Isaya 32 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 32:1-20

Ufalme Wa Haki

132:1 2Nya 31:20; Eze 37:24; Za 72:1-4; Yer 23:5; Isa 28:6; Za 149:2; Isa 6:5Tazama, mfalme atatawala kwa uadilifu

na watawala watatawala kwa haki.

232:2 1Fal 18:4; Isa 4:6; Za 55:8; 23:2; Isa 49:10; Yer 31:9; Za 107:35Kila mtu atakuwa kama kivuli cha kujificha kutokana na upepo

na kimbilio kutokana na dhoruba,

kama vijito vya maji jangwani

na kivuli cha mwamba mkubwa katika ardhi yenye kiu.

332:3 Isa 29:18; 42:7, 16; Kum 29:4Ndipo macho ya wale wanaoona hayatafumbwa tena,

nayo masikio ya wale wanaosikia yatasikiliza.

432:4 Isa 6:10; 29:24; 35:6Moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu na kuelewa,

nao ulimi wenye kigugumizi utanena kwa ufasaha.

532:5 1Sam 25:25Mpumbavu hataitwa tena muungwana,

wala mtu mbaya kabisa kupewa heshima ya juu.

632:6 Isa 3:15; Mit 19:3; Isa 9:16-17; Mit 24:2; Isa 26:10Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu,

moyo wake hushughulika na uovu:

Hutenda mambo yasiyo ya kumcha Mungu,

na hueneza habari za makosa kuhusu Bwana;

yeye huwaacha wenye njaa bila kitu,

na wenye kiu huwanyima maji.

732:7 Yer 5:26-28; Dan 12:10; Mik 7:3; Isa 29:19-20; Za 72:4; Isa 29:21Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu,

hufanya mipango miovu

ili kumwangamiza maskini kwa uongo,

hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki.

832:8 1Nya 29:9; Mit 11:25; Isa 14:24Lakini mtu muungwana hufanya mipango ya kiungwana,

na kwa matendo ya kiungwana yeye hufanikiwa.

Wanawake Wa Yerusalemu

932:9 Isa 28:23; Dan 4:4; Amo 6:1; Sef 2:15Enyi wanawake wenye kuridhika sana,

amkeni na mnisikilize.

Enyi binti mnaojisikia kuwa salama,

sikieni lile ninalotaka kuwaambia!

1032:10 Isa 5:5-6; 24:7; 37:30Muda zaidi kidogo ya mwaka mmoja,

ninyi mnaojisikia salama mtatetemeka,

mavuno ya zabibu yatakoma

na mavuno ya matunda hayatakuwepo.

1132:11 Nah 3:5; Mik 1:8; Isa 34:14; 47:2; 3:24Tetemekeni, enyi wanawake wenye kuridhika,

tetemekeni kwa hofu, enyi binti mnaojisikia salama!

Vueni nguo zenu,

vaeni nguo ya gunia viunoni mwenu.

1232:12 Nah 2:7; Isa 16:9Pigeni matiti yenu kwa ajili ya mashamba mazuri,

kwa ajili ya mizabibu iliyozaa vizuri

1332:13 Hos 9:6; 10:8; Isa 23:7; 24:11na kwa ajili ya nchi ya watu wangu,

nchi ambayo miiba na michongoma imemea:

naam, ombolezeni kwa ajili ya nyumba zote za furaha

na kwa ajili ya mji huu wenye kufanya sherehe.

1432:14 Isa 13:22; 27:10; 2:15; 34:13; 6:11; 5:17; Za 104:11Ngome itaachwa,

mji wenye kelele nyingi utahamwa,

ngome ndani ya mji na mnara wa ulinzi vitakuwa ukiwa milele,

mahali pazuri pa punda na malisho ya makundi ya kondoo,

1532:15 Yoe 2:28; Eze 37:9; Za 107:35; Isa 29:17; 11:2mpaka Roho amwagwe juu yetu kutoka juu,

nalo jangwa kuwa shamba lenye rutuba,

na shamba lenye rutuba kuwa kama msitu.

1632:16 Isa 9:7; 28:6; 35:1, 6; 42:11; Za 48:1; Isa 1:26Haki itakaa katika jangwa,

na uadilifu utakaa katika shamba lenye rutuba.

1732:17 Za 85:10; 119:165; Rum 14:17; Ebr 12:11Matunda ya haki yatakuwa amani,

matokeo ya haki yatakuwa utulivu

na matumaini milele.

1832:18 Yos 1:13; 11:18; Hos 2:18-23; Amo 9:14Watu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani,

katika nyumba zilizo salama,

katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu.

1932:19 Isa 19:18; 24:10; 28:17; 30:30; Zek 11:2; Ay 40:11Hata kama mvua ya mawe iangushe msitu

na mji ubomolewe kabisa,

2032:20 Mhu 11:1; Isa 30:24; Ay 39:8; Kum 28:12tazama jinsi utakavyobarikiwa,

ukipanda mbegu yako katika kila kijito,

na kuwaacha ngʼombe wako

na punda wajilishe kwa uhuru.