Isaya 16 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 16:1-14

Hali Ya Kukata Tamaa Ya Moabu

116:1 Isa 10:32; Amu 1:36; 2Fal 14:7; 2Nya 32:23; 2Fal 3:4; Oba 1:3Pelekeni wana-kondoo kama ushuru

kwa mtawala wa nchi,

Kutoka Sela, kupitia jangwani,

hadi mlima wa Binti Sayuni.

216:2 Mit 27:8; Hes 21:13-14; Yer 48:40; Hes 21:29Kama ndege wanaopapatika

waliofukuzwa kutoka kwenye kiota,

ndivyo walivyo wanawake wa Moabu

kwenye vivuko vya Arnoni.

316:3 1Fal 18:4“Tupeni shauri,

toeni uamuzi.

Wakati wa adhuhuri,

fanyeni kivuli chenu kama usiku.

Waficheni watoro,

msisaliti wakimbizi.

416:4 Isa 55:7; 9:4; 2:2-4Waacheni watoro wa Moabu wakae pamoja nanyi;

kuweni mahali pao pa salama ili kuepuka mharabu.”

Mtesi atafikia mwisho na maangamizi yatakoma,

aletaye vita atatoweka kutoka nchi.

516:5 1Sam 13:14; Mik 4:7; Isa 7:2; Dan 7:14; Mit 20:28; Isa 9:7; Lk 1:32Kwa upendo kiti cha enzi kitaimarishwa,

kwa uaminifu mtu ataketi juu yake,

yeye atokaye nyumba ya Daudi:

yeye ambaye katika kuhukumu hutafuta haki,

na huhimiza njia ya haki.

616:6 Eze 25:8; Yer 25:21; Law 26:19; Ay 20:6; Sef 2:8; Yer 49:16; Amo 2:1Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu:

kiburi chake cha kujivuna na udanganyifu,

kiburi chake na ufidhuli wake,

lakini majivuno yake si kitu.

716:7 1Nya 16:3; 2Fal 3:25; Yer 48:20; 49:3; Isa 13:6Kwa hiyo Wamoabu wanaomboleza,

wanaiombolezea Moabu kwa pamoja.

Wanaomboleza na kuhuzunika

kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi.

816:8 Ay 8:16; Hes 21:32; 21:25; Isa 15:6; 5:2; Ay 8:16; Za 80:11Mashamba ya Heshboni yananyauka,

pia na mizabibu ya Sibma.

Watawala wa mataifa

wamekanyaga mizabibu iliyo mizuri sana,

ambayo ilipata kufika Yazeri

na kuenea kuelekea jangwani.

Machipukizi yake yalienea

yakafika hadi baharini.

916:9 Isa 15:3; Eze 27:31; Yer 40:12; Ay 7:3; Hes 32:3; Ezr 3:13Hivyo ninalia kama Yazeri aliavyo,

kwa ajili ya mizabibu ya Sibma.

Ee Heshboni, ee Eleale,

ninakulowesha kwa machozi!

Kelele za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva

na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa.

1016:10 Isa 24:7-8; Amu 9:27; Ay 24:11; Yer 25:30; Isa 5:2Furaha na shangwe zimeondolewa

kutoka mashamba ya matunda;

hakuna yeyote aimbaye wala apazaye sauti

katika mashamba ya mizabibu;

hakuna yeyote akanyagaye zabibu shinikizoni,

kwa kuwa nimekomesha makelele.

1116:11 Isa 15:5; Hos 11:8; Flp 2:1; Ay 30:31; Isa 63:15Moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama kinubi,

nafsi yangu yote kwa ajili ya Kir-Haresethi.

1216:12 Za 115:4-7; 1Kor 8:4; Hes 22:4; Isa 15:2; 1Fal 11:7; 18:29Wakati Moabu anapojitokeza mahali pake pa juu,

anajichosha mwenyewe tu;

anapokwenda mahali pake pa kuabudia miungu ili kuomba,

haitamfaidi lolote.

13Hili ndilo neno ambalo Bwana ameshasema kuhusu Moabu. 1416:14 Isa 25:10; Yer 48:42; Kum 15:18; 13:16; Isa 20:3; 37:30; Law 19:13Lakini sasa Bwana anasema: “Katika miaka mitatu, kama vile mtumishi aliyefungwa na mkataba angeihesabu, fahari ya Moabu na watu wake wengi watadharauliwa, nao walionusurika watakuwa wachache sana, tena wanyonge.”