Furaha Ya Waliokombolewa
135:1 Isa 27:10; 41:18-19; 51:3; 32:15-16; 27:6Jangwa na nchi kame vitafurahi;
nyika itashangilia na kuchanua maua.
Kama waridi, 235:2 Wim 7:5; Mwa 21:6; Ezr 3:7; Za 105:43; Isa 32:15; 12:6; 25:9; 1Nya 27:29litachanua maua,
litashangilia sana na kupaza sauti kwa furaha.
Litapewa utukufu wa Lebanoni,
fahari ya Karmeli na Sharoni;
wataona utukufu wa Bwana,
fahari ya Mungu wetu.
335:3 Ay 4:3-4; Ebr 12:12Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu,
yafanyeni imara magoti yaliyolegea,
435:4 Isa 40:2; 2Nya 32:6; Zek 1:13; Kum 20:3; Isa 21:4; Yos 1:9; Isa 7:4; 1:24; 34:8; 25:9; 40:1; 10:9, 10-11; 51:5; 62:11; Dan 10:19; Ufu 22:12waambieni wale wenye mioyo ya hofu,
“Kuweni hodari, msiogope;
tazama, Mungu wenu atakuja,
pamoja na malipo ya Mungu,
atakuja na kuwaokoa ninyi.”
535:5 Mt 9:27; 11:5; Isa 42:18; 29:18; 2Nya 32:6; Isa 40:2; Zek 1:13; Isa 21:4; Ufu 22:12Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa
na masikio ya viziwi yatazibuliwa.
635:6 Lk 7:22; Yn 5:8-9; Mk 7:35; Kut 17:6; Yn 7:38; Mdo 3:2; Mt 15:30; Mdo 3:8Ndipo kilema atarukaruka kama kulungu,
nao ulimi wa aliye bubu utapaza sauti kwa shangwe.
Maji yatatiririka kwa kasi katika nyika,
na vijito katika jangwa.
735:7 Za 68:6; Isa 41:17; 44:3; 55:1; 49:10; 58:11; 13:22; Za 107:35; Ay 8:11; 40:21Mchanga wa moto utakuwa bwawa la maji,
ardhi yenye kiu itabubujika chemchemi.
Maskani ya mbweha walikolala hapo awali
patamea majani, matete na mafunjo.
835:8 Yer 31:21; Yoe 3:17; Mt 7:13-14; 1Pet 1:15; Isa 52:1; 33:8Nako kutakuwa na njia kuu,
nayo itaitwa Njia ya Utakatifu.
Wasio safi hawatapita juu yake;
itakuwa ya wale watembeao katika Njia ile;
yeye asafiriye juu yake,
ajapokuwa mjinga, hatapotea.
935:9 Isa 30:9; 11:6-9; Law 25:47-55; Kut 6:6; Isa 13:22; 62:12Huko hakutakuwepo na simba,
wala mnyama mkali hatapita njia hiyo,
wala hawatapatikana humo.
Ila waliokombolewa tu ndio watakaopita huko,
1035:10 Yn 16:22; Isa 51:11; 30:29; Ufu 21:4; Ay 19:25; Za 51:8waliokombolewa na Bwana watarudi.
Wataingia Sayuni wakiimba;
furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao.
Watapata furaha na shangwe;
huzuni na majonzi vitakimbia.