Isaya 34 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 34:1-17

Hukumu Dhidi Ya Mataifa

134:1 Isa 43:9; Kum 4:26; 32:1; Za 24:1; Isa 33:13Njooni karibu, enyi mataifa, nanyi msikilize;

sikilizeni kwa makini,

enyi kabila za watu!

Dunia na isikie, navyo vyote vilivyo ndani yake,

ulimwengu na vyote vitokavyo ndani yake!

234:2 Isa 13:5; Zek 5:3; Isa 10:25; 30:25Bwana ameyakasirikia mataifa yote;

ghadhabu yake ni juu ya majeshi yao yote.

Atawaangamiza kabisa,

atawatia mikononi mwa wachinjaji.

334:3 Yoe 2:20; Amo 4:10; Eze 38:22; Isa 5:25; Za 110:6; Eze 5:17; 14:19Waliouawa watatupwa nje,

maiti zao zitatoa uvundo,

milima itatota kwa damu zao.

434:4 2Pet 3:10; Yoe 2:31; Eze 32:7-8; Ay 9:7; Ufu 6:13; Isa 13:13; Mt 24:29; Ay 8:12; Mk 13:15; Isa 15:6; Ebr 1:12Nyota zote za mbinguni zitayeyuka

na anga litasokotwa kama kitabu,

jeshi lote la angani litaanguka

kama majani yaliyonyauka kutoka kwenye mzabibu,

kama tini iliyonyauka kutoka kwenye mtini.

534:5 Yer 49:7; 46:10; Zek 13:7; 2Sam 8:13-14; Yos 6:17; Kum 32:41-42; Amo 3:14-15; Yer 47:6; Eze 21:5; 2Nya 28:17; Amo 1:11-12; 6:11; Mal 1:4Upanga wangu umekunywa na kushiba huko mbinguni,

tazama, unashuka katika hukumu juu ya Edomu,

wale watu ambao nimeshawahukumu,

kuwaangamiza kabisa.

634:6 Kum 32:41; Law 3:9; Mwa 36:33; Isa 30:25; Yer 25:34; Ufu 19:17Upanga wa Bwana umeoga katika damu,

umefunikwa na mafuta ya nyama:

damu ya kondoo na mbuzi,

mafuta kutoka figo za kondoo dume.

Kwa maana Bwana ana dhabihu huko Bosra,

na machinjo makuu huko Edomu.

734:7 Hes 23:22; Za 68:30; 2Sam 1:22Nyati wataanguka pamoja nao,

ndama waume na mafahali wakubwa.

Nchi yao italowana kwa damu,

nayo mavumbi yataloa mafuta ya nyama.

834:8 Isa 2:12; 1:24; 59:18; Yoe 3:4; Eze 25:12-17; Amo 1:6-10Kwa sababu Bwana anayo siku ya kulipiza kisasi,

mwaka wa malipo,

siku ya kushindania shauri la Sayuni.

934:9 Mwa 19:24Vijito vya Edomu vitageuka kuwa lami,

mavumbi yake yatakuwa kiberiti kiunguzacho,

nchi yake itakuwa lami iwakayo!

1034:10 Ufu 14:10-11; 19:3; Yer 49:18; Mal 1:3; Isa 13:20; Eze 29:12; 35:3Haitazimishwa usiku wala mchana,

moshi wake utapaa juu milele.

Kutoka kizazi hadi kizazi itakuwa ukiwa,

hakuna mtu yeyote atakayepita huko tena.

1134:11 Law 11:16-18; Ufu 18:2; Mao 2:8; Amo 7:8; Kum 14:15-17; Yoe 3:19; 2Fal 21:13Bundi wa jangwani na bundi mwenye sauti nyembamba wataimiliki,

bundi wakubwa na kunguru wataweka viota humo.

Mungu atanyoosha juu ya Edomu

kamba ya kupimia ya machafuko matupu,

na timazi ya ukiwa.

1234:12 Isa 41:11-12; Za 107:10; Ay 12:21; Isa 40:23; Eze 24:5; Yer 39:6Watu wake wa kuheshimiwa hawatakuwa na chochote

kitakachoitwa ufalme huko,

nao wakuu wao wote watatoweka.

1334:13 Hos 9:6; Isa 32:13; 13:22; Yer 9:11; Isa 7:19; Za 44:19Miiba itaenea katika ngome za ndani,

viwawi na michongoma itaota

kwenye ngome zake.

Itakuwa maskani ya mbweha,

makao ya bundi.

1434:14 Za 74:14; Isa 13:22; Ufu 18:2Viumbe vya jangwani vitakutana na fisi,

nao mbuzi-mwitu watalia wakiitana;

huko viumbe vya usiku vitastarehe pia

na kujitafutia mahali pa kupumzika.

1534:15 Za 17:8; Kum 14:13Bundi wataweka viota huko na kutaga mayai,

atayaangua na kutunza makinda yake

chini ya uvuli wa mabawa yake;

pia huko vipanga watakusanyika,

kila mmoja na mwenzi wake.

1634:16 Isa 30:8; Dan 7:10; Isa 1:20; 58:14; 48:13Angalieni katika gombo la Bwana na msome:

Hakuna hata mmoja katika hawa atakayekosekana,

hakuna hata mmoja atakayemkosa mwenzi wake.

Kwa kuwa ni kinywa chake Mungu kimeagiza,

na Roho wake atawakusanya pamoja.

1734:17 Za 78:55; Isa 17:14; Yer 13:25Huwagawia sehemu zao,

mkono wake huwagawanyia kwa kipimo.

Wataimiliki hata milele

na kuishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.