Isaya 29 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 29:1-24

Ole Wa Mji Wa Daudi

129:1 Isa 22:12-13; 1:14; 2Sam 5:7; Isa 28:1Ole wako, wewe Arieli, Arieli,

mji alimokaa Daudi!

Ongezeni mwaka kwa mwaka,

na mzunguko wa sikukuu zenu uendelee.

229:2 Mao 2:5; Isa 3:26; Eze 43:15Hata hivyo nitauzunguka Arieli kwa jeshi,

utalia na kuomboleza,

utakuwa kwangu kama mahali

pa kuwashia moto madhabahuni.

329:3 Lk 19:43-44; 2Fal 25:1Nitapiga kambi pande zote dhidi yako,

nitakuzunguka kwa minara

na kupanga mazingirwa yangu dhidi yako.

429:4 Isa 8:19; 47:1; 52:2; 26:16; Law 19:31Utakaposhushwa, utanena kutoka ardhini,

utamumunya maneno yako kutoka mavumbini.

Sauti yako itatoka katika nchi kama vile ya mzimu,

utanongʼona maneno yako toka mavumbini.

529:5 Isa 17:13; 1The 5:3; Za 55:15; Kum 9:21; Za 78:39; Isa 51:12; Za 103:15Lakini adui zako wengi watakuwa kama vumbi laini,

kundi la wakatili watakuwa

kama makapi yapeperushwayo.

Naam, ghafula, mara moja,

629:6 Mk 13:8; Ufu 6:12; Isa 26:21; Zek 14:1-5; Kut 19:16; Mt 24:7; Za 83:13-15Bwana Mwenye Nguvu Zote atakuja

na ngurumo, tetemeko la ardhi, na kwa sauti kuu,

atakuja na dhoruba, tufani na miali ya moto iteketezayo.

729:7 Mik 4:11-12; Zek 12:9; Ay 20:8Kisha makundi ya mataifa yote yale yapiganayo dhidi ya Arieli,

yale yanayomshambulia yeye na ngome zake, na kumzunguka kwa jeshi,

watakuwa kama ilivyo ndoto,

kama maono wakati wa usiku:

829:8 Za 73:20; Yer 30:16; Isa 17:12-14; Zek 12:3; Isa 54:17kama vile mtu aliye na njaa aotavyo kuwa anakula,

lakini huamka, bado njaa yake ingalipo,

kama vile mtu mwenye kiu aotavyo kuwa anakunywa maji,

lakini huamka akiwa anazimia, akiwa bado angali ana kiu.

Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa makundi yote ya mataifa

yanayopigana dhidi ya Mlima Sayuni.

929:9 Yer 13:13; Isa 63:9; Law 10:9; Yer 4:9; Isa 6:10; 63:6; Za 60:3; Yer 13:13; Isa 51:22Duwaeni na kushangaa,

jifanyeni vipofu wenyewe na msione,

leweni, lakini si kwa mvinyo,

pepesukeni lakini si kwa kileo.

1029:10 2The 2:9-11; Za 69:23; Mik 3:6; Amu 4:21; Isa 44:18; 6:9-10; Rum 11:8Bwana amewaleteeni usingizi mzito:

Ameziba macho yenu (ninyi manabii);

amefunika vichwa vyenu (ninyi waonaji).

1129:11 Dan 8:26; Mt 13:11; Isa 28:7; Ufu 5:1-2; Isa 8:16; Dan 12:9Kwa maana kwenu ninyi, maono haya yote si kitu ila maneno yaliyotiwa lakiri katika kitabu. Kama mkimpa mtu yeyote awezaye kusoma kitabu hiki, nanyi mkamwambia, “Tafadhali kisome,” yeye atajibu, “Mimi siwezi, kwa kuwa kimetiwa lakiri.” 12Au kama mkimpa mtu yeyote kitabu hiki asiyeweza kusoma na kumwambia, “Tafadhali kisome,” atajibu, “Mimi sijui kusoma.”

1329:13 Yer 12:2; Kol 2:22; Eze 33:31; Mt 15:8-9; Mk 7:6-7; Isa 58:2; Za 119:70; Yer 14:11Bwana anasema:

“Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao

na kuniheshimu kwa midomo yao,

lakini mioyo yao iko mbali nami.

Ibada yao kwangu inatokana na maagizo

waliyofundishwa na wanadamu.

1429:14 Yer 49:7; Ay 10:16; 5:13; Isa 6:9-10; 1Kor 1:19; Yer 8:9; Isa 6:9-10Kwa hiyo mara nyingine tena nitawashangaza watu hawa,

kwa ajabu juu ya ajabu.

Hekima ya wenye hekima itapotea,

nayo akili ya wenye akili itatoweka.”

1529:15 Ay 22:13-14; Eze 8:12; 2Fal 21:16; Ay 22:13; Isa 28:15; Ay 8:3; Za 10:11-13Ole kwa wale wanaokwenda kwenye vilindi virefu

kumficha Bwana mipango yao,

wafanyao kazi zao gizani na kufikiri,

“Ni nani anayetuona? Ni nani atakayejua?”

1629:16 Yer 18:6; Rum 9:20-21; Za 94:9; Ay 10:9; Isa 10:15; 45:9; Ay 9:12; Yer 18:6; Mwa 2:7Mnapindua mambo juu chini,

kana kwamba mfinyanzi aweza kufikiriwa kuwa kama udongo wa mfinyanzi!

Je, kile kilichofinyangwa chaweza kumwambia yule aliyekifinyanga,

“Wewe hukunifinyanga mimi?”

Je, chungu kinaweza kumwambia mfinyanzi,

“Wewe hujui chochote?”

1729:17 Za 84:6; Isa 32:15; 10:25; 2:13; Za 107:33Kwa muda mfupi sana, je, Lebanoni haitageuzwa kuwa shamba lenye rutuba,

na shamba lenye rutuba liwe kama msitu?

1829:18 Mk 7:37; Za 146:8; Mt 11:5; Lk 7:22; Isa 32:3; Za 107:14Katika siku ile viziwi watasikia maneno ya kitabu,

na katika utusitusi na giza

macho ya kipofu yataona.

1929:19 Za 72:4; 25:9; Isa 5:19; 12:6; 3:15; Yak 2:5; Mt 5:5; 11:29; Mwa 42:26Mara nyingine tena wanyenyekevu watafurahi katika Bwana,

wahitaji watafurahi katika yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

2029:20 2Nya 36:16; Isa 28:22; Eze 11:2; Isa 13:11; 59:4; Ay 15:35; Za 7:14Wakatili watatoweka na wenye kudhihaki watatokomea,

nao wote wenye jicho la uovu watakatiliwa mbali,

2129:21 Amo 5:10-15; Isa 5:23; Hab 1:4; Mit 21:28wale ambao kwa neno humfanya mtu kuwa mwenye hatia,

wamtegeao mtego mtetezi katika mahakama,

na kwa ushuhuda wa uongo humnyima haki

yeye asiye na hatia.

2229:22 Mwa 11:16; Yoe 2:26; Yos 24:3; Sef 3:11; Kut 6:6; Mwa 17:16; Isa 41:8; 51:2Kwa hiyo hili ndilo Bwana, aliyemkomboa Abrahamu, analosema kwa nyumba ya Yakobo:

“Yakobo hataaibishwa tena,

wala nyuso zao hazitabadilika sura tena.

2329:23 Isa 53:10; 54:1-4; 19:25; 49:20-26; 5:19; Mt 6:9Wakati watakapoona watoto wao miongoni mwao,

kazi ya mikono yangu,

watalitakasa Jina langu takatifu;

wataukubali utakatifu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Yakobo,

nao watamcha Mungu wa Israeli.

2429:24 Mit 12:8; Ebr 5:2; Isa 60:16; 42:16; Za 95:10; Isa 28:7; 32:4Wale wanaopotoka rohoni watapata ufahamu,

nao wale wanaolalamika watayakubali mafundisho.”

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以赛亚书 29:1-24

耶路撒冷被围

1耶和华说:“亚利伊勒29:1 “亚利伊勒”在此处用来指锡安/耶路撒冷,2节、7节同。亚利伊勒

大卫安营的城啊!

你有祸了!

尽管你年复一年地守节期,

2我终必叫你受苦。

你必悲伤哀号,

在我面前成为一座祭坛。

3我必安营把你团团围住,

屯兵围困你,

修筑高台攻打你。

4你必一败涂地,

躺在尘土中说话,

你细微的声音从土中传来,

好像地下幽灵的声音。

你必从尘埃中喃喃细语。

5但你的众仇敌必像纤细的尘埃一样消散,

众多的残暴之徒必如被风刮去的糠秕。

突然,刹那之间,

6万军之耶和华必带着雷轰、地震、巨响、旋风、暴风和烈火来临。

7攻打、围困亚利伊勒及其堡垒的各国军队必如梦幻,

如夜间的异象一样消失。

8他们好像饥饿的人梦中吃饭,

醒来仍然饥饿;

像口渴的人梦中喝水,

醒来仍然渴得发昏。

攻打锡安山的各国军队都必如此。”

9你们驻足惊奇吧!

你们自我蒙蔽,继续瞎眼吧!

你们醉了,但不是因为酒;

你们东倒西歪,但不是因为烈酒。

10因为耶和华把沉睡的灵倾倒在你们身上,

祂封住你们的眼睛,

盖住你们的头。

你们的眼睛就是先知,

你们的头就是先见。

11对你们而言,这整个启示都好像封了印的书卷。你们把书卷交给识字的人读,他会说:“我不能读,这书卷是封着的。” 12你们把书卷交给不识字的人读,他会说:“我不识字。”

13主说:“这些人嘴上亲近我,

他们用嘴唇尊崇我,心却远离我。

他们敬拜我不过是遵行人定的规条。

14所以,我要再次行奇妙无比的事,使他们震惊。

他们智者的智慧必泯灭,

明哲的聪明必消失。”

15那些向耶和华深藏计谋的人有祸了!

他们暗中行事,

自以为谁也无从看见和知晓。

16他们颠倒是非!

窑匠岂可被看作泥土?

受造者岂可对创造者说

“你没有造我”?

陶器怎能对陶匠说:

“你什么也不懂”?

17再过不久,黎巴嫩将变成沃野,

沃野上庄稼将茂密如林。

18那时,耳聋的必听见那书卷上的话,

盲人的眼睛必能看穿黑暗。

19卑微的人必因耶和华而欢喜,

贫穷的人必因以色列的圣者而快乐。

20残暴之徒必消失,

嘲讽者必绝迹,

所有伺机作恶者必被铲除。

21他们恶言诬陷人,

暗算城门口的审判官,

用谎言冤枉无辜。

22因此,关于雅各家,

救赎亚伯拉罕的耶和华说:

雅各的子孙必不再羞愧,

脸上再无惧色。

23因为他们看见我赐给他们的子孙时,

必尊我的名为圣,

必尊雅各的圣者为圣,

必敬畏以色列的上帝。

24心里迷惘的必明白真理,

发怨言的必欣然受教。”