Isaya 23 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 23:1-18

Unabii Kuhusu Tiro

123:1 Zek 9:2-4; Amo 1:9-10; Eze 26:1-21; Mwa 10:4; 1Fal 10:22; Yos 19:29; Yer 47:4Neno kuhusu Tiro:

Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi!

Kwa kuwa Tiro imeangamizwa,

imeachwa bila nyumba wala bandari.

Kuanzia nchi ya Kitimu23:1 Kitimu hapa ni Kipro, kisiwa katika Bahari ya Mediterania.

neno limewajia.

223:2 Ay 2:13; Eze 27:1-24; Amu 1:31Nyamazeni kimya, enyi watu wa kisiwani,

pia ninyi wafanyabiashara wa Sidoni,

ambao mabaharia wamewatajirisha.

323:3 Isa 19:7; Za 83:7; Eze 27:3; Mwa 41:5Kwenye maji makuu

nafaka za Shihori zilikuja;

mavuno ya Naili yalikuwa mapato ya Tiro,

naye akawa soko la mataifa.

423:4 Mwa 10:15, 19Uaibishwe ee Sidoni, nawe ee ngome la bahari,

kwa kuwa bahari imesema:

“Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa wala sijapata kuzaa,

wala sijapata kulea wana wala kutunza mabinti.”

523:5 Eze 30:9; 26:17-18Habari ifikapo Misri,

watakuwa katika maumivu makuu kwa ajili ya taarifa kutoka Tiro.

623:6 Mwa 10:4Vukeni mpaka Tarshishi,

ombolezeni, enyi watu wa kisiwani.

723:7 Isa 5:14; 32:13; 22:2; Eze 26:13; Isa 23:12Je, huu ndio mji wenu uliojaa sherehe,

mji wa zamani, zamani kabisa

ambao miguu yake imeuchukua

kufanya makao nchi za mbali sana?

823:8 Isa 2:12; Eze 28:2; 1Tim 3:4; Nah 3:16; Eze 28:5; Ufu 18:23Ni nani amepanga hili dhidi ya Tiro,

mji utoao mataji,

ambao wafanyabiashara wake ni wana wa mfalme

na wachuuzi wake ni watu mashuhuri wa dunia?

923:9 Ay 40:11; Isa 13:11; 5:13; Eze 27:3; Isa 14:24; 9:15Bwana Mwenye Nguvu Zote ndiye alipanga jambo hili,

ili kukishusha kiburi cha utukufu wote

na kuwanyenyekesha wale wote

ambao ni mashuhuri duniani.

10Ee Binti Tarshishi,

pita katika nchi yako kama vile Mto Naili

kwa kuwa huna tena bandari.

1123:11 Kut 14:21; Eze 26:4; Zek 9:3-4; Za 46:6Bwana amenyoosha mkono wake juu ya bahari

na kuzifanya falme zake zitetemeke.

Ametoa amri kuhusu Kanaani

kwamba ngome zake ziangamizwe.

1223:12 Ufu 18:22; Sef 3:14; Zek 2:10; Isa 37:22; Yer 14:17; Mao 2:13; Mwa 10:4Alisema, “Usizidi kufurahi,

ee Bikira Binti Sidoni, sasa umepondwa!

“Simama, vuka uende Kitimu;

hata huko hutapata pumziko.”

1323:13 Isa 43:14; Yer 51:12; Za 74:14; Isa 18:6Tazama katika nchi ya Wakaldayo,

watu hawa ambao sasa hawaonekani kama wapo!

Waashuru wameifanya nchi hiyo

kuwa mahali pa viumbe wa jangwani.

Wamesimamisha minara yao ya vita kuuzunguka,

wameziteka ngome zake na kuziacha tupu

na kuufanya kuwa magofu.

1423:14 Mwa 10:4; Isa 2:16; Eze 27:25; 1Fal 10:22Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi;

ngome yenu imeangamizwa!

1523:15 Yer 25:22; Za 90:10Wakati huo Tiro utasahauliwa kwa miaka sabini, muda wa maisha ya mfalme. Lakini mwisho wa miaka hiyo sabini, itakuwa kwa Tiro kama ilivyo katika wimbo wa kahaba:

1623:16 Mit 7:10“Twaa kinubi, tembea mjini kote,

ewe kahaba uliyesahauliwa;

piga kinubi vizuri, imba nyimbo nyingi,

ili upate kukumbukwa.”

1723:17 Kum 23:17-18; Mwa 10:15-19; Ufu 17:1; 18:3-9; Eze 16:26; Yer 25:26; Nah 3:4Mwishoni mwa miaka sabini, Bwana atashughulika na Tiro. Naye atarudia ajira yake ya ukahaba, na atafanya biashara yake na falme zote juu ya uso wa dunia. 1823:18 Yos 6:17-19; Za 72:10; Zek 14:20-21; Isa 61:6; Mik 4:13; Kut 28:36; Isa 18:7; 60:5-9; Amo 1:9-10Lakini faida na mapato yake yatawekwa wakfu kwa Bwana; hayatahifadhiwa wala kufichwa. Faida zake zitakwenda kwa wale wakaao mbele za Bwana kwa ajili ya chakula tele na mavazi mazuri.