Isaya 18 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 18:1-7

Unabii Dhidi Ya Kushi

118:1 Mwa 10:6; Sef 2:12; Isa 5:8; Za 68:31; Eze 29:10; Oba 1:1Ole kwa nchi ya mvumo wa mabawa,18:1 Au: wa nzige.

kando ya mito ya Kushi,

218:2 Mwa 10:8-9; 2Nya 12:3; Kut 2:3; Ay 9:26; Mwa 41:14iwapelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari

kwa mashua za mafunjo juu ya maji.

Nendeni, wajumbe wepesi,

kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo,

kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu,

taifa gomvi lenye lugha ngeni,

ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito.

318:3 Za 60:4; Yer 4:21; Za 33:8; Isa 5:26; 5:26; 31:9; Yos 6:21; Amu 3:27Enyi mataifa yote ya ulimwengu,

ninyi mnaoishi duniani

wakati bendera itakapoinuliwa milimani,

mtaiona,

nayo tarumbeta itakapolia,

mtaisikia.

418:4 Hos 5:15; 2Sam 1:21; Za 133:3; Isa 64:12; 26:21; Amu 5:31; Za 18:12; Isa 26:19Hili ndilo Bwana aliloniambia:

“Nitatulia kimya na kutazama

kutoka maskani yangu,

kama joto linalometameta katika mwanga wa jua,

kama wingu la umande

katika joto la wakati wa mavuno.”

518:5 Isa 17:10-11; Eze 17:6; Isa 10:33Kwa maana, kabla ya mavuno,

wakati wa kuchanua ukishapita

na maua yakawa zabibu zinazoiva,

atayakata machipukizi kwa mundu wa kupogolea matawi,

naye atakata na kuyaondoa matawi yaliyopanuka.

618:6 Yer 7:33; Eze 32:4; 39:17; Isa 37:36; 8:8; 56:9Yote yataachwa kwa ajili ya ndege wawindao wa mlimani

na wanyama pori,

ndege watajilisha juu yake wakati wote wa kiangazi,

nao wanyama pori wakati wote wa masika.

718:7 Sef 3:10; Za 68:31; 2Nya 9:24; Isa 60:7; Mwa 41:4; 41:14Wakati huo matoleo yataletwa kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote

kutoka kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo,

kutoka kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu,

kutoka taifa gomvi lenye lugha ngeni,

ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito,

matoleo yataletwa katika Mlima Sayuni, mahali pa Jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote.