Isaya 52 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 52:1-15

152:1 Isa 51:9; Es 6:8; Ufu 21:2; Yoe 3:17; Zek 3:4; Isa 49:18; Kut 28:2, 40; Neh 1:1Amka, amka, ee Sayuni,

jivike nguvu.

Vaa mavazi yako ya fahari,

ee Yerusalemu, mji mtakatifu.

Asiyetahiriwa na aliye najisi

hataingia kwako tena.

252:2 Zek 2:7; Isa 29:4; 10:27; Za 81:9; 9:14Jikungʼute mavumbi yako,

inuka, uketi kwenye kiti cha enzi, ee Yerusalemu.

Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako,

ee Binti Sayuni uliye mateka.

352:3 Za 44:12; Isa 45:13; 1:27; 1Pet 1:18Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana:

“Mliuzwa pasipo malipo,

nanyi mtakombolewa bila fedha.”

452:4 Mwa 46:6; Isa 10:24Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:

“Hapo kwanza watu wangu walishuka Misri kuishi,

hatimaye, Ashuru wakawaonea.

552:5 Eze 36:20; Rum 2:24; Isa 37:23“Basi sasa nina nini hapa?” asema Bwana.

“Kwa kuwa watu wangu wamechukuliwa pasipo malipo,

nao wale wanaowatawala wanawadhihaki,”

asema Bwana.

“Mchana kutwa

jina langu limetukanwa bila kikomo.

652:6 Isa 49:23; Kut 6:3; Isa 41:26; 10:20Kwa hiyo watu wangu watalijua Jina langu;

kwa hiyo katika siku ile watajua

kwamba ndimi niliyetangulia kulisema.

Naam, ni mimi.”

752:7 2Sam 18:26; Rum 10:15; 1Kor 15:24-25; Lk 2:14; Isa 42:11; 40:9; Efe 6:15Tazama jinsi miguu ya wale waletao habari njema

ilivyo mizuri juu ya milima,

wale wanaotangaza amani,

wanaoleta habari njema,

wanaotangaza wokovu,

wauambiao Sayuni,

“Mungu wako anatawala!”

852:8 Sef 3:9; Eze 3:17; 1Sam 14:16; Isa 56:10; Yer 6:17; Hes 10:36; Zek 8:3Sikiliza! Walinzi wako wanapaza sauti zao,

pamoja wanapaza sauti zao kwa furaha.

Wakati Bwana atakaporejea Sayuni,

wataliona kwa macho yao wenyewe.

952:9 Za 98:4; Isa 35:2; Za 74:3; Isa 48:20; Ezr 9:9; Lk 2:25; Isa 51:3Pazeni sauti ya nyimbo za furaha pamoja,

enyi magofu ya Yerusalemu,

kwa maana Bwana amewafariji watu wake,

ameikomboa Yerusalemu.

1052:10 Lk 2:30; Za 67:2; Isa 66:18; 2Nya 32:8; Za 44:3; Isa 30:30; Yos 4:24Mkono mtakatifu wa Bwana umefunuliwa

machoni pa mataifa yote,

nayo miisho yote ya dunia itaona

wokovu wa Mungu wetu.

1152:11 Yer 50:8; 2Kor 6:17; Hes 8:6; 2Tim 2:9; Isa 1:16; 2Nya 36:10; Isa 48:20Ondokeni, ondokeni, tokeni huko!

Msiguse kitu chochote kilicho najisi!

Tokeni kati yake mwe safi,

ninyi mchukuao vyombo vya Bwana.

1252:12 Kut 14:19; 12:11; Mik 2:13; Yn 10:4Lakini hamtaondoka kwa haraka,

wala hamtakwenda kwa kukimbia;

kwa maana Bwana atatangulia mbele yenu,

Mungu wa Israeli atakuwa mlinzi nyuma yenu.

Mateso Na Utukufu Wa Mtumishi

1352:13 Isa 53:3; Mdo 3:13; Yos 1:8; Isa 20:3; 57:15; Flp 2:9Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa hekima;

atatukuzwa, na kuinuliwa juu, na kukwezwa sana.

1452:14 Law 26:32; Ay 2:12; 16:16; 18:20; 2Sam 10:4Kama walivyokuwa wengi

walioshangazwa naye,

kwani uso wake ulikuwa umeharibiwa sana

zaidi ya mtu yeyote

na umbo lake kuharibiwa

zaidi ya mfano wa mwanadamu:

1552:15 Ebr 9:13; Rum 15:21; Efe 3:4-5; Za 107:42; Amu 18:19; Law 14:7; 16:14-15hivyo atayashangaza mataifa mengi,

nao wafalme watafunga vinywa vyao kwa sababu yake.

Kwa kuwa yale ambayo hawakuambiwa, watayaona,

nayo yale wasiyoyasikia, watayafahamu.