Isaya 31 – NEN & NIVUK

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 31:1-9

Ole Wa Wale Wanaotegemea Misri

131:1 Eze 17:15; Kum 17:16; 20:1; Yer 37:5; Dan 9:13; Hos 11:8; Isa 30:2-5; Ay 6:10Ole wao wale washukao Misri kwa ajili ya msaada,

wale wategemeao farasi,

wanaoweka tumaini katika wingi wa magari yao ya vita,

na katika nguvu nyingi za wapanda farasi,

lakini hawamwangalii yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,

wala hawatafuti msaada kwa Bwana.

231:2 Za 92:5; Rum 16:27; Hes 23:19; Mit 19:21; Isa 29:15; Amo 3:6; Isa 29:19; 32:6Hata hivyo yeye pia ana hekima na anaweza kuleta maafa,

wala hayatangui maneno yake.

Yeye atainuka dhidi ya nyumba ya mwovu,

dhidi ya wale ambao huwasaidia watenda mabaya.

331:3 Eze 28:9; Isa 20:5; Za 9:20; 2The 2:4; Ay 30:21; Yer 51:25; Isa 30:5-7; Neh 1:10Lakini Wamisri ni wanadamu, wala si Mungu,

farasi wao ni nyama, wala si roho.

Wakati Bwana atakaponyoosha Mkono wake,

yeye anayesaidia atajikwaa,

naye anayesaidiwa ataanguka,

wote wawili wataangamia pamoja.

431:4 Nah 3:18; Ay 30:21; Isa 30:5-7; Hes 24:9; 1Sam 17:34; Eze 34:23; Isa 42:13; Hos 11:10Hili ndilo Bwana analoniambia:

“Kama vile simba angurumavyo,

simba mkubwa juu ya mawindo yake:

hata ingawa kundi lote la wachunga mifugo

huitwa pamoja dhidi yake,

hatiwi hofu na kelele zao

wala kusumbuliwa na ghasia zao;

ndivyo Bwana Mwenye Nguvu Zote atakavyoshuka

kufanya vita juu ya Mlima Sayuni

na juu ya vilele vyake.

531:5 Za 91:4; Kum 32:11; Zek 9:15; Za 34:7; Mt 23:37; Kut 12:23Kama ndege warukao,

Bwana Mwenye Nguvu Zote ataukinga Yerusalemu;

ataukinga na kuuokoa,

atapita juu yake na kuufanya salama.”

631:6 Ay 22:23; Isa 1:5, 27Mrudieni yeye ambaye nyumba ya Israeli imemwasi sana. 731:7 Isa 2:20; 30:22; 1Fal 12:30; Za 135:5Kwa kuwa katika siku ile kila mmoja wenu atazikataa sanamu za fedha na za dhahabu zilizotengenezwa kwa mikono yenu yenye dhambi.

831:8 Isa 10:12; Kut 12:12; Hab 2:8; Mwa 49:15; Isa 14:25; Yer 25:12; Kum 20:11“Ashuru itaanguka kwa upanga ambao si wa mwanadamu;

upanga usio wa kibinadamu utawaangamiza.

Watakimbia mbele ya upanga

na vijana wao wa kiume watafanyizwa kazi kwa lazima.

931:9 Kum 32:31-37; Isa 10:17; Law 6:13; Isa 18:3; Yer 4:6; 51:9; Za 21:9Ngome zao zitaanguka kwa sababu ya hofu;

kwa kuona bendera ya vita,

majemadari wao watashikwa na hofu ya ghafula,”

asema Bwana,

ambaye moto wake uko Sayuni,

nayo tanuru yake iko Yerusalemu.

New International Version – UK

Isaiah 31:1-9

Woe to those who rely on Egypt

1Woe to those who go down to Egypt for help,

who rely on horses,

who trust in the multitude of their chariots

and in the great strength of their horsemen,

but do not look to the Holy One of Israel,

or seek help from the Lord.

2Yet he too is wise and can bring disaster;

he does not take back his words.

He will rise up against that wicked nation,

against those who help evildoers.

3But the Egyptians are mere mortals and not God;

their horses are flesh and not spirit.

When the Lord stretches out his hand,

those who help will stumble,

those who are helped will fall;

all will perish together.

4This is what the Lord says to me:

‘As a lion growls,

a great lion over its prey –

and though a whole band of shepherds

is called together against it,

it is not frightened by their shouts

or disturbed by their clamour –

so the Lord Almighty will come down

to do battle on Mount Zion and on its heights.

5Like birds hovering overhead,

the Lord Almighty will shield Jerusalem;

he will shield it and deliver it,

he will “pass over” it and will rescue it.’

6Return, you Israelites, to the One you have so greatly revolted against. 7For in that day every one of you will reject the idols of silver and gold your sinful hands have made.

8‘Assyria will fall by no human sword;

a sword, not of mortals, will devour them.

They will flee before the sword

and their young men will be put to forced labour.

9Their stronghold will fall because of terror;

at the sight of the battle standard their commanders will panic,’

declares the Lord,

whose fire is in Zion,

whose furnace is in Jerusalem.