Isaya 49 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 49:1-26

Mtumishi Wa Bwana

149:1 Isa 44:24; Yer 1:5; Lk 1:15; Isa 33:13; 11:11; Mt 1:20; Isa 7:14; 9:6; Kut 33:12Nisikilizeni, enyi visiwa, sikieni hili,

ninyi mataifa mlio mbali:

Kabla sijazaliwa, Bwana aliniita,

tangu kuzaliwa kwangu, amelitaja jina langu.

249:2 Za 64:3; Hos 6:5; Efe 6:17; Ay 40:18; Ufu 1:16; Kut 33:22; Zek 9:13Akafanya kinywa changu kuwa kama upanga ulionolewa,

katika uvuli wa mkono wake akanificha;

akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa,

na kunificha katika podo lake.

349:3 Isa 20:3; Zek 3:8; Law 10:3; Isa 44:23Akaniambia, “Wewe u mtumishi wangu,

Israeli, ambaye katika yeye

nitaonyesha utukufu wangu.”

449:4 Eze 3:19; Law 26:20; Isa 35:4; Ay 27:2; Isa 55:2; 65:23; 45:25; 54:17Lakini nilisema, “Nimetumika bure,

nimetumia nguvu zangu bure bila faida.

Hata hivyo linalonistahili liko mkononi mwa Bwana,

nao ujira wangu uko kwa Mungu wangu.”

549:5 Kum 30:4; Isa 11:12; 43:4; Za 139:13; Gal 1:15; Za 18:1Sasa Bwana asema:

yeye aliyeniumba tumboni kuwa mtumishi wake,

kumrudisha tena Yakobo kwake

na kumkusanyia Israeli,

kwa maana nimepata heshima machoni pa Bwana,

naye Mungu wangu amekuwa nguvu yangu;

649:6 Zek 8:22; Lk 2:32; Yn 11:52; Isa 9:2; Yon 1:9; Isa 26:18; Kum 30:4; Mdo 13:47yeye asema:

“Je, ni jambo dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu

ili kurejeza makabila ya Yakobo,

na kuwarudisha wale Waisraeli niliowahifadhi?

Pia nitakufanya uwe nuru kwa ajili ya watu wa Mataifa,

ili upate kuleta wokovu wangu hata miisho ya dunia.”

749:7 Isa 48:17; Za 69:7-9; Isa 52:15; Mwa 27:29; Za 22:6, 29; 86:9; Kum 7:9Hili ndilo asemalo Bwana,

yeye Mkombozi na Aliye Mtakatifu wa Israeli,

kwake yeye aliyedharauliwa na kuchukiwa na taifa,

kwa mtumishi wa watawala:

“Wafalme watakuona na kusimama,

wakuu wataona na kuanguka kifudifudi,

kwa sababu ya Bwana, aliye mwaminifu,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, aliyekuchagua wewe.”

Kurejezwa Kwa Israeli

849:8 Za 69:13; 2Kor 6:2; Law 25:10; Za 37:9; Isa 60:10; 41:10; 26:3; 5:249:8 Isa 44:28; Neh 2:17Hili ndilo asemalo Bwana:

“Wakati wangu uliokubalika nitakujibu,

nami katika siku ya wokovu nitakusaidia;

nitakuhifadhi, nami nitakufanya

kuwa agano kwa ajili ya watu,

ili kurudisha nchi

na kugawanyia urithi tena wale waliokuwa ukiwa,

949:9 Lk 4:19; Isa 41:18; Zek 9:12; Isa 42:7; Za 107:10kuwaambia mateka, ‘Tokeni nje,’

nao wale walio gizani, ‘Kuweni huru!’

“Watajilisha kando ya barabara

na kupata malisho yao juu ya kila kilima kilicho kitupu.

1049:10 Isa 33:16; Ufu 7:16; Isa 35:7; Za 21:6; Isa 42:16; 33:21Hawataona njaa wala kuona kiu,

wala hari ya jangwani au jua halitawapiga.

Yeye mwenye huruma juu yao atawaonyesha njia,

na kuwaongoza kando ya chemchemi za maji.

1149:11 Isa 11:6; Yer 31:9; Isa 40:4Nitaifanya milima yangu yote kuwa barabara,

na njia kuu zangu zitainuliwa.

1249:12 Isa 2:3; 43:5-6; 59:19; Mt 8:11Tazama, watakuja kutoka mbali:

wengine kutoka kaskazini, wengine kutoka magharibi,

wengine kutoka nchi ya Sinimu.”49:12 Sinimu hapa ina maana ya Aswani.

1349:13 Za 98:4; 71:21; 2Kor 1:4; Isa 48:20; Za 96:11; 65:12-13; 9:12Pigeni kelele kwa furaha, enyi mbingu;

furahi, ee dunia;

pazeni sauti kwa kuimba, enyi milima!

Kwa maana Bwana anawafariji watu wake,

naye atakuwa na huruma kwa watu wake walioumizwa.

1449:14 Isa 40:9; Za 9:10; Isa 27:8; Za 71:11Lakini Sayuni alisema, “Bwana ameniacha,

Bwana amenisahau.”

1549:15 Mt 7:11; Isa 44:21; 1Fal 3:26; Isa 66:13“Je, mama aweza kumsahau mtoto

aliyeko matitini mwake akinyonya,

wala asiwe na huruma

juu ya mtoto aliyemzaa?

Ingawa anaweza kusahau,

mimi sitakusahau wewe!

1649:16 Wim 8:6; Kut 28:9; Za 48:12-13; Isa 62:6; Mwa 38:18Tazama, nimekuchora kama muhuri

katika vitanga vya mikono yangu,

kuta zako zi mbele yangu daima.

1749:17 Isa 49:19Wana wako wanaharakisha kurudi,

nao wale waliokuteka wanaondoka kwako.

1849:18 Mit 17:6; Rum 14:11; Hes 14:21; Yer 2:32; Isa 11:12; 43:5; 54:9; 45:23Inua macho yako ukatazame pande zote:

wana wako wote wanakusanyika na kukujia.

Kwa hakika kama vile niishivyo,

utawavaa wote kama mapambo,

na kujifunga nao kama bibi arusi,”

asema Bwana.

1949:19 Law 26:33; Isa 62:4; Zek 10:10; Eze 36:10-11; Zek 2:4; Isa 60:18; 1:20“Ingawa uliangamizwa na kufanywa ukiwa,

na nchi yako ikaharibiwa,

sasa nafasi itakuwa finyu kwa ajili ya watu wako,

nao wale waliokuangamiza watakuwa mbali sana.

2049:20 Mt 3:9; Rum 11:11, 12Watoto waliozaliwa wakati wa msiba wako

bado watakuambia,

‘Mahali hapa ni finyu sana kwetu,

tupe eneo kubwa zaidi la kuishi.’

2149:21 Isa 5:13; Lk 15:5; Isa 60:4; 29:23; 66:7-8; 47:8; Yer 10:20; Mwa 15:2Ndipo utasema moyoni mwako,

‘Ni nani aliyenizalia hawa?

Nilikuwa nimefiwa, tena tasa;

nilikuwa nimehamishwa na kukataliwa.

Ni nani aliyewalea hawa?

Niliachwa peke yangu,

lakini hawa wametoka wapi?’ ”

2249:22 Isa 60:10-11; Hes 11:12; Mwa 3:14; Za 72:9; Kut 6:2; Mik 7:17; Mwa 3:14Hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:

“Tazama, nitawaashiria watu wa Mataifa,

nitainua bendera yangu kwa mataifa;

watawaleta wana wako mikononi yao,

na kuwabeba binti zenu juu ya mabega yao.

23Wafalme watakuwa baba zenu wa kuwalea,

na malkia wao watakuwa mama zenu wa kuwalea.

Watasujudu mbele yako nyuso zao zikigusa ardhi;

wataramba mavumbi yaliyo miguuni mwako.

Ndipo utajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana;

wale wanaonitumaini mimi hawataaibika.”

2449:24 Mt 12:29; Mk 3:27; Lk 11:21Je, nyara zaweza kuchukuliwa kutoka kwa mashujaa wa vita,

au mateka kuokolewa kutoka kwa watu wakali?

2549:25 Yer 50:33-34; Isa 14:2; 25:9; Mk 3:27; Isa 13:11; 25:4-9; 1Sam 24:15Lakini hili ndilo asemalo Bwana:

“Naam, mateka watachukuliwa kutoka kwa mashujaa,

na nyara zitapokonywa kutoka kwa watu wakali.

Nitashindana na wale wanaoshindana nawe,

nami nitawaokoa watoto wako.

2649:26 Isa 9:4, 20; Nah 1:10; Ufu 16:6; Eze 39:7; Hes 23:24; Yer 25:27; Isa 11:9; Ay 19:25; Isa 48:17; Mwa 49:24; Za 132:2Nitawafanya wale wanaokuonea kula nyama yao wenyewe,

watalewa kwa damu yao wenyewe,

kama vile kwa mvinyo.

Ndipo wanadamu wote watajua

ya kuwa Mimi, Bwana, ni Mwokozi wako,

Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.”