Isaya 42 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 42:1-25

Mtumishi Wa Bwana

142:1 Isa 49:3-6; 14:1; Yn 3:34; Lk 9:35; Mwa 49:10; Mt 3:16-17; 20:28“Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza,

mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye;

nitaweka Roho yangu juu yake,

naye ataleta haki kwa mataifa.

242:2 Za 8:1-4Hatapaza sauti wala kupiga kelele,

wala hataiinua sauti yake barabarani.

342:3 Za 72:2; Mt 12:17-21; Za 96:13; Isa 36:6; Ay 30:24; 13:25Mwanzi uliopondeka hatauvunja,

na utambi unaofuka moshi hatauzima.

Kwa uaminifu ataleta haki,

442:4 Mwa 49:10; Ebr 12:2; Rum 8:22-25; Kut 34:29; Isa 51:4; 11:11hatazimia roho wala kukata tamaa,

mpaka atakaposimamisha haki juu ya dunia.

Visiwa vitaweka tumaini lao katika sheria yake.”

542:5 Za 24:2; Mdo 17:24-25; Isa 44:24; 48:13; Za 102:25Hili ndilo asemalo Mungu, Bwana,

yeye aliyeziumba mbingu na kuzitanda,

aliyeitandaza dunia na vyote vitokavyo humo,

awapaye watu wake pumzi,

na uzima kwa wale waendao humo:

642:6 Kut 31:2; Amu 4:10; Yer 23:6; Mdo 13:47; Dan 9:7; Isa 26:18; Lk 22:20“Mimi, Bwana, nimekuita katika haki;

nitakushika mkono wako.

Nitakulinda na kukufanya

kuwa Agano kwa ajili ya watu

na nuru kwa Mataifa,

742:7 Zek 9:11; 2:7; 2Tim 2:26; Lk 4:19; Mt 11:5; Isa 32:3; 51:14; Za 146:8kuwafungua macho wale wasioona,

kuwaacha huru kutoka kifungoni waliofungwa jela,

na kuwafungua kutoka gerezani

wale wanaokaa gizani.

842:8 Kut 3:14-15; 6:3; Isa 48:11; Za 81:10; Ebr 2:14-15; Kut 8:10; Isa 46:9“Mimi ndimi Bwana; hilo ndilo Jina langu!

Sitampa mwingine utukufu wangu

wala sanamu sifa zangu.

942:9 Isa 41:22; 40:21; Eze 2:4Tazama, mambo ya kwanza yametokea,

nami natangaza mambo mapya;

kabla hayajatokea

nawatangazia habari zake.”

Wimbo Wa Kumsifu Bwana

1042:10 Za 98:1; Kum 30:4; Za 96:11; 1Fal 10:9; 1Nya 16:32; Za 48:10; Isa 11:11Mwimbieni Bwana wimbo mpya,

sifa zake toka miisho ya dunia,

ninyi mshukao chini baharini,

na vyote vilivyomo ndani yake,

enyi visiwa na wote wakaao ndani yake.

1142:11 Mwa 25:13; Isa 32:16; 52:7; Nah 1:15; Isa 60:7; Amu 1:36Jangwa na miji yake na vipaze sauti zao;

makao anamoishi Kedari na yashangilie.

Watu wa Sela waimbe kwa furaha,

na wapige kelele kutoka vilele vya milima.

1242:12 Isa 24:15; 1Nya 16:24; 1Pet 2:9; Za 26:7; 66:2Wampe Bwana utukufu,

na kutangaza sifa zake katika visiwa.

1342:13 Isa 9:6; Yos 6:5; Yoe 3:16; Isa 66:14; 26:11; Kut 14:14; Hos 11:10Bwana ataenda kama mtu mwenye nguvu,

kama shujaa atachochea shauku yake,

kwa kelele ataamsha kilio cha vita,

naye atashinda adui zake.

1442:14 Es 4:14; Yer 4:31; Mwa 43:31; Lk 18:7“Kwa muda mrefu nimenyamaza kimya,

nimekaa kimya na kujizuia.

Lakini sasa, kama mwanamke wakati wa kujifungua,

ninapiga kelele, ninatweta na kushusha pumzi.

1542:15 Eze 38:20; Za 107:33; Isa 11:15; 50:2; Nah 1:4-6Nitaharibu milima na vilima

na kukausha mimea yako yote;

nitafanya mito kuwa visiwa

na kukausha mabwawa.

1642:16 Kum 4:31; Ebr 13:5; Yer 31:8-9; Isa 26:7; 29:24; 57:18; Mdo 26:18; Ebr 13:5Nitawaongoza vipofu kwenye njia ambayo hawajaijua,

kwenye mapito wasiyoyazoea nitawaongoza;

nitafanya giza kuwa nuru mbele yao,

na kufanya mahali palipoparuza kuwa laini.

Haya ndiyo mambo nitakayofanya;

mimi sitawaacha.

1742:17 Kut 32:4; Za 97:7; Isa 1:26Lakini wale wanaotumaini sanamu,

wanaoviambia vinyago, ‘Ninyi ndio miungu yetu,’

watarudishwa nyuma kwa aibu kubwa.

Israeli Kipofu Na Kiziwi

18“Sikieni, enyi viziwi;

tazameni, enyi vipofu, mpate kuona!

1942:19 Isa 43:8; Eze 12:2; Isa 41:8-9; Hag 1:13; Isa 26:3Ni nani aliye kipofu isipokuwa mtumishi wangu,

na kiziwi kama mjumbe ninayemtuma?

Ni nani aliye kipofu kama yeye aliyejitoa kwangu,

aliye kipofu kama mtumishi wa Bwana?

2042:20 Isa 6:9-10; Yer 5:21; Rum 2:21; Yer 6:10; Isa 48:21; 41:17Mmeona vitu vingi, lakini hamkuzingatia;

masikio yenu yako wazi, lakini hamsikii chochote.”

2142:21 2Kor 3:7; Isa 43:25Ilimpendeza Bwana

kwa ajili ya haki yake

kufanya sheria yake kuwa kuu na tukufu.

2242:22 Isa 24:18-22; Lk 19:41-44; Amu 6:4; 2Fal 24:13; Isa 5:29; Za 66:11; Yos 22:5; Isa 1:14; 30:11Lakini hili ni taifa lililoibwa na kutekwa nyara,

wote wamenaswa katika mashimo,

au wamefichwa katika magereza.

Wamekuwa nyara,

wala hapana yeyote awaokoaye.

Wamefanywa mateka,

wala hapana yeyote asemaye, “Warudishe.”

2342:23 Kum 32:29; Za 81:13; Isa 47:7; 48:18; 57:11Ni nani miongoni mwenu atakayesikiliza hili,

au atakayezingatia kwa makini katika wakati ujao?

2442:24 2Fal 17:6; Isa 43:28; 10:5-6Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka,

na Israeli kwa wateka nyara?

Je, hakuwa yeye, Bwana,

ambaye tumetenda dhambi dhidi yake?

Kwa kuwa hawakufuata njia zake,

hawakutii sheria zake.

2542:25 Hos 7:9; Nah 1:6; 2Fal 22:13; Ay 40:11; Eze 7:19; 2Fal 25:9; Isa 29:13Hivyo akawamwagia hasira yake inayowaka,

ukali wa vita.

Iliwazunguka kwa miali ya moto, lakini hata hivyo hawakuelewa;

iliwateketeza, lakini hawakuyatia moyoni.