Isaya 37 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 37:1-38

Kuokolewa Kwa Yerusalemu Kunatabiriwa

(2 Wafalme 19:1-7)

137:1 2Nya 34:19; Mwa 37:34; 1Fal 8:33; Mt 21:13Mfalme Hezekia aliposikia haya, akararua nguo zake na kuvaa nguo ya gunia, naye akaenda katika Hekalu la Bwana. 237:2 2Fal 22:14; Isa 13:1; 36:3; 2Fal 18:18Akawatuma Eliakimu msimamizi wa nyumba ya mfalme, Shebna mwandishi, na viongozi wa makuhani, wote wakiwa wamevaa nguo za magunia, waende kwa nabii Isaya mwana wa Amozi. 337:3 Isa 66:9; Hos 13:13; 2Fal 19:3; Amu 6:2; Isa 5:30; 26:18Wakamwambia, “Hili ndilo asemalo Hezekia: Siku hii ni siku ya dhiki, ya kukaripiwa na ya aibu, kama wakati watoto wanapofikia karibu kuzaliwa na kumbe hakuna nguvu ya kuwazaa. 437:4 Yak 5:14-15; Isa 36:13, 18-20; Amo 7:2; 2Nya 32:17; Yos 3:10; 1Sam 7:8Yamkini Bwana, Mungu wako atayasikia maneno ya jemadari wa jeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, tena kwamba atamkemea kwa maneno ambayo Bwana, Mungu wako ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wako.”

5Maafisa wa Mfalme Hezekia walipofika kwa Isaya, 637:6 Yos 1:9; Isa 7:4; Hes 15:30Isaya akawaambia, “Mwambieni bwana wenu, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Usiogope kwa hayo uliyoyasikia, yale maneno ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana nayo. 737:7 Isa 31:8; 1Nya 5:26Sikiliza! Nitatia roho fulani ndani yake ili kwamba atakaposikia taarifa fulani, atarudi nchi yake mwenyewe, nami huko nitafanya auawe kwa upanga.’ ”

837:8 Hes 33:20; Neh 11:30; Yer 34:7; Yos 10:3Jemadari wa jeshi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru ameondoka Lakishi, alirudi, akamkuta mfalme akipigana na Libna.

937:9 2Nya 32:11; Isa 20:3Basi Senakeribu akapata taarifa kwamba Tirhaka, Mkushi mfalme wa Misri, alikuwa anaenda kupigana naye. Aliposikia jambo hili akatuma wajumbe kwa Hezekia na neno hili: 1037:10 2Nya 32:11, 15; Isa 36:15“Mwambieni Hezekia mfalme wa Yuda: Usikubali huyo Mungu unayemtumainia akudanganye wakati anaposema, ‘Yerusalemu haitatiwa mkononi mwa mfalme wa Ashuru.’ 1137:11 Isa 36:18-20Hakika umesikia yale ambayo wafalme wa Ashuru wametenda kwa nchi zote, wakiwaangamiza kabisa. Je, wewe utaokolewa? 1237:12 Mwa 12:1-4; Mdo 7:2; 2Fal 18:11Je, miungu ya mataifa ambayo yaliangamizwa na baba zangu iliweza kuwaokoa? Yaani miungu ya Gozani, Harani, Resefu, na ya watu wa Edeni waliokuwa Telasari? 1337:13 Isa 10:9; 2Fal 17:24; Isa 36:20Yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme wa Arpadi, mfalme wa mji wa Sefarvaimu, au wa Hena au wa Iva?”

Maombi Ya Hezekia

1437:14 2Nya 32:17; 1Fal 8:33Hezekia akapokea barua kutoka kwa wale wajumbe naye akaisoma. Kisha akapanda katika Hekalu la Bwana, akaikunjua mbele za Bwana. 1537:15 2Nya 32:20Naye Hezekia akamwomba Bwana akisema: 1637:16 Kum 10:17; Za 46:10; Kut 25:22; Mwa 3:24; Za 86:10; Dan 4:34; Mdo 4:24“Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, uketiye juu ya kiti cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Wewe umeumba mbingu na nchi. 1737:17 Dan 9:18; Yer 25:29; 2Nya 6:40; 1Fal 8:29; 2Nya 32:17Tega sikio, Ee Bwana, usikie; fungua macho yako, Ee Bwana, uone; sikiliza maneno yote ambayo Senakeribu ametuma kumtukana Mungu aliye hai.

1837:18 2Fal 15:29; Nah 2:11-12“Ni kweli, Ee Bwana, kwamba wafalme wa Ashuru wameyaangamiza mataifa haya yote pamoja na nchi zao. 1937:19 Isa 36:20; Yer 2:11; Gal 4:8; Yos 7:15; Isa 26:14; 2Nya 13:9; Isa 40:18-20; 44:9-11Wameitupa miungu yao kwenye moto na kuiangamiza, kwa kuwa haikuwa miungu, bali miti na mawe tu, iliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. 2037:20 1Sam 17:46; Za 46:10; Mit 20:22; Yos 4:24Sasa basi, Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe kutoka mkononi mwake, ili kwamba falme zote duniani zipate kujua kwamba wewe peke yako, Ee Bwana, ndiwe Mungu.”

Kuanguka Kwa Senakeribu

(2 Wafalme 19:20-37)

2137:21 Isa 37:2Kisha Isaya mwana wa Amozi akapeleka ujumbe kwa Hezekia, akasema: “Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: Kwa sababu umeniomba kuhusu Senakeribu mfalme wa Ashuru, 2237:22 Isa 23:12; 10:32; Ay 16:4hili ndilo neno ambalo Bwana amelisema dhidi yake:

“Bikira binti Sayuni anakudharau na kukudhihaki.

Binti Yerusalemu anatikisa kichwa chake unapokimbia.

2337:23 Hes 15:30; Dan 7:25; Isa 2:11; 52:5; Eze 36:20-23; Ay 15:25; Isa 12:6Ni nani uliyemtukana na kumkufuru?

Ni nani uliyeinua sauti yako dhidi yake,

na kumwinulia macho yako kwa kiburi?

Ni dhidi ya yule Aliye Mtakatifu wa Israeli!

2437:24 Isa 14:8; 36:9; 1Fal 5:8-10; Isa 14:5, 13; 41:19; Hos 14:8Kupitia kwa wajumbe wako

umelundika matukano juu ya Bwana.

Nawe umesema,

‘Kwa magari yangu mengi ya vita,

nimepanda juu ya vilele vya milima,

vilele vya juu sana katika Lebanoni.

Nami nimeiangusha mierezi yake mirefu,

misunobari yake iliyo bora sana.

Nimefikia sehemu zake zilizoinuka juu sana,

misitu yake iliyo mizuri sana.

2537:25 Kum 11:10; Dan 4:30; Isa 19:6; 44:27; 10:14Nimechimba visima katika nchi za kigeni

na kunywa maji yake.

Kwa nyayo za miguu yangu

nimekausha vijito vyote vya Misri.’

2637:26 Mdo 4:27-28; 1Pet 2:8; Isa 25:1-2; Kum 13:16; Mdo 2:23; Isa 10:6“Je, hujasikia?

Zamani sana niliamuru hili.

Siku za kale nilipanga hili;

sasa nimelifanya litokee,

kwamba umegeuza miji yenye ngome

kuwa malundo ya mawe.

2737:27 Isa 15:6; Za 129:6Watu wa miji hiyo wameishiwa nguvu,

wanavunjika mioyo na kuaibishwa.

Wao ni kama mimea katika shamba,

kama machipukizi mororo ya kijani,

kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba,

ambayo hukauka kabla ya kukua.

2837:28 Za 139:1-3; 2:1“Lakini ninajua mahali ukaapo,

kutoka kwako na kuingia kwako,

na jinsi unavyoghadhibika dhidi yangu.

2937:29 Isa 10:12; Ay 41:2; 40:24; Eze 38:4; Amo 4:2; 2Nya 33:11Kwa sababu unaghadhibika na ufidhuli dhidi yangu,

na kwa sababu ufidhuli wako umefika masikioni mwangu,

nitaweka ndoana yangu puani mwako

na hatamu yangu kinywani mwako,

nami nitakufanya urudi kwa njia ile uliyoijia.

3037:30 Isa 20:3; 32:10; 16:14; Law 25:4; Yer 31:5; Za 107:37“Hii ndiyo itakuwa ishara kwako, ee Hezekia:

“Mwaka huu utakula kile kiotacho chenyewe,

na mwaka wa pili utakula kutoka machipukizi yake.

Lakini katika mwaka wa tatu panda na uvune,

panda mashamba ya mizabibu na ule matunda yake.

3137:31 Isa 27:6; 11:10Mara nyingine tena mabaki ya nyumba ya Yuda

wataeneza mizizi chini na kuzaa matunda juu.

3237:32 Isa 11:11; 1:9; 9:7Kwa kuwa kutoka Yerusalemu watakuja mabaki,

na kutoka Mlima Sayuni kundi la walionusurika.

Wivu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote,

ndio utatimiza jambo hili.

3337:33 Isa 32:18; 2Sam 20:15“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu mfalme wa Ashuru:

“Hataingia katika mji huu

wala hatapiga mshale hapa.

Hatakuja mbele yake na ngao

wala kupanga majeshi kuuzingira.

3437:34 Isa 37:29Kwa njia ile aliyoijia ndiyo atakayorudi;

hataingia katika mji huu,”

asema Bwana.

3537:35 Isa 31:5; 38:6; Eze 48:9-11; 36:21-22; 2Fal 20:6; 1Nya 17:19“Nitaulinda mji huu na kuuokoa,

kwa ajili yangu mwenyewe,

na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu!”

3637:36 Kut 12:12, 23; Isa 10:12Ndipo malaika wa Bwana akaenda, akawaua wanajeshi 185,000 katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali! 3737:37 Mwa 10:11; Nah 1:1; 2Nya 32:1Basi Senakeribu mfalme wa Ashuru akavunja kambi na kuondoka. Akarudi Ninawi na kukaa huko.

3837:38 Mwa 8:4; Yer 51:27; 2Fal 17:24; Isa 14:25; 9:4; 10:26Siku moja, alipokuwa akiabudu katika hekalu la mungu wake Nisroki, wanawe Adrameleki na Shareza wakamuua kwa upanga, nao wakakimbilia nchi ya Ararati. Naye Esar-Hadoni mwanawe akawa mfalme badala yake.