Isaya 46 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 46:1-13

Miungu Ya Babeli

146:1 Yer 51:44; Isa 45:20; 21:9; Yer 50:2Beli anasujudu hadi nchi, Nebo anainama;

sanamu zao zabebwa na wanyama wa mizigo.

Vinyago hivi mnavyobeba kila mahali ni mzigo wa kulemea,

mzigo kwa waliochoka.

246:2 2Sam 5:21; Yer 51:47; Amu 18:17-18Vinyago pamoja na wale wanaovibeba wanainama chini;

hiyo miungu haiwezi kuwaokoa watu,

wote wanakwenda utumwani pamoja.

346:3 Isa 48:12; Kut 19:14; Isa 44:2; Kum 1:31; Za 28:9; 22:10“Nisikilizeni mimi, ee nyumba ya Yakobo,

ninyi nyote mliobaki wa nyumba ya Israeli,

ninyi ambao nimewategemeza tangu mlipotungwa mimba,

nami nimewabeba tangu kuzaliwa kwenu.

446:4 Mal 3:6; Za 71:18; Isa 43:13; Kum 32:39; Za 18:35; 119:117Hata mpaka wakati wa uzee wenu na mvi, Mimi ndiye,

Mimi ndiye nitakayewasaidia ninyi.

Nimewahuluku, nami nitawabeba,

nitawasaidia ninyi na kuwaokoa.

546:5 Kut 15:11; Ay 41:10; Isa 40:18, 25; Yer 49:19“Mtanilinganisha na nani, au mtanihesabu kuwa sawa na nani?

Ni nani mtakayenifananisha naye ili tuweze kulinganishwa?

646:6 Kut 20:5; Hos 13:2; Isa 40:19; 44:17Wengine humwaga dhahabu kutoka kwenye mifuko yao,

na kupima fedha kwenye mizani;

huajiri mfua dhahabu kutengeneza mungu,

kisha huisujudia na kuiabudu.

746:7 1Sam 5:3; Isa 41:7; 1Fal 16:26Huiinua mabegani na kuichukua;

huiweka mahali pake, papo hapo ndipo isimamapo.

Wala haiwezi kusogea kutoka mahali pale.

Ingawa mtu huililia, haimjibu;

haiwezi kumwokoa kwenye taabu zake.

846:8 Isa 44:21; 1:2“Kumbukeni hili, litieni akilini,

liwekeni moyoni, enyi waasi.

946:9 Kum 8:10; Kut 8:10; Mk 12:32; Isa 41:22; 45:21Kumbukeni mambo yaliyopita, yale ya zamani za kale;

mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine;

mimi ndimi Mungu,

wala hakuna mwingine aliye kama mimi.

1046:10 Mit 19:21; Efe 1:11; Mdo 5:39; Isa 45:21; 41:22; 7:7-9; 44:26Ni mimi nitangazaye mwisho tangu mwanzo,

naam, tangu zamani za kale,

mambo ambayo hayajatendeka.

Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama,

nami nitatenda mapenzi yangu yote.

1146:11 Mwa 41:25; Yer 44:28; Amu 4:10; Ezr 1:2; Isa 8:5Kutoka mashariki ninaita ndege awindaye;

kutoka nchi ya mbali,

mtu atakayetimiza kusudi langu.

Lile ambalo nimelisema, ndilo nitakalolitimiza;

lile nililolipanga, ndilo nitakalolitenda.

1246:12 Yer 2:5; Za 119:150; Rum 10:3; Kut 32:9; Isa 9:9Nisikilizeni, ninyi wenye mioyo migumu,

ninyi mlio mbali na haki.

1346:13 Isa 24:23; Mdo 13:36; Rum 1:17; Isa 1:26; 45:8; Rum 3:21; Yoe 2:32Ninaleta haki yangu karibu,

haiko mbali;

wala wokovu wangu hautachelewa.

Nitawapa Sayuni wokovu,

Israeli utukufu wangu.