Isaya 53 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 53:1-12

153:1 Isa 28:9; Yn 12:38; Rum 10:16; Za 98:1; Isa 30:30Ni nani aliyeamini ujumbe wetu,

na mkono wa Bwana umefunuliwa kwa nani?

253:2 Mk 9:12; Isa 52:14; 2Fal 19:26; Ay 14:7; Isa 4:2; 11:10Alikua mbele yake kama mche mwororo

na kama mzizi katika nchi kavu.

Hakuwa na uzuri wala utukufu wa kutuvutia kwake,

hakuwa na chochote katika sura yake cha kutufanya tumtamani.

353:3 Ebr 4:15; Mt 16:21; 27:29; 1Sam 2:30; Za 69:29; Kut 1:10; Lk 18:31-33Alidharauliwa na kukataliwa na wanadamu,

mtu wa huzuni nyingi, ajuaye mateso.

Kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,

alidharauliwa, wala hatukumhesabu kuwa kitu.

453:4 Mt 8:17; Zek 13:7; Yn 19:7; Kum 5:24; Ay 4:5; Yer 23:5-6; Eze 34:23-24; Mik 5:2Hakika alichukua udhaifu wetu

na akajitwika huzuni zetu,

hata hivyo tulidhania kuwa amepigwa na Mungu,

akapigwa sana naye, na kuteswa.

553:5 Kum 32:39; Yn 3:17; 1Pet 2:24-25; 2Nya 7:14; Rum 4:25; 1Kor 15:3; Ebr 9:8; Kut 28:38Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu,

alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu;

adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake,

na kwa majeraha yake sisi tumepona.

653:6 Za 119:176; 1Pet 2:25Sisi sote, kama kondoo, tumepotea,

kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe,

naye Bwana aliweka juu yake

maovu yetu sisi sote.

753:7 Mdo 8:32; Mk 14:61; 1Pet 2:23; Isa 49:26; Mt 27:31; Yn 1:29; Za 44:22Alionewa na kuteswa,

hata hivyo hakufungua kinywa chake;

aliongozwa kama mwana-kondoo

apelekwaye machinjoni,

kama vile kondoo anyamazavyo mbele ya wao wamkataye manyoya,

hivyo hakufungua kinywa chake.

853:8 Za 88:5; Dan 9:26; Mdo 8:32-33; Za 39:8; Mk 14:49Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa.

Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake?

Kwa maana alikatiliwa mbali na nchi ya walio hai,

alipigwa kwa ajili ya makosa ya watu wangu.

953:9 Mk 15:43-46; Lk 23:50-53; Isa 42:1-3; Ay 16:17; Ufu 14:5; Yn 19:19, 38-41Wakamfanyia kaburi pamoja na waovu,

pamoja na matajiri katika kifo chake,

ingawa hakutenda jeuri,

wala hapakuwa na hila kinywani mwake.

1053:10 2Kor 5:21; Mwa 12:17; Za 22:30; Mdo 2:23; Isa 46:10; Law 5:15; Yn 3:17Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Bwana

kumchubua na kumsababisha ateseke.

Ingawa Bwana amefanya maisha yake

kuwa sadaka ya hatia,

ataona uzao wake na kuishi siku nyingi,

nayo mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake.

1153:11 Yn 10:14-18; Rum 5:18-19; Ay 33:30; Isa 20:3; Mdo 7:52; Yn 1:29; Rum 4:24; Mdo 10:43Baada ya maumivu ya nafsi yake,

ataona nuru ya uzima na kuridhika;

kwa maarifa yake, mtumishi wangu mwenye haki

atawafanya wengi kuwa wenye haki,

naye atayachukua maovu yao.

1253:12 Flp 2:9; Mt 26:28, 38; 27:38; Lk 23:34; Kut 15:9; Za 119:162; Ebr 9:28; Isa 59:19; Rum 8:34; Mk 15:27; Lk 22:37Kwa hiyo nitamgawia sehemu miongoni mwa wakuu,

naye atagawana nyara pamoja na wenye nguvu,

kwa sababu aliyamimina maisha yake hadi mauti,

naye alihesabiwa pamoja na wakosaji.

Kwa kuwa alichukua dhambi za wengi,

na kuwaombea wakosaji.