Isaya 26 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 26:1-21

Wimbo Wa Ushindi

126:1 Isa 14:32; Zek 2:5; Isa 10:20; 30:29; 32:18; Zek 9:8; Za 48:13Katika siku ile, wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda:

Tuna mji ulio na nguvu,

Mungu huufanya wokovu kuwa kuta zake na maboma yake.

226:2 Isa 58:8; 62:2; Ufu 21:13; Za 24:4-7; 83:13; Isa 1:26; 50:8Fungua malango ili taifa lenye haki lipate kuingia,

taifa lile lidumishalo imani.

326:3 Ay 22:21; Flp 4:7; Isa 9:6-7; 1Nya 5:20; Za 28:7; 22:5Utamlinda katika amani kamilifu

yeye ambaye moyo wake ni thabiti

kwa sababu anakutumaini wewe.

426:4 Isa 12:2; 50:10; Za 62:8; Mwa 49:24Mtumaini Bwana milele,

kwa kuwa Bwana, Bwana, ni Mwamba wa milele.

526:5 Isa 25:12; 25:5; Eze 26:11Huwashusha wale wajikwezao,

huushusha chini mji wenye kiburi,

huushusha hadi ardhini

na kuutupa chini mavumbini.

626:6 Isa 5:5; 49:26; 3:15; 14:30Miguu huukanyaga chini,

miguu ya hao walioonewa,

hatua za hao maskini.

726:7 Kum 32:4; Kut 14:19; Isa 42:16; Za 26:12; 25:8; Isa 40:4Mapito ya wenye haki yamenyooka.

Ewe uliye Mwenye Haki,

waisawazisha njia ya mtu mnyofu.

826:8 Za 18:22; 145:2; Isa 12:4; Kum 18:18; Isa 65:5; Za 37:9Naam, Bwana, tukienenda katika sheria zako,

twakungojea wewe,

jina lako na sifa zako

ndizo shauku za mioyo yetu.

926:9 Za 42:1-2; Mt 6:33; Za 63:6; 119:55; 1Nya 16:14; Za 78:34Nafsi yangu yakutamani wakati wa usiku,

wakati wa asubuhi roho yangu yakuonea shauku.

Wakati hukumu zako zinapokuja juu ya dunia,

watu wa ulimwengu hujifunza haki.

1026:10 Isa 32:6; 1Sam 12:24; Rum 2:4; Mhu 8:12; Mt 5:45; Isa 22:12-13; Yer 2:19; Yn 5:38Ingawa neema yaonyeshwa kwa waovu,

hawajifunzi haki,

hata katika nchi ya unyofu huendelea kutenda mabaya

wala hawazingatii utukufu wa Bwana.

1126:11 Ay 34:27; Isa 18:3; 44:9, 18; Ebr 10:27; Za 10:12; Yoe 2:18; Zek 1:14; Mik 7:16Ee Bwana, mkono wako umeinuliwa juu,

lakini hawauoni.

Wao na waone wivu wako kwa ajili ya watu wako tena waaibishwe,

moto uliowekwa akiba kwa ajili ya adui zako na uwateketeze.

1226:12 Za 119:165; Isa 9:6; Za 68:28Bwana, unaamuru amani kwa ajili yetu,

yale yote tuliyoweza kuyakamilisha ni wewe uliyetenda kwa ajili yetu.

1326:13 Za 66:12; Isa 42:8; 2:8; 63:7Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametutawala,

lakini jina lako pekee ndilo tunaloliheshimu.

1426:14 Kum 4:28; Za 9:5; Isa 10:3; Ay 28:5Wao sasa wamekufa, wala hawako tena hai,

roho za waliokufa hazitarudi tena.

Uliwaadhibu na kuwaangamiza,

umefuta kumbukumbu lao lote.

1526:15 Isa 33:17; 14:2; Ay 12:23Umeliongeza hilo taifa, Ee Bwana,

umeliongeza hilo taifa.

Umejipatia utukufu kwa ajili yako mwenyewe,

umepanua mipaka yote ya nchi.

1626:16 Amu 6:2; Hos 5:15; Isa 5:30; Za 39:11; Isa 29:4Bwana, walikujia katika taabu yao,

wewe ulipowarudi,

waliweza kuomba kwa kunongʼona tu.

1726:17 Isa 21:3; Ufu 12:2; Yn 16:21Kama mwanamke mwenye mimba aliyekaribia kuzaa

anavyogaagaa na kulia kwa ajili ya maumivu yake,

ndivyo tulivyokuwa mbele zako, Ee Bwana.

1826:18 Isa 59:4; Mwa 49:10; Za 17:14; Isa 42:6; 49:6; 51:4; Yer 12:16Tulikuwa na mimba, tuligaagaa kwa maumivu,

lakini tulizaa upepo.

Hatukuleta wokovu duniani,

hatujazaa watu katika ulimwengu huu.

1926:19 Hos 13:14; Efe 5:14; Isa 25:8; Eze 37:1-14; Dan 12:2; Isa 18:4; Mwa 27:28; Za 22:29Lakini wafu wenu wataishi,

nayo miili yao itafufuka.

Ninyi mnaokaa katika mavumbi,

amkeni mkapige kelele kwa furaha.

Umande wenu ni kama umande wa asubuhi,

dunia itawazaa wafu wake.

2026:20 Kut 12:23; Za 30:5; Ay 14:13; 2Kor 4:17; Isa 10:25; 30:27Nendeni, watu wangu, ingieni vyumbani mwenu

na mfunge milango nyuma yenu,

jificheni kwa kitambo kidogo

mpaka ghadhabu yake ipite.

2126:21 Yud 14; Mik 1:3; Ay 16:18; Isa 29:6; 18:4; Lk 11:50-51; Isa 30:12-14Tazama, Bwana anakuja kutoka makao yake

ili kuwaadhibu watu wa dunia kwa ajili ya dhambi zao.

Dunia itadhihirisha umwagaji damu juu yake,

wala haitaendelea kuwaficha watu wake waliouawa.