Isaya 40 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 40:1-31

Faraja Kwa Watu Wa Mungu

140:1 Zek 1:17; 2Kor 1:3; Sef 3:14-17; Yer 31:13; Isa 49:13; 57:18Wafarijini, wafarijini watu wangu,

asema Mungu wenu.

240:2 Mwa 34:3; Isa 41:11-13; 49:25; Zek 9:12; Ufu 18:6; Yer 16:18; Law 26:4Sema na Yerusalemu kwa upole,

umtangazie

kwamba kazi yake ngumu imekamilika,

kwamba dhambi yake imefanyiwa fidia,

kwamba amepokea kutoka mkononi mwa Bwana

maradufu kwa ajili ya dhambi zake zote.

340:3 Isa 11:16; Mt 3:3; Mal 3:1; Mk 1:3; Isa 43:19; Yn 1:23Sauti ya mtu aliaye:

“Itengenezeni jangwani njia ya Bwana,

nyoosheni njia kuu nyikani

kwa ajili ya Mungu wetu.

440:4 Za 26:12; Yer 31:9; Isa 2:14; 49:11; 26:7; 45:2Kila bonde litainuliwa,

kila mlima na kilima kitashushwa;

penye mabonde patanyooshwa,

napo palipoparuza patasawazishwa.

540:5 Kut 16:7; Isa 58:14; Lk 3:4-6; Eze 36:23; Hes 14:21; Isa 59:19; Lk 2:20Utukufu wa Bwana utafunuliwa,

nao wanadamu wote watauona pamoja.

Kwa maana kinywa cha Bwana kimenena.”

640:6 Ay 14:2; Mwa 6:3; Isa 29:5Sauti husema, “Piga kelele.”

Nami nikasema, “Nipige kelele gani?”

“Wanadamu wote ni kama majani,

nao utukufu wao wote

ni kama maua ya kondeni.

740:7 Kut 15:10; Ay 41:21; Yos 8:12; Isa 15:6; Za 103:6; Eze 22:21Majani hunyauka na maua huanguka,

kwa sababu pumzi ya Bwana huyapuliza.

Hakika wanadamu ni majani.

840:8 1Pet 1:25; Isa 59:21; Mt 5:18; Za 119:89; Isa 5:24; Yak 1:10; Mit 19:21Majani hunyauka na maua huanguka,

lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.”

940:9 Nah 1:15; Isa 25:9; Rum 10:15; Isa 41:27; 52:7-10; 1Kor 15:1-4Wewe uletaye habari njema Sayuni,

panda juu ya mlima mrefu.

Wewe uletaye habari njema Yerusalemu,

inua sauti yako kwa kupiga kelele,

inua sauti, usiogope;

iambie miji ya Yuda,

“Yuko hapa Mungu wenu!”

1040:10 Ufu 22:7; Isa 35:4; Za 44:3; Isa 9:6-7; Ufu 22:12; Mt 21:5; Isa 28:2Tazameni, Bwana Mwenyezi anakuja na nguvu,

nao mkono wake ndio utawalao kwa ajili yake.

Tazameni, ujira wake u pamoja naye,

nayo malipo yake yanafuatana naye.

1140:11 Za 28:9; Yn 10:11; Ebr 13:20; Mwa 48:15; Mik 5:4; Hes 12:11; Kum 26:19Huchunga kundi lake kama mchungaji wa mifugo:

Hukusanya wana-kondoo katika mikono yake

na kuwachukua karibu na moyo wake,

huwaongoza taratibu wale wanyonyeshao.

1240:12 Mit 30:4; Ebr 1:10-12; Ay 38:10; 12:15; Mit 16:11Ni nani aliyepima maji ya bahari

kwenye konzi ya mkono wake,

au kuzipima mbingu kwa shibiri40:12 Shibiri ni sawa na sentimita 20 au inchi 8. yake?

Ni nani aliyeyashika mavumbi ya dunia katika kikapu,

au kupima milima kwenye kipimio

na vilima kwenye mizani?

1340:13 Ay 15:8; 1Kor 2:16; Rum 11:34Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya Bwana,

au kumfundisha akiwa kama mshauri wake?

1440:14 Ay 21:22; Kol 2:3; Ay 12:13; 34:13; Isa 55:9Ni nani ambaye Bwana ametaka shauri kwake ili kumwelimisha,

naye ni nani aliyemfundisha njia iliyo sawa?

Ni nani aliyemfundisha maarifa

au kumwonyesha mapito ya ufahamu?

1540:15 Za 62:9; Isa 2:22; Kum 9:21Hakika mataifa ni kama tone ndani ya ndoo,

ni kama vumbi jembamba juu ya mizani,

huvipima visiwa kana kwamba vilikuwa vumbi laini.

1640:16 Mik 6:7; Ebr 10:5-9; Isa 37:24; Za 50:9-11Lebanoni hautoshi kwa moto wa madhabahuni,

wala wanyama wake hawatoshi kwa sadaka za kuteketezwa.

1740:17 Isa 30:28; Ay 12:19; Isa 29:7; Dan 4:35; Isa 37:19Mbele yake mataifa yote ni kama si kitu,

yanaonekana yasio na thamani

na zaidi ya bure kabisa.

1840:18 Mdo 17:29; Kut 8:10; Kum 4:15; 1Sam 2:2Basi, utamlinganisha Mungu na nani?

Utamlinganisha na kitu gani?

1940:19 Kut 20:4; Zek 10:2; Yer 10:3-4; Isa 31:7; 37:19; 42:17; Hab 2:18Kwa habari ya sanamu, fundi huisubu,

naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabu

na kuitengenezea mikufu ya fedha.

2040:20 Isa 44:19; 5:3Mtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hii

huuchagua mti usiooza.

Humtafuta fundi stadi

wa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika.

2140:21 Mdo 14:17; Rum 1:19; Isa 48:13; 51:13; 2Fal 19:25Je, hujui?

Je, hujasikia?

Je, hujaambiwa tangu mwanzo?

Je, hujafahamu tangu kuumbwa kwa dunia?

2240:22 Hes 13:33; Ay 22:14; 36:29; 2Nya 6:18; Isa 48:13; Ay 26:7Anakaa kwenye kiti cha enzi juu ya duara ya dunia,

nao watu wakaao ndani yake ni kama panzi.

Huzitandaza mbingu kama chandarua,

na kuzitandaza kama hema la kuishi.

2340:23 Ay 12:18; Isa 34:12; Za 107:40; Amo 2:3Huwafanya wakuu kuwa si kitu,

na kuwashusha watawala wa dunia hii kuwa kitu bure.

2440:24 2Sam 22:16; Isa 11:4; Ay 5:3; 8:12; 18:16; 24:24; Isa 41:2, 16Mara baada ya kupandwa,

mara baada ya kutiwa ardhini,

mara baada ya kutoa mizizi yao ardhini,

ndipo huwapulizia nao wakanyauka,

nao upepo wa kisulisuli

huwapeperusha kama makapi.

2540:25 Kum 4:15; Mdo 17:24-29; 1Nya 16:25; Isa 37:23“Utanilinganisha mimi na nani?

Au ni nani anayelingana nami?” asema yeye Aliye Mtakatifu.

2640:26 Za 89:11-13; 2Fal 17:16; Neh 9:6; Isa 34:16; 51:6; Ay 9:4; Efe 1:19Inueni macho yenu mtazame mbinguni:

Ni nani aliyeumba hivi vyote?

Ni yeye aletaye nje jeshi la nyota moja baada ya nyingine

na kuziita kila moja kwa jina lake.

Kwa sababu ya uweza wake mkuu na nguvu zake kuu,

hakuna hata mojawapo inayokosekana.

2740:27 Ay 6:29; Lk 18:7-8; Ay 27:2Kwa nini unasema, ee Yakobo,

nanyi ee Israeli, kulalamika,

“Njia yangu imefichwa Bwana asiione,

Mungu wangu hajali shauri langu?”

2840:28 Kum 33:27; Za 90:2; Rum 11:33; Isa 37:16; 44:12; Za 147:5Je wewe, hufahamu?

Je wewe, hujasikia?

Bwana ni Mungu wa milele,

Muumba wa miisho ya dunia.

Hatachoka wala kulegea,

wala hakuna hata mmoja

awezaye kuupima ufahamu wake.

2940:29 Isa 57:19; Yer 31:25; Mwa 18:14; Za 68:35; 119:28Huwapa nguvu waliolegea

na huongeza nguvu za wadhaifu.

3040:30 Isa 9:17; Yer 9:21; Isa 5:27Hata vijana huchoka na kulegea,

nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka,

3140:31 2Fal 6:33; Kut 19:4; Ebr 12:1-3; Mao 3:25; 2Kor 4:8-10, 16; Za 37:9; Isa 30:18bali wale wamtumainio Bwana

atafanya upya nguvu zao.

Watapaa juu kwa mbawa kama tai;

watapiga mbio wala hawatachoka,

watatembea kwa miguu wala hawatazimia.