Isaya 41 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 41:1-29

Msaidizi Wa Israeli

141:1 Za 37:7; Isa 48:16; 50:8; Hab 2:20; Zek 2:13; Isa 11:11; 1Sam 2:4“Nyamazeni kimya mbele zangu, enyi visiwa!

Mataifa na wafanye upya nguvu zao!

Wao na wajitokeze, kisha waseme,

tukutane pamoja mahali pa hukumu.

241:2 2Sam 22:43; Isa 40:24; Yer 51:11; Ezr 1:2; Isa 44:28; Yer 50:3; 25:9“Ni nani aliyemchochea mmoja kutoka mashariki,

akimwita katika haki kwa utumishi wake?

Huyatia mataifa mikononi mwake,

na kuwatiisha wafalme mbele zake.

Huwafanya kuwa mavumbi kwa upanga wake,

huwafanya makapi yapeperushwayo na upepo kwa upinde wake.

341:3 Dan 8:4Huwafuatia na kuendelea salama,

katika njia ambayo miguu yake haijawahi kupita.

441:4 Isa 48:12; Ufu 22:13; Mdo 15:18; Isa 43:7; Kum 32:29Ni nani aliyefanya jambo hili na kulitimiliza,

akiita vizazi tangu mwanzo?

Mimi, Bwana, ni wa kwanza

nami nitakuwa pamoja na wa mwisho:

mimi Bwana ndiye.”

541:5 Eze 26:17-18; Kum 30:4; Isa 11:11-12Visiwa vimeliona na kuogopa,

miisho ya dunia inatetemeka.

Wanakaribia na kuja mbele,

641:6 Isa 1:6kila mmoja humsaidia mwingine

na kusema kwa ndugu yake, “Uwe hodari!”

741:7 Isa 40:19; 44:13; Yer 30:3-5Fundi humtia moyo sonara,

yeye alainishaye kwa nyundo

humhimiza yeye agongeaye kwenye fuawe,

Humwambia yeye aunganishaye, “Ni kazi njema.”

Naye huikaza sanamu kwa misumari ili isitikisike.

841:8 Mwa 18:19; Isa 29:22; Neh 9:7; 2Nya 20:7; Yak 2:23; Isa 63:16; Za 136:22“Lakini wewe, ee Israeli, mtumishi wangu,

Yakobo, niliyemchagua,

ninyi wazao wa Abrahamu rafiki yangu,

941:9 Isa 37:16; Kum 7:6; Isa 20:3; 11:12nilikuchukua toka miisho ya dunia,

nilikuita kutoka pembe zake za mbali.

Nilisema, ‘Wewe ni mtumishi wangu’;

nimekuchagua, wala sikukukataa.

1041:10 Kum 3:22; Rum 8:3; Isa 49:8; Yer 30:10; 46:27-28; Ay 40:14; Za 18:35Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;

usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.

Nitakutia nguvu na kukusaidia;

nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

1141:11 Isa 17:12; 54:17; Kut 23:22; Isa 29:8; Zek 12:3; Yer 2:3; Isa 29:23“Wote walioona hasira dhidi yako

hakika wataaibika na kutahayarika,

wale wakupingao

watakuwa kama vile si kitu, na kuangamia.

1241:12 Za 37:35-36; Isa 34:12; Ay 7:8; Isa 29:20; 17:14Ingawa utawatafuta adui zako,

hutawaona.

Wale wanaopigana vita dhidi yako

watakuwa kama vile si kitu kabisa.

1341:13 Za 73:23; Isa 42:6; 45:1; 51:18Kwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,

nikushikaye mkono wako wa kuume

na kukuambia, Usiwe na hofu,

nitakusaidia.

1441:14 Ay 4:19; Za 22:6; Kut 15:13; Ay 19:23; Isa 1:27Usiogope, ee Yakobo uliye mdudu,

ee Israeli uliye mdogo,

kwa kuwa Mimi mwenyewe nitakusaidia,” asema Bwana,

Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

1541:15 Ay 41:30; Mik 4:13; Isa 21:10; Kut 19:18; Yer 9:10; Eze 33:28“Tazama, nitakufanya chombo cha kupuria,

kipya na chenye makali, chenye meno mengi.

Utaipura milima na kuiponda

na kuvifanya vilima kuwa kama makapi.

1641:16 Yer 51:2; Isa 45:25; 60:19; Dan 2:35; Yer 15:7; Isa 25:9; Mk 1:24Utaipepeta, nao upepo utaichukua,

dhoruba itaipeperushia mbali.

Bali wewe utajifurahisha katika Bwana

na katika utukufu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

1741:17 Isa 43:20; 35:7; 30:19“Maskini na wahitaji wanatafuta maji,

lakini hayapo,

ndimi zao zimekauka kwa kiu.

Lakini Mimi Bwana nitawajibu,

Mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha.

1841:18 Isa 30:25; 43:19; Ay 38:26; Isa 35:7; 2Fal 3:17Nitaifanya mito itiririke juu ya vilima vilivyo kame,

nazo chemchemi ndani ya mabonde.

Nitaligeuza jangwa liwe mabwawa ya maji,

nayo ardhi iliyokauka kuwa chemchemi za maji.

1941:19 Isa 60:13; Kut 25:10-13; Isa 37:24; 44:14Katika jangwa nitaotesha

mwerezi, mshita, mhadasi na mzeituni.

Nitaweka misunobari, mivinje na misanduku

pamoja huko nyikani,

2041:20 Ay 12:9; Isa 4:5ili kwamba watu wapate kuona na kujua,

wapate kufikiri na kuelewa,

kwamba mkono wa Bwana umetenda hili,

kwamba yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ndiye alilifanya.”

2141:21 Isa 43:14; 44:6Bwana asema, “Leta shauri lako.

Toa hoja yako,” asema Mfalme wa Yakobo.

2241:22 Isa 48:14; 65:17; Yn 13:19; Isa 43:9; 45:21“Leteni sanamu zenu zituambie

ni nini kitakachotokea.

Tuambieni mambo ya zamani yalikuwa nini,

ili tupate kuyatafakari

na kujua matokeo yake ya mwisho.

Au tutangazieni mambo yatakayokuja,

2341:23 Kum 18:22; Isa 44:7-8; Yer 10:5; Isa 43:5; 2Fal 19:26tuambieni ni nini kitakachotokea baadaye,

ili tupate kujua kuwa ninyi ni miungu.

Fanyeni jambo lolote zuri au baya,

ili tupate kutishika na kujazwa na hofu.

2441:24 Isa 37:19; 1Kor 8:4; Za 115:8; 1Sam 12:21; Isa 48:8Lakini ninyi ni zaidi ya bure kabisa,

na kazi zenu hazifai kitu kabisa;

yeye awachaguaye ni chukizo sana.

2541:25 Yer 51:48; Nah 3:14; 2Sam 22:43; Yer 50:9“Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini,

naye yuaja, mmoja toka mawio ya jua aliitaye Jina langu.

Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope,

kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia.

2641:26 Hab 2:18-19; 1Fal 18:26; Isa 52:6Ni nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua,

au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa sawa’?

Hakuna aliyenena hili,

hakuna aliyetangulia kusema hili,

hakuna yeyote aliyesikia maneno kutoka kwenu.

2741:27 Isa 48:3, 16; 40:9Nilikuwa wa kwanza kumwambia Sayuni,

‘Tazama, wako hapa!’

Nilimpa Yerusalemu mjumbe wa habari njema.

2841:28 Eze 22:30; Za 22:11; Isa 40:13-14; 50:2; 59:16; 64:7; Yer 25:4Ninatazama, lakini hakuna yeyote:

hakuna yeyote miongoni mwao awezaye kutoa shauri,

hakuna yeyote wa kutoa jibu wakati ninapowauliza.

2941:29 Yer 5:13; 1Sam 12:21; Isa 37:19Tazama, wote ni ubatili!

Matendo yao ni bure;

vinyago vyao ni upepo mtupu na machafuko.