Isaya 38 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 38:1-22

Kuugua Kwa Mfalme Hezekia

(2 Wafalme 20:1-11; 2 Nyakati 32:24-26)

138:1 Isa 37:2-3; 2Sam 17:23; 2Fal 8:10Katika siku hizo Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemalo Bwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”

2Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana: 338:3 Neh 5:19; 13:14; Kum 6:18; Za 26:3; 1Fal 8:61; 2Nya 29:19; Za 6:8“Ee Bwana, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Naye Hezekia akalia kwa uchungu.

438:4 1Sam 13:13; Isa 39:5Ndipo neno la Bwana likamjia Isaya, kusema: 538:5 2Fal 18:2-3; Za 6:6“Nenda ukamwambie Hezekia, ‘Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa baba yako Daudi: Nimeyasikia maombi yako na nimeona machozi yako. Nitakuongezea miaka kumi na mitano katika maisha yako. 638:6 Isa 31:5; 37:35Nami nitakuokoa wewe pamoja na mji huu mkononi mwa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu.

738:7 Mwa 24:14; 2Fal 20:8; 2Nya 32:31; Isa 7:11, 14; 20:3“ ‘Hii ndiyo ishara ya Bwana kwako ya kwamba Bwana atafanya kile alichoahidi: 838:8 Yos 10:13Nitafanya kivuli cha jua kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi kirudi nyuma madaraja kumi.’ ” Hivyo jua likarudi nyuma madaraja kumi ambayo lilikuwa limeshuka.

9Maandiko ya Hezekia mfalme wa Yuda baada ya kuugua kwake na kupona:

1038:10 Ay 17:16; Za 102:24; 2Kor 1:9; Ay 17:11; Za 107:18Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu,

je, ni lazima nipite katika malango ya mauti,38:10 Mauti hapa maana yake ni Kuzimu.

na kupokonywa miaka yangu iliyobaki?”

1138:11 Za 27:13; Ay 28:13; 35:14; Isa 12:2; Za 116:5Nilisema, “Sitamwona tena Bwana,

Bwana katika nchi ya walio hai,

wala sitamtazama tena mwanadamu,

wala kuwa na wale ambao sasa wanakaa katika ulimwengu huu.

1238:12 2Kor 5:4; Ay 4:21; Isa 33:20; Ebr 1:12; Hes 11:15; Za 32:4; 1Pet 1:13-14Kama hema la mchunga mifugo,

nyumba yangu imebomolewa na kutwaliwa kutoka kwangu.

Kama mfumaji nimevingirisha maisha yangu,

naye amenikatilia mbali kutoka kitanda cha mfumi.

Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

1338:13 Ay 9:17; Mao 3:4; Yer 34:17; Za 37:7; 51:8; Ay 10:16; Dan 6:24Nilingoja kwa uvumilivu hadi mapambazuko,

lakini alivunja mifupa yangu yote kama simba.

Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

1438:14 Isa 59:11; Mwa 50:24; Ay 17:3; Mwa 8:8; Za 6:7Nililia kama mbayuwayu au korongo,

niliomboleza kama hua aombolezaye.

Macho yangu yalififia nilipotazama mbinguni.

Ee Bwana, ninataabika, njoo unisaidie!”

1538:15 Ay 7:11; 1Fal 21:27; Za 39:9; 2Sam 7:20Lakini niseme nini?

Amesema nami, naye yeye mwenyewe amelitenda hili.

Nitatembea kwa unyenyekevu

katika miaka yangu yote

kwa sababu ya haya maumivu makali

ya nafsi yangu.

1638:16 Ebr 12:9; Za 119:25Bwana, kwa mambo kama haya watu huishi,

nayo roho yangu hupata uzima katika hayo pia.

Uliniponya

na kuniacha niishi.

1738:17 Yer 31:34; Mik 7:19; Ay 17:16; Za 103:3, 12; Rum 8:28; Ebr 12:11; Isa 43:25Hakika ilikuwa ya faida yangu

ndiyo maana nikapata maumivu makali.

Katika upendo wako ukaniokoa

kutoka shimo la uharibifu;

umeziweka dhambi zangu zote

nyuma yako.

1838:18 Mhu 9:10; Hes 16:30; Za 6:5; 30:9; 88:10-11; 115:17Kwa maana kaburi38:18 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. haliwezi kukusifu,

mauti haiwezi kuimba sifa zako;

wale washukao chini shimoni

hawawezi kuutarajia uaminifu wako.

1938:19 Kum 6:7; 11:19; Za 78:3; 118:7; 119:175Walio hai, walio hai: hao wanakusifu,

kama ninavyofanya leo.

Baba huwaambia watoto wao

habari za uaminifu wako.

2038:20 Za 68:25; 9:13; 45:8; 116:17-19; 63:4; 23:6Bwana ataniokoa,

nasi tutaimba kwa vyombo vya nyuzi

siku zote za maisha yetu

katika Hekalu la Bwana.

21Isaya alikuwa amesema, “Tengenezeni dawa ya kubandika ya tini, mweke juu ya jipu, naye atapona.”

22Hezekia alikuwa ameuliza, “Kutakuwa na ishara gani kwamba nitapanda kwenda Hekalu la Bwana?”