Isaya 47 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 47:1-15

Anguko La Babeli

147:1 Mao 2:10; Isa 21:9; 23:12; Yer 51:33; Zek 2:7; Ay 2:13; Isa 29:4“Shuka uketi mavumbini,

ee Bikira Binti Babeli;

keti chini pasipo na kiti cha enzi,

ee binti wa Wakaldayo.

Hutaitwa tena mwororo wala wa kupendeza.

247:2 Mt 24:41; Kut 11:5; Amu 16:21; Mwa 24:65; Isa 32:11Chukua mawe ya kusagia, usage unga,

vua shela yako.

Pandisha mavazi yako, ondoa viatu vyako,

vuka vijito kwa shida.

347:3 Mwa 2:25; Rum 12:19; Neh 3:5; Isa 13:18-19; 20:4; 34:8; Eze 16:37Uchi wako utafunuliwa

na aibu yako itaonekana.

Nitalipa kisasi;

sitamhurumia hata mmoja.”

447:4 Yer 50:34; Amo 4:13; Isa 48:2, 17; Ay 19:25Mkombozi wetu: Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake;

ndiye yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

547:5 Dan 2:37; Isa 13:10, 19; 9:2; 21:9; Ufu 17:18; Ay 2:13; Ufu 18:7“Keti kimya, ingia gizani,

Binti wa Wakaldayo,

hutaitwa tena malkia wa falme.

647:6 2Nya 28:9; Isa 10:13; Zek 1:15; Kum 13:15; Yer 50:11; Isa 14:6; 42:24Niliwakasirikia watu wangu

na kuaibisha urithi wangu;

niliwatia mikononi mwako,

nawe hukuwaonea huruma.

Hata juu ya wazee

uliweka nira nzito sana.

747:7 Ufu 18:7; Kum 32:29; Isa 10:13; Dan 4:30; Isa 42:23-25Ukasema, ‘Nitaendelea

kuwa malkia milele!’

Lakini hukutafakari mambo haya

wala hukuwaza juu ya kile kingeweza kutokea.

847:8 Isa 32:9; 45:6; 49:21; 54:4; Sef 2:15; Ufu 18:7“Sasa basi, sikiliza, ewe kiumbe mpenda anasa,

ukaaye mahali pako pa salama,

na kujiambia mwenyewe,

‘Mimi ndiye, wala hakuna mwingine zaidi yangu.

Kamwe sitakuwa mjane,

wala sitafiwa na watoto.’

947:9 1The 5:3; Isa 13:8; Nah 3:4; Za 55:15; Mal 3:5; Kum 18:10-11; Ufu 9:21; 18:8-10Haya mawili yatakupata, kufumba na kufumbua,

katika siku moja:

kufiwa na watoto, na ujane.

Yote yatakupata kwa kipimo kikamilifu,

ijapokuwa uchawi wako ni mwingi,

na uaguzi wako ni mwingi.

1047:10 Ay 15:31; 2Fal 21:16; Isa 5:21; 29:15; Za 52:7; 62:10Umeutegemea uovu wako,

nawe umesema, ‘Hakuna yeyote anionaye.’

Hekima yako na maarifa yako vinakupoteza

unapojiambia mwenyewe,

‘Mimi ndiye, wala hakuna mwingine zaidi yangu.’

1147:11 Dan 5:30; Za 55:15; 1The 5:3; Isa 10:3; 14:15; 21:9; Lk 17:27; Isa 17:14Maafa yatakujia,

nawe hutaweza kuyaondoa kwa uaguzi.

Janga litakuangukia,

wala hutaweza kulikinga kwa fidia;

msiba mkuu usioweza kuutabiri

utakujia ghafula.

1247:12 Kut 7:11“Endelea basi na uaguzi wako,

na wingi wa uchawi wako,

ambao umeutumikia tangu utoto wako.

Labda utafanikiwa,

labda unaweza ukasababisha hofu kuu.

1347:13 Yer 51:58; Hab 2:13; Isa 19:3; 5:29; 43:13; 57:10; 46:7; Dan 2:2Ushauri wote uliopokea umekuchosha bure!

Wanajimu wako na waje mbele,

wale watazama nyota watabiriao mwezi baada ya mwezi,

wao na wawaokoe na lile linalokuja juu yenu.

1447:14 Isa 5:24; Nah 1:10; Yer 50:30-32; Isa 30:30; 10:17Hakika wako kama mabua makavu;

moto utawateketeza.

Hawawezi hata kujiokoa wao wenyewe

kutokana na nguvu za mwali wa moto.

Hapa hakuna makaa ya kumtia mtu yeyote joto;

hapa hakuna moto wa kuota.

1547:15 Ufu 18:11; Isa 44:17Hayo ndiyo yote wanayoweza kuwatendea ninyi,

hawa ambao umetaabika nao

na kufanya nao biashara tangu utoto.

Kila mmoja atatoroka;

hakuna yeyote awezaye kukuokoa.