Isaya 54 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 54:1-17

Utukufu Wa Baadaye Wa Sayuni

154:1 Isa 49:20; Gal 4:27; Mwa 21:6; Za 98:4; Isa 66:7; 49:20“Imba, ewe mwanamke tasa,

wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto;

paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha,

wewe ambaye kamwe hukupata utungu;

kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi

kuliko wa mwanamke mwenye mume,”

asema Bwana.

254:2 Mwa 26:22; Isa 26:15; Kut 35:18; 39:40; Isa 49:19-20“Panua mahali pa hema lako,

tandaza mapazia ya hema lako uyaeneze mbali,

wala usiyazuie;

ongeza urefu wa kamba zako,

imarisha vigingi vyako.

354:3 Mwa 13:14; Isa 48:19; Ay 12:23; Isa 14:2; 60:4-11; 49:19Kwa maana utaenea upande wa kuume

na upande wa kushoto;

wazao wako watayamiliki mataifa

na kukaa katika miji yao iliyoachwa ukiwa.

454:4 Isa 30:10; Yoe 2:21; Isa 28:16; Mwa 30:23; Za 25:7; 119:39; Yer 22:21; Isa 47:8“Usiogope, wewe hutaaibika.

Usiogope aibu, wewe hutaaibishwa.

Wewe utasahau aibu ya ujana wako,

wala hutakumbuka tena mashutumu ya ujane wako.

554:5 Wim 3:3; Isa 41:14; 48:17; Rum 3:29; Hos 2:7-16; Za 149:2; Isa 51:13Kwa maana Muumba wako ndiye mume wako,

Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ni Mkombozi wako,

yeye anaitwa Mungu wa dunia yote.

654:6 Isa 49:14-21; 60:15; 62:4; Yer 44:2; Hos 1:10; Kut 20:14; Mal 2:14Bwana atakuita urudi

kana kwamba ulikuwa mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni;

kama mke aliyeolewa bado angali kijana

na kukataliwa,” asema Mungu wako.

754:7 Ay 14:13; Isa 26:20; 2Kor 4:17; Isa 27:8; Za 71:11; Isa 49:18“Kwa kitambo kidogo nilikuacha,

lakini kwa huruma nyingi nitakurudisha.

854:8 Isa 9:12; Yer 31:3; Za 92:2; Isa 26:20; Za 25:6; Isa 55:3; 63:7; Hos 2:19Katika ukali wa hasira

nilikuficha uso wangu kwa kitambo,

lakini kwa fadhili za milele

nitakuwa na huruma juu yako,”

asema Bwana Mkombozi wako.

954:9 Mwa 8:21; Mik 7:18; Eze 39:29; Isa 14:24; Kum 28:20; Isa 49:18“Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Noa,

nilipoapa kuwa maji ya Noa kamwe hayatafunika tena dunia.

Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi,

kamwe sitawakemea tena.

1054:10 Za 46:2; Ebr 12:27; Mwa 9:16; Kut 34:10; Ufu 6:14; Hes 25:12; Isa 55:7Ijapotikisika milima, na vilima viondolewe,

hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika,

wala agano langu la amani halitaondolewa,”

asema Bwana, mwenye huruma juu yenu.

1154:11 Isa 14:32; 29:6; 1Nya 29:2; Ufu 21:18; 21:19-20; Isa 26:18; 28:16; Kut 24:10“Ewe mji uliyeteswa, uliyepigwa kwa dhoruba na usiyetulizwa,

nitakujenga kwa almasi, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi.

1254:12 Ufu 21:21Nitafanya minara yako ya akiki,

malango yako kwa vito vingʼaavyo,

nazo kuta zako zote za vito vya thamani.

1354:13 Mik 4:2; Ebr 8:11; Law 26:6; Isa 11:9; 28:9; 48:18; Yn 6:45Watoto wako wote watafundishwa na Bwana,

nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu.

1454:14 2Sam 7:10; Isa 9:4; 17:14; 26:2; Yer 30:20; Sef 3:17; Zek 9:8Kwa haki utathibitika:

Kuonewa kutakuwa mbali nawe;

hutaogopa chochote.

Hofu itakuwa mbali nawe;

haitakukaribia wewe.

1554:15 Isa 41:11-16Kama mtu yeyote akikushambulia,

haitakuwa kwa ruhusa yangu;

yeyote akushambuliaye

atajisalimisha kwako.

1654:16 Isa 44:12; 10:5; 13:5“Tazama, ni mimi niliyemuumba mhunzi,

yeye afukutaye makaa kuwa moto,

na kutengeneza silaha inayofaa kwa kazi yake.

Tena ni mimi niliyemwambia mharabu

kufanya uharibifu mwingi.

1754:17 Isa 29:8; Mdo 6:10; Isa 45:24-25; 41:11; 56:6-8; Zek 1:20-21; Isa 65:8-9Hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako

itakayofanikiwa,

nawe utauthibitisha kuwa mwongo

kila ulimi utakaokushtaki.

Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana

na hii ndiyo haki yao itokayo kwangu,”

asema Bwana.