Isaya 25 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 25:1-12

Msifuni Bwana

125:1 Hes 23:19; Za 40:5; Yoe 2:21-26; Isa 7:13; 14:24; 37:26; Efe 1:11Ee Bwana, wewe ni Mungu wangu,

nitakutukuza na kulisifu jina lako,

kwa maana katika ukamilifu wa uaminifu

umetenda mambo ya ajabu,

mambo yaliyokusudiwa tangu zamani.

225:2 Isa 37:26; Yer 51:37; Isa 17:3; 13:22; Kum 13:16; Ay 12:14Umeufanya mji kuwa lundo la kifusi,

mji wenye ngome kuwa magofu,

ngome imara ya wageni kuwa si mji tena,

wala hautajengwa tena kamwe.

325:3 Kut 6:2; Za 22:23; Isa 11:14; 13:11; Ufu 11:13Kwa hiyo mataifa yenye nguvu yatakuheshimu,

miji ya mataifa katili itakuheshimu wewe.

425:4 Yoe 3:16; Isa 33:16; Za 46:1-11; Isa 49:25; 2Sam 22:3; Za 118:8; Isa 3:14Umekuwa kimbilio la watu maskini,

kimbilio la mhitaji katika taabu yake,

hifadhi wakati wa dhoruba

na kivuli wakati wa hari.

Kwa maana pumzi ya wakatili

ni kama dhoruba ipigayo ukuta

525:5 Yer 51:25; Za 18:44; Isa 13:11na kama joto la jangwani.

Wewe wanyamazisha makelele ya wageni;

kama vile hari ipunguzwavyo na kivuli cha wingu,

ndivyo wimbo wa wakatili unyamazishwavyo.

625:6 Mt 22:4; Mit 9:2; Dan 7:14; Mwa 29:22; Za 36:8Juu ya mlima huu Bwana Mwenye Nguvu Zote ataandaa

karamu ya vinono kwa mataifa yote,

karamu ya mvinyo wa zamani,

nyama nzuri sana na divai zilizo bora sana.

725:7 2Kor 3:15-16; Efe 4:8; 1:17; Ay 4:9Juu ya mlima huu ataharibu

sitara ihifadhiyo mataifa yote,

kile kifuniko kifunikacho mataifa yote,

825:8 Hos 13:14; 1Kor 15:54-55; Yer 31:16; Ufu 7:14-17; Ebr 2:14; Isa 26:19yeye atameza mauti milele.

Bwana Mwenyezi atafuta machozi katika nyuso zote;

ataondoa aibu ya watu wake duniani kote.

Bwana amesema hili.

925:9 Isa 40:9; Yer 14:8; Za 20:5; Kum 32:43; Isa 2:11; 49:25-26; Za 145:19Katika siku ile watasema,

“Hakika huyu ndiye Mungu wetu;

tulimtumaini, naye akatuokoa.

Huyu ndiye Bwana, tuliyemtumaini;

sisi tushangilie na kufurahia katika wokovu wake.”

1025:10 Mwa 19:37; Hes 21:29; Kum 23:6; Isa 11:14; Amo 2:1-2Mkono wa Bwana utatulia juu ya mlima huu,

bali Moabu atakanyagwa chini

kama majani makavu yakanyagwavyo kwenye shimo la mbolea.

1125:11 Isa 5:25; 14:26; Law 26:19; Ay 40:12; Isa 2:10-17; 16:14Watakunjua mikono yao katikati yake,

kama vile mwogeleaji akunjuavyo mikono yake ili aogelee.

Mungu atashusha kiburi chao

licha ya ujanja wa mikono yao.

1225:12 Ay 40:11; Isa 26:5; Yer 51:44; Isa 2:15Atabomoa kuta ndefu za maboma yako

na kuziangusha chini,

atazishusha chini ardhini,

mpaka mavumbini kabisa.