Isaya 51 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 51:1-23

Wokovu Wa Milele Kwa Sayuni

151:1 Isa 46:3; Kum 7:13; Mit 26:27; Kum 16:20; Za 94:15; Isa 63:8; Rum 9:30-31; Isa 17:10“Nisikilizeni, ninyi mnaofuatia haki

na mnaomtafuta Bwana:

Tazameni mwamba ambako mlichongwa,

na mahali pa kuvunjia mawe ambako mlichimbwa;

251:2 Mwa 17:6; Ebr 11:11; Mwa 12:2; Isa 29:22; Rum 4:16mwangalieni Abrahamu, baba yenu,

na Sara, ambaye aliwazaa.

Wakati nilipomwita alikuwa mmoja tu,

nami nikambariki na kumfanya kuwa wengi.

351:3 Isa 40:1; Mwa 13:10; Yer 16:9; Za 102:13; Isa 44:26; Za 51:18; Isa 61:4Hakika Bwana ataifariji Sayuni,

naye atayaangalia kwa huruma magofu yake yote;

atayafanya majangwa yake yawe kama Edeni,

nazo sehemu zake zisizolimika ziwe kama bustani ya Bwana.

Shangwe na furaha zitakuwako ndani yake,

shukrani na sauti za kuimba.

451:4 Kut 6:7; Isa 26:18; 42:4-6; Za 50:7; Isa 3:15; 63:8“Nisikilizeni, watu wangu;

nisikieni, taifa langu:

Sheria itatoka kwangu;

haki yangu itakuwa nuru kwa mataifa.

551:5 Isa 35:4; 46:13; Za 98:1; 85:9; Mwa 49:10; Isa 52:10Haki yangu inakaribia mbio,

wokovu wangu unakuja,

nao mkono wangu utaleta hukumu kwa mataifa.

Visiwa vitanitegemea

na kungojea mkono wangu kwa matumaini.

651:6 Za 37:20; Lk 21:33; Za 102:25-26; Ebr 1:10-12; Mt 24:35; Isa 54:10Inueni macho yenu mbinguni,

mkaitazame dunia chini;

mbingu zitatoweka kama moshi,

dunia itachakaa kama vazi,

na wakazi wake kufa kama mainzi.

Bali wokovu wangu utadumu milele,

haki yangu haitakoma kamwe.

751:7 Za 37:31; Mt 10:28; Mdo 5:41; Za 119:39; Lk 6:22; Isa 54:4; 50:7“Nisikieni, ninyi mnaojua lililo sawa,

ninyi watu ambao mna sheria yangu mioyoni mwenu:

Msiogope mashutumu ya wanadamu

wala msitiwe hofu na matukano yao.

851:8 Ay 13:28; Yak 5:2; Isa 14:11Kwa maana nondo atawala kama vazi,

nao funza atawatafuna kama sufu.

Lakini haki yangu itadumu milele,

wokovu wangu kwa vizazi vyote.”

951:9 Kut 32:7; Za 68:30; Ay 26:12; Eze 29:3; Amu 5:12; Mwa 18:14; Za 65:6; 74:13Amka, Amka! Jivike nguvu,

ewe mkono wa Bwana,

Amka, kama siku zilizopita,

kama vile vizazi vya zamani.

Si ni wewe uliyemkata Rahabu vipande vipande,

uliyemchoma yule joka?

1051:10 Zek 10:11; Kut 14:21; Ufu 16:12; Kut 15:5, 8, 13; Ay 36:30Si ni wewe uliyekausha bahari,

maji ya kilindi kikuu,

uliyefanya barabara katika vilindi vya bahari

ili waliokombolewa wapate kuvuka?

1151:11 Isa 35:9; 44:23; 48:20; Ufu 7:17; Yer 31:13; 30:19; Sef 3:17; Isa 30:19Wale waliolipiwa fidia na Bwana watarudi.

Wataingia Sayuni wakiimba;

furaha ya milele itakuwa taji juu ya vichwa vyao.

Furaha na shangwe zitawapata,

huzuni na kulia kwa uchungu kutatoweka.

1251:12 Za 118:6; 2Kor 1:3-4; 1Pet 1:24; Isa 15:6; 2Fal 1:15; Isa 2:22; 40:6-7“Mimi, naam mimi,

ndimi niwafarijie ninyi.

Ninyi ni nani hata kuwaogopa

wanadamu wanaokufa,

wanadamu ambao ni majani tu,

1351:13 Ay 8:13; 4:17; Isa 17:10; 7:4; Ay 20:7; Isa 45:11; 48:13; 9:4kwamba mnamsahau Bwana Muumba wenu,

aliyezitanda mbingu

na kuiweka misingi ya dunia,

kwamba mnaishi katika hofu siku zote

kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu,

ambaye nia yake ni kuangamiza?

Iko wapi basi ghadhabu ya mdhalimu?

1451:14 Isa 49:10; Zek 9:11; Isa 42:7Wafungwa waliojikunyata kwa hofu

watawekwa huru karibuni;

hawatafia kwenye gereza lao,

wala hawatakosa chakula.

1551:15 Kut 14:21; Isa 43:16; Za 74:13; Yer 31:35; Za 93:3; Isa 13:4Kwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,

ambaye huisukasuka bahari ili mawimbi yake yangurume:

Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.

1651:16 Kut 4:12-15; 2Pet 3:13; Kum 18:18; 33:22; Zek 8:8; Eze 14:11; Yer 7:23; 24:7Nimeweka maneno yangu kinywani mwako

na kukufunika kwa uvuli wa mkono wangu:

Mimi niliyeweka mbingu mahali pake,

niliyeweka misingi ya dunia,

niwaambiaye Sayuni,

‘Ninyi ni watu wangu.’ ”

Kikombe Cha Ghadhabu Ya Bwana

1751:17 Amu 5:12; Ay 21:20; Ufu 16:19; Za 60:3; 16:5; Mt 20:22; Isa 42:25Amka, amka!

Simama, ee Yerusalemu,

wewe uliyekunywa kutoka mkono wa Bwana

kikombe cha ghadhabu yake,

wewe uliyekunywa mpaka kufikia machujo yake,

kikombe kile cha kunywea

kiwafanyacho watu kuyumbayumba.

1851:18 Ay 31:18; Za 88:18; Isa 49:21; 41:13Kati ya wana wote aliowazaa

hakuwepo hata mmoja wa kumwongoza,

kati ya wana wote aliowalea

hakuwepo hata mmoja wa kumshika mkono.

1951:19 Isa 40:2; 47:9; 49:13; Yer 14:12; 24:10Majanga haya mawili yamekuja juu yako:

ni nani awezaye kukufariji?

Maangamizi, uharibifu, njaa na upanga:

ni nani awezaye kukutuliza?

2051:20 Yer 14:16; Mao 2:19; Isa 5:25; Ay 18:10; Yer 44:6; Ay 40:11; Kum 28:20Wana wako wamezimia,

wamelala kwenye mwanzo wa kila barabara,

kama swala aliyenaswa kwenye wavu.

Wamejazwa na ghadhabu ya Bwana

na makaripio ya Mungu wako.

2151:21 Isa 14:32; 29:9; Mao 3:15Kwa hiyo sikiliza hili, wewe uliyeteswa,

uliyelewa, lakini si kwa mvinyo.

2251:22 Yer 50:34; Hab 2:16; Isa 49:25; Yer 25:15; Mt 20:2251:22 Yer 50:34; Hab 2:16; Isa 49:25; Yer 25:15; Mt 20:22Hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi wako,

Mungu wako, yeye ambaye huwatetea watu wake:

“Tazama, nimeondoa mkononi mwako

kikombe kilichokufanya uyumbayumbe;

kutoka kikombe hicho,

kikombe cha kunywa cha ghadhabu yangu,

kamwe hutakunywa tena.

2351:23 Yer 49:12; Zek 12:3; Yos 10:24; Isa 14:4; 49:26; Yer 25:15-17, 26; Mik 7:1051:23 Yer 49:12; Zek 12:3; Yos 10:24; Isa 14:4; 49:26; Yer 25:15-17, 26; Mik 7:10Nitakiweka mikononi mwa watesi wako,

wale waliokuambia,

‘Anguka kifudifudi

ili tuweze kutembea juu yako.’

Ukaufanya mgongo wako kama ardhi,

kama njia yao ya kupita.”