Isaya 48 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 48:1-22

Israeli Mkaidi

148:1 Kum 6:13; Kut 23:13; Dan 8:12; Zek 8:3; Mwa 17:5; 29:35; Isa 19:18“Sikilizeni hili, ee nyumba ya Yakobo,

ninyi mnaoitwa kwa jina la Israeli,

na mnaotoka katika ukoo wa Yuda,

ninyi mnaoapa kwa jina la Bwana,

mnaomwomba Mungu wa Israeli,

lakini si katika kweli au kwa haki;

248:2 Neh 11:1; Rum 2:17; Mik 3:11; Isa 1:26; Mt 4:5; Isa 10:20; 47:4ninyi mnaojiita raiya wa mji mtakatifu,

na kumtegemea Mungu wa Israeli,

Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake:

348:3 Isa 40:21; 45:21; Yos 21:45; Isa 41:22; 17:14; 30:13Nilitoa unabii mambo ya kwanza tangu zamani,

kinywa changu kiliyatangaza na kuyafanya yajulikane;

kisha ghafula nikayatenda, nayo yakatokea.

448:4 Kum 9:27; 31:27; Mdo 5:21; Isa 9:9; Kut 32:9; Eze 3:9; Mdo 7:51Kwa kuwa nalijua jinsi ulivyokuwa mkaidi;

mishipa ya shingo yako ilikuwa chuma,

kipaji chako cha uso kilikuwa shaba.

548:5 Yer 44:15-18; Isa 42:9; 40:21Kwa hiyo nilikuambia mambo haya tangu zamani,

kabla hayajatokea nilikutangazia

ili usije ukasema,

‘Sanamu zangu zilifanya hayo;

kinyago changu cha mti na mungu wangu wa chuma aliyaamuru.’

648:6 Isa 41:22; Rum 16:25Umesikia mambo haya; yaangalie hayo yote.

Je, hutayakubali?

“Kuanzia sasa na kuendelea nitakueleza mambo mapya,

juu ya mambo yaliyofichika usiyoyajua.

748:7 Isa 65:18; 45:21; Kut 6:7Yameumbwa sasa, wala si tangu zamani;

hukupata kuyasikia kabla ya siku ya leo.

Hivyo huwezi kusema,

‘Naam, niliyajua hayo.’

848:8 Za 58:3; Kum 9:24; Isa 41:24; Mal 2:11-14; Isa 43:27Hujayasikia wala kuyaelewa,

tangu zamani sikio lako halikufunguka.

Ninafahamu vyema jinsi ulivyo mdanganyifu,

uliitwa mwasi tangu kuzaliwa kwako.

948:9 Yos 7:9; Ay 9:13; Za 78:38; 1Sam 12:22; Isa 37:35; 30:18Kwa ajili ya Jina langu mwenyewe

ninaichelewesha ghadhabu yangu,

kwa ajili ya sifa zangu nimeizuia isikupate,

ili nisije nikakukatilia mbali.

1048:10 Za 66:10Tazama, nimekusafisha, ingawa si kama fedha,

nimekujaribu katika tanuru ya mateso.

1148:11 1Sam 12:22; Law 18:21; Isa 42:8; Kum 32:26-27; Eze 20:9; Yer 14:7, 21Kwa ajili yangu mwenyewe,

kwa ajili yangu mwenyewe, nafanya hili.

Jinsi gani niliache Jina langu lichafuliwe?

Sitautoa utukufu wangu kwa mwingine.

Israeli Anawekwa Huru

1248:12 Isa 46:3; 41:4; Ufu 22:13; Isa 43:13; 42:6“Ee Yakobo, nisikilize mimi,

Israeli, ambaye nimekuita:

Mimi ndiye;

mimi ndimi mwanzo na mwisho.

1348:13 Ebr 1:10-12; Ay 9:8; Isa 34:16; 40:26; Kut 20:11; Isa 45:18Mkono wangu mwenyewe uliweka misingi ya dunia,

nao mkono wangu wa kuume umezitanda mbingu;

niziitapo, zote husimama pamoja.

1448:14 Isa 43:9; 46:10-11; 41:2, 22; Yer 50:45; Isa 21:9“Kusanyikeni, ninyi nyote, msikilize:

Ni ipi miongoni mwa hizo sanamu

ambayo imetabiri vitu hivi?

Watu wa Bwana waliochaguliwa na kuungana

watatimiza kusudi lake dhidi ya Babeli;

mkono wa Mungu utakuwa dhidi ya Wakaldayo.

1548:15 Amu 4:10; Isa 45:1Mimi, naam, Mimi, nimenena;

naam, nimemwita yeye.

Nitamleta,

naye atafanikiwa katika lile nililomtuma.

1648:16 Isa 45:19; Zek 2:8-11; Isa 33:13; 50:5-9; 11:2“Nikaribieni na msikilize hili:

“Tangu tangazo la kwanza sikusema kwa siri;

wakati litokeapo, nitakuwako hapo.”

Sasa Bwana Mwenyezi amenituma,

kwa Roho wake.

1748:17 Ay 19:25; Za 32:4; Isa 54:8; 47:4; 28:9; Yer 7:13; Isa 49:10Hili ndilo asemalo Bwana,

Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:

“Mimi ni Bwana, Mungu wako,

nikufundishaye ili upate faida,

nikuongozaye katika njia ikupasayo kuiendea.

1848:18 Kum 5:29; Isa 42:23; Za 147:14; 45:8; Isa 54:13; 33:21; 45:5Laiti ungesikiliza kwa makini maagizo yangu,

amani yako ingekuwa kama mto,

haki yako kama mawimbi ya bahari.

1948:19 Mwa 22:17; Ay 5:25; Yer 35:19; Isa 43:5; 61:9; Mwa 12:2; Isa 56:5Wazao wako wangekuwa kama mchanga,

watoto wako kama chembe zake zisizohesabika;

kamwe jina lao lisingefutiliwa mbali,

wala kuangamizwa kutoka mbele zangu.”

2048:20 Zek 2:6-7; Ufu 18:4; Isa 12:6; Mik 4:10; Isa 52:11; Yer 48:6; 50:8Tokeni huko Babeli,

kimbieni kutoka kwa Wakaldayo!

Tangazeni hili kwa kelele za shangwe

na kulihubiri.

Lipelekeni mpaka miisho ya dunia;

semeni, “Bwana amemkomboa

mtumishi wake Yakobo.”

2148:21 Isa 41:17; 33:16; 30:25; Kut 17:6; Za 105:41; Hes 20:11Hawakuona kiu alipowaongoza kupita jangwani;

alifanya maji yatiririke kutoka kwenye mwamba kwa ajili yao;

akapasua mwamba

na maji yakatoka kwa nguvu.

2248:22 Isa 3:11; 57:21; Ay 3:26“Hakuna amani kwa waovu,” asema Bwana.