Isaya 19 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 19:1-25

Unabii Kuhusu Misri

119:1 Yer 43:12; Yoe 3:19; Kut 12:12; 2Sam 22:10; Yos 2:11; Isa 20:3; Kum 10:14; Isa 13:1Neno kuhusu Misri:

Tazama, Bwana amepanda juu ya wingu liendalo kwa haraka

naye anakuja Misri.

Sanamu za Misri zinatetemeka mbele yake,

nayo mioyo ya Wamisri inayeyuka ndani yao.

219:2 Amu 7:22; 12:4; Mk 13:8; Mt 10:21, 36; 24:7; 2Nya 15:6; Lk 21:10“Nitamchochea Mmisri dhidi ya Mmisri,

ndugu atapigana dhidi ya ndugu,

jirani dhidi ya jirani,

mji dhidi ya mji,

ufalme dhidi ya ufalme.

319:3 Law 19:31; Dan 2:2, 10; Za 18:45; Ay 5:12; 2Nya 10:13; Isa 47:13Wamisri watakufa moyo,

na nitaibatilisha mipango yao.

Watatafuta ushauri kwa sanamu na kwa roho za waliokufa,

kwa waaguzi na kwa wale waongeao na mizimu.

419:4 Yer 46:26; Eze 32:11; 29:19; Isa 20:4Nitawatia Wamisri

mikononi mwa bwana mkatili

na mfalme mkali atatawala juu yao,”

asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote.

519:5 Isa 44:27; Yer 50:38; 2Sam 14:14Maji ya mito yatakauka,

chini ya mto kutakauka kwa jua.

619:6 Kut 7:18; Eze 30:12; Isa 37:25; 15:6; Mwa 41:2; Ay 8:11Mifereji itanuka;

vijito vya Misri vitapungua

na kukauka.

Mafunjo na nyasi vitanyauka,

719:7 Kum 29:23; Isa 23:3; Zek 10:11; Hes 11:5pia mimea iliyoko kando ya Mto Naili,

pale mto unapomwaga maji baharini.

Kila shamba lililopandwa kando ya Mto Naili litakauka,

litapeperushwa na kutoweka kabisa.

819:8 Hes 11:5; Amo 4:2; Hab 1:15; Eze 47:10Wavuvi watalia na kuomboleza,

wale wote watupao ndoano katika Mto Naili,

watadhoofika kwa majonzi.

919:9 Mit 7:16; Eze 16:10; 27:7; Yos 2:10Wale watu wafanyao kazi ya kitani kilichochambuliwa watakata tamaa,

wafumaji wa kitani safi watavunjika moyo.

10Wafanyao kazi ya kufuma nguo watahuzunishwa,

nao vibarua wataugua moyoni.

1119:11 Hes 13:22; 1Fal 4:30; Mdo 7:22; Mwa 41:37Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa,

washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga.

Unawezaje kumwambia Farao,

“Mimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima,

mwanafunzi wa wafalme wa zamani”?

1219:12 1Kor 1:20; Isa 41:22-23; Rum 9:17; Isa 14:24Wako wapi sasa watu wako wenye hekima?

Wao wakuonyeshe na kukufahamisha

ni nini Bwana Mwenye Nguvu Zote

amepanga dhidi ya Misri.

1319:13 Yer 2:16; Hos 9:6; Hes 13:22; Yer 46:14-19; Eze 30:13-16; Za 118:22Maafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu,

viongozi wa Memfisi19:13 Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu. wamedanganyika,

walio mawe ya pembe ya taifa lake

wameipotosha Misri.

1419:14 Mit 12:8; Mt 17:17; Za 107:27Bwana amewamwagia

roho ya kizunguzungu;

wanaifanya Misri iyumbayumbe

katika yale yote inayoyafanya,

kama vile mlevi ayumbayumbavyo

katika kutapika kwake.

1519:15 Isa 9:14Misri haiwezi kufanya kitu chochote,

cha kichwa wala cha mkia,

cha tawi la mtende wala cha tete.

1619:16 Isa 2:17; 11:10; Nah 3:13; Kum 2:25Katika siku ile Wamisri watakuwa kama wanawake. Watatetemeka kwa hofu mbele ya mkono wa Bwana Mwenye Nguvu Zote anaoinua dhidi yao. 1719:17 Mwa 35:5; Isa 14:24Nayo nchi ya Yuda itawatia hofu Wamisri, kila mmoja atakayetajiwa Yuda ataingiwa na hofu, kwa sababu ya kile ambacho Bwana Mwenye Nguvu Zote anapanga dhidi yao.

1819:18 Za 22:27; Yer 4:2; 43:13; Isa 10:20; 24:12; 32:19; Sef 3:9; Yer 44:1; Isa 48:1Katika siku hiyo miji mitano ya Misri, itazungumza lugha ya Kanaani, na kuapa kumtii Bwana Mwenye Nguvu Zote. Mji mmojawapo utaitwa Mji wa Uharibifu.19:18 Yaani Heliopoli (Mji wa Jua).

1919:19 Yos 22:10; Kut 24:4; Za 68:18; Mwa 12:7; 28:18; Isa 10:20; Za 68:31Katika siku hiyo patakuwepo madhabahu ya Bwana katikati ya Misri na mnara wa kumbukumbu kwa Bwana kwenye mpaka wa Misri. 2019:20 Isa 25:9; 49:24-26; Yos 4:20; Mwa 21:30; Amu 2:18; Kum 28:29Itakuwa alama na ushahidi kwa ajili ya Bwana Mwenye Nguvu Zote katika nchi ya Misri. Watakapomlilia Bwana kwa sababu ya watesi wao, Mungu atawapelekea mwokozi na mtetezi, naye atawaokoa. 2119:21 Isa 11:9; 43:10; 56:7; Mwa 27:29; Za 86:9; Hes 30:2; Kum 23:21Hivyo Bwana atajijulisha mwenyewe kwa Wamisri, nao katika siku hiyo watamkubali Bwana. Wataabudu kwa kumtolea dhabihu na sadaka za nafaka, watamwekea Bwana nadhiri na kuzitimiza. 2219:22 Kut 12:23; 11:10; Ebr 12:11; Eze 33:11; Yoe 2:13; Kum 32:39; Isa 45:14; Hos 10:2Bwana ataipiga Misri kwa tauni; atawapiga na kuwaponya. Watamgeukia Bwana, naye atayasikia maombi yao na kuwaponya.

2319:23 Isa 11:15-16; 20:6; 27:13; 66:23; Mik 7:12; Mwa 27:29Katika siku hiyo kutakuwepo na njia kuu kutoka Misri hadi Ashuru. Waashuru watakwenda Misri, na Wamisri watakwenda Ashuru. Wamisri na Waashuru wataabudu pamoja. 2419:24 Isa 11:11; Mwa 12:2Katika siku hiyo Israeli itakuwa ya tatu, pamoja na Misri na Ashuru, nao watakuwa baraka kwa dunia. 2519:25 Za 87:4; 100:3; Efe 2:10; Kut 34:9; Yer 30:22; Hos 2:23; Mwa 12:3; Isa 29:23; 43:7Bwana Mwenye Nguvu Zote atawabariki, akisema, “Baraka iwe kwa Misri watu wangu, kwa Ashuru kazi ya mikono yangu, na kwa Israeli urithi wangu.”