 67:6; Ay 14:9; Law 25:19Kama vile mvua na theluji

ishukavyo kutoka mbinguni,

nayo hairudi tena huko

bila kunywesha dunia

na kuichipusha na kuistawisha,

hivyo hutoa mbegu kwa mpanzi

na mkate kwa mlaji,

1155:11 Isa 54:10-13; 1Nya 16:33; Za 98:4; Isa 35:2; Za 65:12-13; 96:12-13; 98:8ndivyo lilivyo neno langu lile litokalo kinywani mwangu:

Halitanirudia tupu,

bali litatimiliza lile nililokusudia

na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma.

12Mtatoka nje kwa furaha

na kuongozwa kwa amani;

milima na vilima

vitapaza sauti kwa nyimbo mbele yenu,

nayo miti yote ya shambani

itapiga makofi.

1355:13 Hes 33:55; Za 102:12; Yer 32:20; Isa 5:6; 41:19; 63:12; Yer 33:9Badala ya kichaka cha miiba

itaota miti ya misunobari,

na badala ya michongoma

utaota mhadasi.55:13 Mhadasi ni aina ya mti ambao huota milimani karibu na Yerusalemu, hutoa harufu nzuri itumikayo kutengeneza manukato; kwa Kiebrania ni “hadas”, na ilikuwa inatumika kujenga vibanda wakati wa Sikukuu ya Vibanda (ona pia Neh 8:15).

Hili litakuwa jambo la kumpatia Bwana jina,

kwa ajili ya ishara ya milele,

ambayo haitaharibiwa.”