Isaya 22 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 22:1-25

Unabii Kuhusu Yerusalemu

122:1 Za 125:2; Yoe 3:2-14; Yos 2:8; Isa 13:1; Yer 48:38; 21:13Neno kuhusu Bonde la Maono:

Nini kinachokutaabisha sasa,

kwamba ninyi nyote mmepanda juu ya mapaa?

222:2 Isa 5:14; 32:13; Eze 22:5; Isa 21:5; 10:4; 2Fal 25:3Ewe mji uliojaa ghasia,

ewe mji wa makelele na sherehe!

Watu wenu waliokufa hawakuuawa kwa upanga,

wala hawakufa vitani.

322:3 Isa 13:14; 2Fal 25:6Viongozi wako wote wamekimbia pamoja,

wamekamatwa bila kutumia upinde.

Ninyi nyote mliokamatwa mlichukuliwa wafungwa pamoja,

mlikimbia wakati adui alipokuwa bado mbali.

422:4 Mao 1:16; Lk 19:41; Yer 9:1; Eze 21:6; Isa 15:3; Lk 19:41Kwa hiyo nilisema, “Geukia mbali nami,

niache nilie kwa uchungu.

Usijaribu kunifariji

juu ya maangamizi ya watu wangu.”

522:5 Amo 5:18-20; Es 3:15; Sef 1:15; Isa 2:12; Ay 40:12; 2Sam 22:43; Eze 8:17-18; 13:14; Mao 1:5Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayo siku

ya ghasia, ya kukanyaga, na ya kuogofya

katika Bonde la Maono,

siku ya kuangusha kuta

na ya kupiga kelele mpaka milimani.

622:6 Isa 21:2; 2Fal 16:9; Yer 51:56; 49:35; Za 46:9Elamu analichukua podo,

pamoja na waendesha magari ya vita na farasi.

Kiri anaifungua ngao.

722:7 Yos 15:18; 2Nya 32:1-2Mabonde yako yaliyo mazuri sana yamejaa magari ya vita,

nao wapanda farasi wamewekwa kwenye malango ya mji;

822:8 2Nya 32:5; 1Fal 7:2; Isa 2:12ulinzi wa Yuda umeondolewa.

Nawe ulitazama siku ile

silaha katika Jumba la Kifalme la Mwituni,

922:9 2Fal 18:17; 2Nya 32:4-5; Wim 4:4; 2Fal 20:20mkaona kuwa Mji wa Daudi

una matundu mengi katika ulinzi wake,

mkaweka akiba ya maji

kwenye Bwawa la Chini.

1022:10 Yer 33:4; 2Nya 32:15; 32:5; Yer 33:4Mlihesabu majengo katika Yerusalemu

nanyi mkabomoa nyumba ili kuimarisha ukuta.

1122:11 Yer 39:4; Neh 3:16; 2Fal 25:4; 19:25; 1Sam 12:24Mlijenga bwawa la maji katikati ya kuta mbili

kwa ajili ya maji ya Bwawa la Zamani,

lakini hamkumtazama Yule aliyelitengeneza,

au kuwa na heshima kwa Yule aliyeubuni tangu zamani za kale.

1222:12 Yoe 2:17; Law 13:40; Mik 1:16; Isa 3:24; Yoe 1:9-13Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,

aliwaita siku ile

ili kulia na kuomboleza,

kungʼoa nywele zenu na kuvaa nguo ya gunia.

1322:13 Mhu 8:15; Isa 5:12; 21:5; Lk 17:26-29; 1Kor 15:32; 1Sam 25:36; Isa 28:7-8Lakini tazama, kuna furaha na sherehe,

kuchinja ngʼombe na kuchinja kondoo,

kula nyama na kunywa mvinyo!

Mnasema, “Tuleni na kunywa,

kwa kuwa kesho tutakufa!”

1422:14 Eze 24:13; Isa 5:9; 1Sam 2:25; Isa 13:11; 30:13-14; 1Sam 3:14Bwana Mwenye Nguvu Zote amelifunua hili nikiwa ninasikia: Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, asema: “Mpaka siku ya kufa kwenu, dhambi hii haitafanyiwa upatanisho.”

1522:15 2Fal 6:30; 18:18; Mwa 41:40; Isa 36:3; 1Fal 4:6Hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, asemalo:

“Nenda ukamwambie huyu wakili Shebna,

ambaye ni msimamizi wa jumba la kifalme:

1622:16 Mt 27:60; Hes 32:42Unafanya nini hapa, na ni nani aliyekupa ruhusa

kujikatia kaburi lako mwenyewe,

ukichonga kaburi lako mahali palipo juu,

na kutoboa kwa patasi mahali pako pa kupumzikia katika mwamba?

1722:17 Yer 10:18; 13:18; 22:26“Jihadhari, Bwana yu karibu kukukamata thabiti,

na kukutupa mbali, ewe mtu mwenye nguvu.

1822:18 Ay 18:11; Isa 14:19; Mwa 41:43Atakuvingirisha uwe kama mpira

na kukutupa katika nchi kubwa.

Huko ndiko utakakofia,

na huko ndiko magari yako ya vita ya fahari yatabakia,

wewe unayeifedhehesha nyumba ya bwana wako!

1922:19 Za 52:5; Lk 16:3Nitakuondoa kutoka kazi yako,

nawe utaondoshwa kutoka nafasi yako.

2022:20 2Fal 18:18“Katika siku ile, nitamwita mtumishi wangu, Eliakimu mwana wa Hilkia. 2122:21 Ay 29:16Nitamvika joho lako, nami nitamfunga mshipi wako kiunoni mwake, na kumkabidhi mamlaka yako. Yeye atakuwa baba kwa wale wanaoishi Yerusalemu na kwa nyumba ya Yuda. 2222:22 1Nya 9:27; Mt 16:19; Ay 12:14; Ufu 3:7; Isa 7:2Nitaweka mabegani mwake ufunguo wa nyumba ya Daudi. Kile afunguacho hakuna awezaye kufunga, na kile afungacho hakuna awezaye kufungua. 2322:23 Eze 15:3; Zek 10:4; Ezr 9:8; Ay 6:25; 1Sam 2:7-8; Ay 36:7Nitamgongomea kama kigingi kilicho mahali palipo imara, naye atakuwa kiti cha enzi cha heshima kwa ajili ya nyumba ya baba yake. 24Utukufu wote wa jamaa yake utakuwa juu yake: Watoto wa jamaa hiyo na machipukizi yake, vyombo vyake vyote vidogo, tangu bakuli hadi magudulia yote.”

2522:25 Isa 46:11; Mik 4:4Bwana Mwenye Nguvu Zote asema, “Katika siku ile, kigingi kilichogongomewa mahali imara kitaachia njia. Kitakatwa, nacho kitaanguka na mzigo ulioningʼinia juu yake utaanguka chini.” Bwana amesema.