Isaya 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 2:1-22

Mlima Wa Bwana

(Mika 4:1-3)

12:1 Isa 1:1Hili ndilo aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu:

22:2 Dan 2:35; 11:45; Yoe 3:17; Mdo 2:17; Isa 11:9; 65:9; Zek 14:10; Yer 16:19Katika siku za mwisho

mlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwa

kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote,

utainuliwa juu ya vilima,

na mataifa yote yatamiminika huko.

32:3 Zek 8:21; Lk 24:47; Yn 4:22; Isa 33:22; 45:23; Yer 3:17; Kum 33:19Mataifa mengi yatakuja na kusema,

“Njooni, twendeni mlimani mwa Bwana,

kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo.

Atatufundisha njia zake,

ili tuweze kuenenda katika mapito yake.”

Sheria itatoka Sayuni,

neno la Bwana litatoka Yerusalemu.

42:4 Hos 2:18; Yer 30:11; Za 96:13; 51:4; 46:9; Yoe 3:10; Mwa 49:10; Zek 9:10Atahukumu kati ya mataifa

na ataamua migogoro ya mataifa mengi.

Watafua panga zao ziwe majembe,

na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi.

Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine,

wala hawatajifunza vita tena.

52:5 Isa 60:19-20; 1Yn 1:5-7; Isa 58:1; 60:1Njooni, enyi nyumba ya Yakobo,

tutembeeni katika nuru ya Bwana.

Siku Ya Bwana

62:6 Kum 18:10, 14; 31:17; Yer 12:7; 2Nya 16:7; Isa 44:25; 2Fal 16:7; Kum 31:17Umewatelekeza watu wako,

nyumba ya Yakobo.

Wamejaa ushirikina utokao Mashariki,

wanapiga ramli kama Wafilisti

na wanashikana mikono na wapagani.

72:7 Mwa 41:43; Kum 17:16; Mik 5:10; Za 17:14; Isa 31:1; Kum 17:17Nchi yao imejaa fedha na dhahabu,

hakuna mwisho wa hazina zao.

Nchi yao imejaa farasi,

hakuna mwisho wa magari yao.

82:8 Isa 10:9-11; 17:8; 44:17; Ufu 9:20; 2Nya 32:19; Mik 5:13; Isa 44:17; Za 135:15Nchi yao imejaa sanamu,

wanasujudia kazi za mikono yao,

vitu vile vidole vyao vimevitengeneza.

92:9 Za 62:9; Isa 13:11; 5:15; 2:11, 17; Hes 4:5; Neh 4:5Kwa hiyo mwanadamu atashushwa

na binadamu atanyenyekezwa:

usiwasamehe.

102:10 Ufu 6:15-16; Nah 3:11; Za 145:12; Isa 2:19; 2The 1:9Ingieni kwenye miamba,

jificheni ardhini

kutokana na utisho wa Bwana

na utukufu wa enzi yake!

112:11 Isa 24:21-23; 37:23; 10:12; 5:15; Eze 31:10; Oba 1:8; Neh 9:29; Ay 40:11; Za 46:10; Hab 2:5Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa

na kiburi cha wanadamu kitashushwa,

Bwana peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo.

122:12 Za 76:12; 59:12; Eze 7:7; Ay 40:11; Isa 13:6-9; 34:8; Yer 30:7; Mao 1:12; 2Sam 22:28; Yoe 1:15; Amo 5:18Bwana Mwenye Nguvu Zote anayo siku aliyoiweka akiba

kwa wote wenye kujivuna na wenye kiburi,

kwa wote wanaojikweza

(nao watanyenyekezwa),

132:13 Amu 9:15; Isa 10:33, 34; 29:17; Eze 27:5; Za 22:12; Zek 11:2kwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana,

na mialoni yote ya Bashani,

142:14 Isa 30:25; 40:4kwa milima yote mirefu

na vilima vyote vilivyoinuka,

152:15 Isa 25:2, 12; 30:25; 32:14; 33:18; Sef 1:16kwa kila mnara ulio mrefu sana

na kila ukuta wenye ngome,

162:16 Mwa 10:4; 1Fal 10:22; 9:26kwa kila meli ya biashara,2:16 Au: ya Tarshishi (ona pia 1Fal 10:22; 22:48; 2Nya 9:21; 20:36; Isa 60:9.)

na kila chombo cha baharini cha fahari.

172:17 2Sam 22:28; Ay 40:112:17 Nah 3:13; Ebr 10:31; Kum 2:25; Isa 11:10, 15Majivuno ya mwanadamu yatashushwa,

na kiburi cha wanadamu kitanyenyekezwa,

Bwana peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo,

182:18 Kum 9:21; Mik 5:13; Eze 36:25; Isa 21:9; Yer 10:11; 1Sam 5:2nazo sanamu zitatoweka kabisa.

192:19 Hos 10:8; Nah 1:3-6; Ay 9:6; 30:9; Ebr 12:26; Hab 3:6; Amu 6:2; Isa 7:19; 14:16; Ay 30:6; Lk 23:30; Ufu 6:15Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba,

na kwenye mahandaki ardhini

kutokana na utisho wa Bwana

na utukufu wa enzi yake,

ainukapo kuitikisa dunia.

202:20 Law 11:19; Eze 36:25; 7:19-20; 14:6; Ufu 9:20; Isa 2:11; Ay 22:24Siku ile, watu watawatupia

panya na popo

sanamu zao za fedha na za dhahabu,

walizozitengeneza ili waziabudu.

212:21 Kut 33:22; Za 145:12; Isa 33:10; 2:19Watakimbilia kwenye mapango miambani

na kwenye nyufa za miamba

kutokana na utisho wa Bwana

na utukufu wa enzi yake,

ainukapo kuitikisa dunia.

222:22 Mit 23:4; Yer 17:5; Yak 4:14; Ay 12:19; Za 119:8-9; Isa 51:12; 40:15; Za 18:42; 118:6, 8; 146:3Acheni kumtumainia mwanadamu,

ambaye hana kitu ila pumzi katika pua zake.

Yeye ana thamani gani?