Unabii Dhidi Ya Babeli
113:1 Isa 14:28; 21:9; 48:14; Ufu 14:8; Mwa 10:10; Mal 1:1; Isa 14:4; 46:1-2Neno kuhusu Babeli ambalo Isaya mwana wa Amozi aliliona:
213:2 Za 20:5; 50:2; Yer 51:27; 51:58; 50:2; Isa 24:12; 45:2; 24:2Twekeni bendera juu ya mlima usio na kitu,
wapazieni sauti,
wapungieni mkono waingie
katika malango ya wenye heshima.
313:3 Yer 51:11; Yoe 3:11; Za 149:2; Isa 21:2; Kum 5:28; Ay 40:11Nimewaamuru watakatifu wangu;
nimewaita mashujaa wangu waitimize hasira yangu:
wale wanaoshangilia ushindi wangu.
413:4 Yoe 3:14; Za 46:6; Isa 42:13; 47:4; Yer 50:41Sikilizeni kelele juu ya milima,
kama ile ya umati mkubwa wa watu!
Sikilizeni, makelele katikati ya falme,
kama mataifa yanayokusanyika pamoja!
Bwana Mwenye Nguvu Zote anakusanya
jeshi kwa ajili ya vita.
513:5 Yos 6:17; Isa 5:26; 34:2; 54:16; 10:25; 34:2; Yer 50:25Wanakuja kutoka nchi za mbali sana,
kutoka miisho ya mbingu,
Bwana na silaha za ghadhabu yake,
kuangamiza nchi yote.
613:6 Amo 5:18; Eze 30:2; Yak 5:1; Isa 2:12; 14:31; 10:3; 15:2Ombolezeni, kwa maana siku ya Bwana i karibu,
itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi.13:6 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.
713:7 Eze 21:7; Yos 2:11; 2Fal 19:26; Ay 4:3; Yer 47:3Kwa sababu ya hili, mikono yote italegea,
moyo wa kila mtu utayeyuka.
813:8 Nah 2:10; Yoe 2:6; Za 31:13; Isa 21:4; Za 48:5; Kut 15:14; Mwa 3:16; Yn 16:21Hofu itawakamata,
uchungu na maumivu makali yatawashika,
watagaagaa kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa.
Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake,
nyuso zao zikiwaka kama moto.
913:9 Isa 2:12; Yer 6:23; 51:2; Isa 9:19; 66:16; Yer 25:31; Yoe 3:2Tazameni, siku ya Bwana inakuja,
siku katili, yenye ghadhabu na hasira kali,
kuifanya nchi kuwa ukiwa
na kuwaangamiza wenye dhambi waliomo ndani yake.
1013:10 Kut 10:22; Ufu 8:12; Amo 5:20; Zek 14:7; Ay 9:7; Mt 24:29; Isa 5:30; 24:23Nyota za mbinguni na makundi ya nyota
havitatoa mwanga wake.
Jua linalochomoza litatiwa giza
na mwezi hautatoa nuru yake.
1113:11 Isa 3:11; 26:21; 65:6-7; 49:25-26; Za 125:3; Mit 16:18; Dan 5:23; 4:37; Eze 28:2Nitauadhibu ulimwengu kwa ajili ya uovu wake,
waovu kwa ajili ya dhambi zao.
Nitakomesha majivuno ya wenye kiburi,
na nitakishusha kiburi cha watu wakatili.
1213:12 Isa 4:1; Mwa 10:29Nitawafanya wanadamu kuwa adimu kuliko dhahabu safi,
watakuwa wachache sana kuliko dhahabu ya Ofiri.
1313:13 Hag 2:6; Za 102:26; Isa 9:19; 14:16; 34:4; Mt 24:7; Ay 9:5; 9:6; Mk 13:8Kwa hiyo nitazifanya mbingu zitetemeke,
nayo dunia itatikisika kutoka mahali pake
katika ghadhabu ya Bwana Mwenye Nguvu Zote,
katika siku ya hasira yake iwakayo.
1413:14 Nah 3:7; Yn 10:11; Yer 51:9; 46:16; 4:9; Mit 6:5; Isa 17:13; 21:15; 33:3; Mt 9:36Kama swala awindwaye,
kama kondoo wasio na mchungaji,
kila mmoja atarudi kwa watu wake mwenyewe,
kila mmoja atakimbilia nchi yake ya kuzaliwa.
1513:15 Yer 50:25; 51:4; Isa 14:19Yeyote atakayetekwa atapasuliwa tumbo,
wote watakaokamatwa watauawa kwa upanga.
1613:16 Nah 3:10; Hes 16:27; 13:16; Mwa 34:29; 2Fal 8:12Watoto wao wachanga watavunjwa vipande vipande
mbele ya macho yao;
nyumba zao zitatekwa
na wake zao watatendwa jeuri.
1713:17 2Fal 18:14-16; Mit 19:24-25; Yer 51:11; 50:9, 41Tazama, nitawachochea Wamedi dhidi yao,
ambao hawajali fedha
wala hawafurahii dhahabu.
1813:18 Za 7:12; Isa 41:2; Yer 49:26Mishale yao itawaangusha vijana,
hawatakuwa na huruma kwa watoto wachanga
wala hawataangalia watoto kwa huruma.
1913:19 Dan 4:30; Za 137:8; Ufu 14:8; Mwa 19:24-25; Rum 9:29; Isa 47:5; Dan 2:37-38Babeli, johari ya falme,
utukufu wa kiburi cha Wababeli,13:19 Wababeli hapa maana yake ni Wakaldayo.
itaangushwa na Mungu
kama Sodoma na Gomora.
2013:20 Isa 14:23; 34:10-15; 2Nya 17:11; Yer 51:29, 37-43, 62Hautakaliwa na watu kamwe
wala watu hawataishi humo kwa vizazi vyote.
Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake huko,
hakuna mchungaji atakayepumzisha makundi yake huko.
2113:21 Za 74:14; Ufu 18:2; Yer 14:6; Law 11:16-18; Kum 14:15-17; 2Nya 11:15Lakini viumbe wa jangwani watalala huko,
mbweha watajaza nyumba zake,
bundi wataishi humo
nao mbuzi-mwitu watarukaruka humo.
2213:22 Isa 34:14; Kum 32:25; Yer 48:16; 9:11; Isa 25:2; 32:14; Yer 50:39; Mal 1:3Fisi watalia ndani ya ngome zake,
mbweha ndani ya majumba yake ya kifahari.
Wakati wake umewadia,
na siku zake hazitaongezwa.